Mabadiliko CHADEMA Makao Makuu


Una jazba kweli... haya niambie wapi nimesema mimi ni msomi? Hayo makubwa aliyoyafanya "makubwa" ni yepi zaidi ya kupayuka ovyo kwenye media bila ya substance.

Unajichanganya kama ninayoandika humu ni ya "kijinga" how dare u r replying posts za "kijinga" hii inathibitisha wewe ndio mjinga zaidi!

Nyie kizazi "mpaka kieleweke" nyie ngoja tu
 
Dogo aende shule haraka iwezekanavyo he has a lot of potential!

Ila approach aliyotumia GT hapo juu....!!!!

Too harsh...wote tu binadamu tulioumbwa na Mungu!
 
Mnyika ni mwanaharakati asiyechumia tumbo; kuna vijana wengi ambao wakipata kanafasi kama hako hata asingeomba akasome;angetulia na elimu yake hiyo; lakini kwa chadema nafikiri utaratibu wao kiungozi walau unaangalia maslahi ya wanachama wake hasa ktk swala la elimu ambao hakika ndio ufunguo wa maisha; SO MNYIKA TWAKUSUBIRIA UBUNGO 2010 ukiwa na mambo hayo mapya; umefanya mambo mengi mno mpaka sasa
 

Ubungo anakwenda kupoteza muda wake bure.
 
Tatizo dogo anashindwa kusoma alama za nyakati. Akina Zitto, Mdee et al wameenda shule anachoshindwa kuelewa kuwa hizi roller coaster politics za Bongo inafika wakati zinaparaganyika na baada ya hapo kila mtu na lwake na hapo ndio atakapoona umuhimu wa shule.

Awaangalie akina Dr Lamwai, Marando, Dr Tenga, Dr Limbu et al. Mambo ya siasa yalipoanza kuwaletea miyeyusho wakarudi kwenye fani zao na maisha yanaendelea.

Sasa ni muhimu dogo akajua kuwa hao Chadema wana enjoy their 15 minutes of fame kama ilivyokuwa kwa NCCR, TLP an CUF soon zitakapoisha ndio atajua kuwa hivyo vidingi vilikuwa vinamrostisha tu wakati hao akina Zitto haoo moto mwingi CCM....
 
Naona watu tuna -ve attitude;

Kwanza mtu kuacha uongozi ili akasome ndicho nilichokijua nakumbua ilishawahi kuongelewa humu hata kabla kwa wenye ubongo wa kutunza vema kumbu kumbu zao; na inaeleweka ameenda kusoma;
Naona huu ndiomuda muafaka; ana experience na TZ yote ametembea sana ingawa hiyo shule ilikuwa ndogo kuliko hata wengine hapa mna madegeree lakini LOGIC bwana du zero
Mnyika ameandika makala nyingi na kwa wale waliopitia pitia mambo haya ya wachache wanajua huyu mtu ana kitu fulani kichwani cha ziada kuliko hata maprofessor uchwara kibao wa bongo

Naombeni kama kweli mna nia ya dhati kulijenga taifa tuwape moyo vijana wenye asili ya upambanaji; sio mchumia tumbo yule angekuwa amechukuliwa na mafisadi zamani; alishawahi kumwandikia MSG RA kuwa =WEWE NI FISADI AKIWA BUNGENI; GT unaweza au wewe ndio wale wanaoenda pale kupiga magoti;
SO mie naona tumpe moyo akirudi jukwaani tutampokea na kumpa moyo kuendeleza mapambano ya maisha duni tuliyo nayo asilimia 85% ya WATZ
 
Huyu kijana tutamsemea, tutahisi hili na lile. Lakini kwa kuwa ni mwana JF yeye ndio atatueleza analokusudia baada ya kupokeza kijiti.
 
He he he !! Malunde-Malundi Kula tano mtu wangu
 

Mkuu Malunde-malundi.
Niko pamoja na wewe dogo alikuwa anashusha nondo za uhakika.
J
 


Unataka kusemaje??? Nini kilitokea UDSM? Nakumbuka 2005 wakati anajinadi tumpe jimbo la ubunge alisema angehitimu 2005? Sasa utasemaje awe na degree angalau moja, as if hana!!
 
Ni kijana muaminifu,muadilifu,mchapa kazi,mwerevu anayejiheshimu na kuheshimika ktk jamii yetu,anapenda kusikiliza, kujifunza, ana akili na hekima. Naamini kwa wasifu huu j.j.m ameelimika na kama suala ni degree basi atimize wajibu tu kwa kukamilisha wasifu wa kisomi wa kuhudhuria hadhara za kitaaluma madarasani ili jamii ijiridhishe juu ya usomi wake.

Mimi nimemkubali kama mwanazuoni kwa maono yake kimaandishi na mihadhara ya siasa na jamii. Ninarejea kumbukumbu zangu kuwa huyu j.j ni kama alishawahi kuwepo hapo udsm kabla ya 2005 ila sina hakika.

Tuendelee kujifunza j.j maana tuko wengi wa aina yako na sasa tunarudi madarasani taratibu ili ku shape fikra zetu na pengine tuwe silaha kali zenye kujenga na kuilinda nchi yetu tanzania kwa hoja na maarifa. Kidumu chama cha mapinduzi
 
Badala ya kukaa na kulumbana huku baadhi yetu tukionekana kufurahia wazi wazi suala la JJ kuachwa katika uteuzi huu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, tungekaa na kujiuliza ni nini haswa kimesababisha JJ akaachwa katika hili.

Michango mingi hapa ni kama watu tunakurupuka na kumshambulia huyu kijana huku wengi wetu tukiona kufurahia wazi wazi, kwa nini wanadamu tunakuwa na roho za ajabu badala ya kutakiana mema tunakuwa twafurahia 'alleged downfalls' of others?

Kila mtu anaweza muongelea Mnyika kwa jinsi ambavyo anamfahamu, mimi ntasema Mnyika ni kisima cha 'knowledge.' Wengi tupo hapa tulipo kutokana na juhudi binafsi za Mnyika. He is what he is and we should respect that as it is. Maamuzi ya Chama juu ya Mnyika yana maana kubwa katika kujenga na si kubomoa.

Nawakilisha.
 
Watanzania tunasahau ya kwamba uongozi katika vyama vya kisiasa si 'birthright' ya kiongozi awae yoyote. Na kwamba katiak Chama abacho kinaendeshwa Kidemokrasia, mabadiliko katika Uongozi ni moja kati ya indicators kwamba ndani ya chama Demokrasia ipo.

Tunakosea sana kusema kwamba Mnyika katoswa kwani ukiangalia chama kina wanachama wengi na ni haki ya kila mwanachama kuweza shika nafasi mbali mbali za uongozi, na pia kutolewa katika hizo nafasi. Nafasi zote za uongozi ni dhamana tu.

Na pia jambo lingine la kulitilia maanani ni kwamba huitaji kuwa kiongozi wa ngazi fulani katika chama ili uweze kutimiza majukumu upasayo yatimiza ukiwa kama Mwanachama wa Chadema na Mtanzania. Maana unakuwa na majukumu kwa chama na pia unakuwa na majukumu kwa Taifa lako.

Tuangalie na kukubali kwamba nyakati hazitobaki kama zilivyo na kamwe jana haitokuwa kesho...

Mabadiliko ya Kweli [Kuanzia Nyumbani]
 
kijana ana elimu ya BBA evening programm ya UDSM na alikuwa mwanaharakati mzuri tu wakati yuko hapo na sio mtu wa kwenda CBE tena.
 
kijana ana elimu ya BBA evening programm ya UDSM na alikuwa mwanaharakati mzuri tu wakati yuko hapo na sio mtu wa kwenda CBE tena.


Ndugu Ochu,

Asante sana kwa kuweka sawa kumbukumbu! Maana 2005 kwenye kampeni za Ubunge, Kibangu (Kata ya Makuburi - Ubungo) alijieleza kwamba angehitimu pale Mlimani-UDSM mwaka huo huo. Sasa nilishtuka sana kuona anaongelewa kama vile hana first degree.

Wasiwasi wangu umeisha sasa. Maana ni vizuri vijana wakawa makini sana na hizi siasa za Tanzania. Zinadanganya sana na mwisho wa siku watajikuta wananunua "PhD" kama wenzao wanaopigiwa kelele kila siku.

Na kama anaenda kujiendeleza zaidi, namshauri aende tu kimya kimya kuliko kujitangaza (kisiasa) kwenye media kama tuliokwisha washuhudia na mwisho wa siku mambo yalipowawia magumu huko chuoni wakarudi kimya kimya.

Mnyika songa mbele. Watanzania si watu wa kuwatetea sana. Mwisho wa siku hao unaojidai kuwatetea na kuwaonea huruma saaaana, mwisho wa siku ndiyo watakaokuja kukucheka. Cheza siasa za bongo kwa akili.

Na kama ni kweli kwamba umeomba mwenyewe kuondolewa kwenye uongozi wa chama ili upate muda wa kujiendeleza umetumia busara, maana wahenga walisema "Mshika mbili moja humponyoka". Na mifano dhahiri unaijua wewe mwenyewe; haiko mbali nawe. Ni kama pua na mdomo.
 
Hata mimi kwa ufahamu wangu, JJ Mnyika ni Graduate wa UDSM. Issue ni jee aligraduate?. kama ni kupitia UD, wengi tumepita lakini sio wote waliograduate. Hata James Mbatia ni mwanaharakati ambae alianzia UD lakini hakugraduate.
Mwita Mwikabe aliyeula CHADEMA pia ni Graduate wa UDSM na aliwahi kuwa rais wa DARUSO ni mwanaharakati uchwala na oportunist, hivyo it wont bee long kabla CHADEMA hawajagundua wameuvaa mkenge.
 
Wasifu wa Mnyika hapa chini. Ushauri tu, kwenye masuala ya elimu, kama umeamua kuongelea ulivyopasua O-level, inatakiwa pia uongelee points ulizopata A-level na university. Kama mambo huko kwingine hayakuwa mazuri sana inakuwa safe kuacha kuongelea masuala ya umepata points ngapi. Ukiongelea ya form four, watu wanauliza A-level je? Unakuwa umefungulia maswali mengi badala ya kuyapunguza. Kama ni interview mtu anakuja na maelezo kama hayo, obvious nitakuwa interested kujua huko kwingine ilikuwaje?

 
Ndugu wanaJF,
Heri ya mwaka mpya 2009.

Nimetuiwa ujumbe wa simu kuwa katika JF kuna habari hii ambayo nimeona niisemee.

Sio kweli kwamba John mnyika, aliyekuwa Mkurgenzi wa Vijana Taifa ameondolewa katika uongozi wa chama. Isipokuwa John amethibitishwa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa kuwa huwezi kuwa na Kurgenzi mbili kwa wakati mmoja, basi Kurgenzi wa Vijana imepata Mkurugenzi mpya ambae anasubiri kuthibitishwa na Kamati Kuu ya chama ambae ni Ndugu Halima Mdee(Mb).

Naomba ifahamike kuwa John Mnyika Hajang'olewa CHADEMA. John ni mmoja wa hazina kubwa sana ya chama chetu na kwa muda mrefu ujao atakuwa tegemeo kubwa la chama na Taifa letu. John hajafanya makosa yeyote katika chama ya kustahili kuvuliwa uongozi. Amekuwa mwadilifu sana katika chama na ametoa mchango mkubwa sana katika ujenzi wa Demokrasia katika Taifa letu.
 
Nani alitegemea kitu tofauti na hicho alichokiandika GT???Huyu mkulu ana tatizo la kuruhusu emotions kumtawala either anapofikiri au anapoandika.Huu ni upungufu mkubwa kwa mtu yeyote makini.
BTW;
Vipi kijiwe cha kwa January kinaendeleaje?
 
Wakulu Heshima Mbele!

Kuna wakati Flani nilikuwa Mbele kumsahauri sana mdogo wangu Jojn Mnyika Nini Cha kufanya,Hasa kuhusiana na shule.Na niliyasema haya kwa kuwa niliwahi kusikia kwamba hakumaliza masomo yake ya BBA pale Mlimani na alikuwa akisuasua sana .Tusubir sababu rasmi za kusimamishwa kwake ila nvyojua watampa kazi nyingine,Otherwise CCM watamchukua kijana na kumkabidhi kazi!

Kuhusu Mwita Mwikabe na John Mrema.
Hawa Wawili walikuwa wapinzani sana kipindi Mwita Rais na Mwikabe ni waziri mkuu wa DARUSO.Nakumbuka ilikuwa ikitupa sana taabu kipindi hicho kama Chama kujua nanai atatusaidia wakati migomo ikitokea,Mrema alikuwa ni mtu waCHADEMA na mwita alikuwa upande wetu na hii ni kwa kuwa tu tuliweza akumtoa chama cha NCCR na kumvuta kwetu .


Ila kimsingi mwita alikuwa ni mwanachama wa NCCR na sikumbuki kama alishawahi kurudisha kadi ya Chama hicho.Wote Mwita na john ni Ma-opportunist na hawajui wako CHADEMA kwa ajili ya nini na kwa Maslahi ya nani.

Kuna thread moja ahapa nilishawahi kusoma ikieleza kuhusu mapandikizi ya CCCM katika vyama hivi,Mwita ni mmoja wao na ukianalia kwa undani zaidi hakuna wapinzani wa kweli na wote hawa kina zitto wanakaa pale ili kujiwekea mazingira mazuri kimaisha na hawana lolote.Ulisahwai kuona wapi mtyu anatolewa katika CHama na anahama?Hii inaonehsa ni mtu anayependa Madaraka na siyo kusaidia watanzania

Kinachohitajika ni umoja wa kitaifa tu kutatua matatzio ya watanzania.Kila jimbo lijiunge na kuweka mikakati yao na wasitegeemee mbowe wala Slaa kuja kutatua matatizo yao.Kama tukiweza kuwa na watu wa aina ya wanaTARIME au Mbeya basi tutashinda .Na ushindi utachngiwa na kuwapa mbinu ya nini cha kufanya ili wajikomboe.

Huwa siku zote nasita kusema kwamba Chama au Muungwana wameshidnwa kuwapa watanzania maisha bora,bali ni watendaji wa serikali waliokosa ubunifu ndiyo wanalipeleka Taifa hili kubaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…