SoC01 Mabadiliko katika mfumo wa elimu ni lazima

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 29, 2021
81
158
Huwa ni kawaida kuona vitu vinabadilika kutokana na mabadiliko mbalimbali.

Mfano, mavazi, kutoka kwenye makuti au maganda ya mimea kwenda kwenye kuvaa nguo, jinsi ya ufanyaji kazi, kutoka kwenye utumiaji wa watu kwenda kwenye utumiaji wa mashine, vyombo vya usafiri, kutoka kutembea kwa miguu, kwenda kwa kutumia wanyama na sasa kwenye magari, ndege na meli za kisasa.

Na pia kwenye kilimo, kutoka kwenye ukulima unategemea mvua kwenda kwenye kilimo cha kisasa cha umwagiliaji.

Haya Ni mambo machache ambayo yamebadilika kutokana na mabadiliko mbalimbali hasa mabadiliko sayansi na tekinologia.

Chakushangaza ni jinsi ambavyo elimu yetu ya Tanzania isivyobadilika. Elimu ya Tanzania ya leo ndio ileile tuliyoitumia wakati wa ukoloni. Na tokea wakati huo mpaka Sasa hakuna mabadiliko yoyote yaliotokea. Subiri nikupe mchanganuo wa mfumo wetu wa elimu. Mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na miaka sita na inamchukua miaka saba kwa yeye kumaliza elimu ya msingi. Baada ya hapo atasoma miaka minne katika elimu ya Sekondari, alafu atahitaji miaka mingine miwili kwaajili ya elimu ya kidato cha tano na cha sita. Baada ya hapo miaka mingine mitatu au zaidi ya chuo kikuu kulingana na masomo atakayochagua.
Sasa ukiangalia hapo utagundua kuwa mpaka kijana amalize elimu yake anatumia si chini ya miaka kumi na sita (16). Na hapo hatujajumuisha miaka ambayo atakaa tu mtaani bila ya kupata ajira. Mfumo wetu huu wa elimu unatakiwa ubadilike kwa sababu zifuatazo;

Kwanza, inainyima serikali nguvu kazi, vijana wanatumia mda mwingi sana mashuleni, bila kufanya kazi yoyote. Na wazee ndio ambao wako kazini. Kwa hapa tulipofikia kiuchumi, hebu fikiria itakuwaje na tutafikia wapi Kama tukiweza kutumia nguvu kazi yote ile ambayo inapotea mashuleni?

Pili, Elimu ya utegemezi, kwamba elimu inayotolewna kwa wanafunzi ni elimu ya daftari tu na sio elimu ambayo wanaweza wakaitumia moja kwa moja katika maisha yao, kujikwamua na kuikwamua nchi ya Tanzania na umasikini. Na elimu hii inawaandaa vijana wa kitanzania kuwa waajiriwa, sasa tatizo linakuja kuwa tuna uhaba wa ajira hii elimu inatusaidiaje. Kwa upande wangu naona inatuongezea tatizo, kwasababu inaanda watu ambao hawawezi kufikiria jinsi ya kutengeneza ajira ili kuajiri wengine kitu ambacho Tanzania inahitaji.

Mtu atasema mbona mfumo huu tunaoutumia Tanzania ndio huohuo unaotumika nje ya nchi? Sawa tunautumia mfumo sawa, lakini Cha msingi Cha kuangalia ni je huu mfumo unakidhi mahitaji ya watanzania na Tanzania kiujumla? Au ndo tunasubiria mpaka mzungu aamke abadilishe mfumo wake ndo na sisi tuige? Kwanini sasa tumsubirie mzungu, wakati sisi tunauwezo wa kufanya mabadiliko hayo?

Wazo langu ni kwamba, mfumo wa elimu wa Tanzania uangaliwe tena na kuhusu kubadilisha kwa papo hapo itakuwa ni ngumu lakini inawezekana kubadilisha ratiba. Badala ya wanafunzi (hasa wa vidato na vyuo) kusoma kwanzia asubuhi mpaka jioni, wasome tu kwa masaa kadhaa, kisha masaa mengine wakafanye kazi. Na hii iwe inasimamiwa kuwa kila mwanafunzi awe anasehemu anapofanyia kazi, na awe analipwa pia.

Kwa njia hii Nina uhakika kuwa uchumi hautayumba na tutapunguza matatizo ya wanafunzi kutoweza kumaliza elimu zao kwasababu ya kukosa ada , kwakuwa atakuwa na uwezo wa kujilipia mwenyewe, tatizo la ngono zembe kwakuwa mwanafunzi alihitaji fedha za kujikimu na mahitaji na kwakuwa alizikosa nyumbani akaamua kwenda kwa wanaume au kujiuza na matatizo mengine yanayofanania na hayo.

Na pia kwa kupitia njia hiyo vijana wengi watapata uzoefu katika biashara na kazi na pia watapata pesa ambayo wataitumia kama mitaji ya kuanzisha biashara zao na kuajiri vijana wengine wengi na itapunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Ila Cha muhimu zaidi ni yetu ya Tanzania, kwa kupitia njia hiyo, itapanda sana kiuchumi. Kwakuwa tutakuwa tumeweza kuitumia vizuri hii nguvu kazi ambayo imekuwa ikipotea kwa muda mrefu. Na pia kwasababu tatizo la ajira litapungua sana baada ya vijana kupata mitaji na kuanzisha biashara zao na mengine mengi.

Kila kitu hakina budi kubadika, kwasababu sio mabadiliko yote ni hasi. Na hata mfumo wetu wa elimu hauna budi kubadilika kuendana na hali iliyopo kwa wakati huu, ili tuweze kukua zaidi kiuchumi na kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea katika nchi yetu ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom