Mabadiliko CHADEMA Makao Makuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko CHADEMA Makao Makuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Jan 15, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko CHADEMA Makao Makuu: Mwikabe aula, Mnyika atoswa

  Mabadiliko yafanywa CHADEMA Makao makuu, baada ya kujitoa CCM Mwita Mwikabwe abahatika kwa kuteuliwa mkurugenzi wa sera ya utafiti. Katika utuezi huo, John Mnyika ametoswa kuwa mkurugenzi wa Vijana na nafasi yake imechukuliwa na Halima Mdee(Mbunge wa Viti Maalum). Wengine waliokumbwa na mabadiliko hayo ni Regia Mtema, aliyetolewa uafisa vijana na nafasi yake kuchukuliwa na Ali Chitanda. Regia ameteuliwa kuwa Afisa wa Mafunzo nafasi ambayo ilishikiliwa na Dady Igogo ambaye ameteuliwa kuwa afisa Sheria. Aliyekuwa afisa sera na utafiti Danda Juju yeye amepelekwa Bunge na Halmashauri. Mabadiliko hayo hayahusishi wakurugenzi wengine kama Benson Kigaila, Erasto tumbo na wengine ambao wote wanaendelea na nafasi zao kama kawaida kama inavyoonyeshwa kwenye tovuti ya chama hicho Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Uteuzi huo umeaanza mara moja

  ............ndiyohiyo
   
  Last edited by a moderator: Jan 16, 2009
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Sijasoma katiba ya CHADEMA, hivyo ningetaka kuuliza ni nani kafanya hayo mabadiliko? Je ni Mwenyekiti wa CHADEMA au ni kikao cha chama?

  Kijana wetu Mnyika amefanya nini mpaka kuondolewa? Kwa mawazo yangu strategically sidhani kama Mnyika alikuwa effective. Alikuwa anajihusisha mno na propaganda; ukizidisha inafika mahali watu wanachoka na hawasomi tena.

  CHADEMA wangemsaidia Mnyika kwa kumpeleka kusoma shule ya maana, naamini ni mchapa kazi na hivyo akipunguza mapungufu yake anaweza kuwa effective.
   
 3. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Katika chama hicho uteuzi wa wakurugenzi hufanywa na kamati kuu ya chama kwa mapendekezo ya sekretariati.

  Maafisa wa chama hicho huteuliwa na sekretariati.

  Kamati kuu ya chama hicho huwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, wakati Sekretariati inaongozwa na Katibu Mkuu wa chama.

  Inaelekea huyo dogo ameshindwa kabisa kuongoza vijana wa CHADEMA ndio maana sasa ameteuliwa mpambanaji Halima Mdee. Huyo Mnyika sasa anasugua Benchi

  ......ndiyohiyo
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Yale yale ya CCM kuwazawadia akina Tambwe
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inaelekea Mnyika amechuka study leave kama alivyowahi kudokeza hapo nyuma.
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  "Mwikabe aula, Myika atoswa"....najiuliza huko Chadema ni kipi hicho ambacho watu 'wanakula' mara wanapopata nafasi ya uongozi? ifike mahali jamani mjitofautishe na CCM ma mambo ya 'kuula'!
   
 7. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi hao CHADEMA wanauhakika gani kama huyo Mwikabe sio mamluki wa sisiem?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Inawezekana ni study leave ama ameomba awe na muda zaidi katika kujiandaa kuchukua jimbo la Ubungo ambalo CCM wanataka kumsimamisha Nape Nnauye kupambana naye!!
   
 9. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mabadiliko ni muhimu katika kujenga chama!!!!
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uongozi ni dhamana, leo unao, kesho hauna. Mimi nadhani Mnyika hajatoswa, bali ni mabadiliko ambayo hutokea katika kuongeza tija. Hata kesho na kesho kutwa Mdee naye ataondoka atakuja mwingine. Alikuwepo Mtei, akaja Makani (Bob) na sasa Mbowe.
   
 11. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Labda ni katika kuweka sawa mambo, maana lile tukio la Mbeya Vijijini haliwezi kupita hivi hivi.
   
 12. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Mwikwabe hajateuliwa mkurugenzi, nimeangalia hapa kwenye sekretariati Sekretariati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakuna kurugenzi ya sera na utafiti. Huyu atakuwa ameteuliwa kuwa afisa kwenye idara ya sera na utafiti. Vipi mabadiliko hayo hayajagusa ofisi yetu ya makao makuu Zanzibar?

  Kuna mtu ana historia ya kila aliyeteuliwa tumjue kwa undani?

  Namfahamu Halima Mdee.

  Mwita Mwikabwe ndio nani?

  Ali Chitanda?

  Dady Igogo?

  Regia Mtema?

  Danda Juju?


  Tujue elimu yao, wamewahi kuongoza wapi? na hata makabila yao-manake isije ikiwa ni wachaga watupu
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chadema boresheni chama kwa ushindani makini ila chungeni mamluki.Nadhani mabadiliko hayo yatakuwa na tija kwa mustakabali wa chama kinachotaka kuongoza dola.Mamluki ni sumu mkiruhusu wapenyeze Chadema.
   
 14. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  KUKUBWA ni kuwa wanapaswa kuwa makini, kwani wakizuia mamluki ndani ya chama wajue na nje wapo kwani hujasikia ya Waislamu walioibuka na kudai Chadema wanaudini wakasahau CUF?
   
 15. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ya study leave na kujiandaa uchaguzi wa jimbo la Ubungo umesema wewe. Huyo hawezi kushinda hata uenyekiti wa kijiji nini ubunge. CHADEMA wangefanya vizuri zaidi kama wangemteua Mwita kuwa mkurugenzi wa vijana- kwa kuwa amewahi kuongoza vijana wa DARUSO na UVCCM, na pia anatoka kabila la wapambanaji wakina Chacha Wangwe. Halima Mdee angepelekwa kurugenzi wa wanawake.


  .......ndiyohiyo
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huo ndio ukabila tunaousemea na kuupiga vita kila siku na sasa umeuonyesha mwenyewe wewe mwanachama wa chadema
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ya kusema fulani AULA ndio yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi. Nafasi sio za kuwapa watu ULAJI. Na wanaochaguliwa wakihamua kula kweli mnawaita mafisadi.
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani siku za Nyuma kuna mahala Mnyika alisema ana mpango wa kuachia ngazi

  Pia,Halima Mdee yuko fiti.Halafu kama Kweli CCM wanataka kumsimamisha Nape huko ubungo apambanae na Mnyika basi tuseme CCM washalikosa hilo jimbo
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  As long as its for the good thing... Hongereni sana; wasiwasi wangu ni kwamba Mnyika is a very intelligent guy and you can't just drop him and excpect everything will be fine... unless yeye mwenyewe amekubali. Na huyu Mwikwabe kaja lini... kaijua Chadema lini... kakubalika na vijana lini... hata akamaliza na ka-probartion lini... hadi leo kupewa dhamana hiyo?? Ina maana hakuwamo mtu wa maana before him?

  Naomba mungu usiwe ule mwanzo wetu tuliouzoea wa wapinzani na replacement circus... Chadema mmeanza mapema sana kugawana vi-miraba vyenu, ngoma ya kitoto haikeshi!!!
   
 20. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya, nimeshaondoa hayo mambo ya kuula. Mi nilijua kuula maana yake ni kubahatika kumbe kuna maana tofauti kabisa

  .......ndiyohiyo
   
Loading...