Mabachela wenzangu, mnapika vyakula gani vya haraka haraka?

Na issue nyingine mabachela tunateseka ni kwenye kufua...mi njia rahisi nina mashati 18 na Boxer 22 navifua vyote naviweka, na nia jeans zisizopungua 9 kadeti 3..nachofanya jeans kufuliwa ni nadra sana nakuwa nazi-edit(haifuliwi inafutwa na maji na kitambaa kwa ustadi mkubwa)...so kufua nafua mara moja kwa mwezi (Boxer,Vest,Mashati na sox pair 3).na haipiti siku tatu nafua shati moja usiku ninavokuwa nimetoka mihangaikoni .Jeans ikifuliwa siku hiyo lazima icheke ...
Uzi wa vyakula we unatuletelea stori za kufua! Umevurugwa?
 
Weka wali kweny ricecooker weka chai yako pemben wali ukiiva pakua weka kweny feni upoe fasta ukishapoa chukua chai piga fasta au unaweza nunua ndondo kwa mamantilie ukija unamwagia juu unapiga

Ukichoka wali chai nunua kiungo cha pilau cha 100 na mshikaki wa jero changanya kwenye ricecooker vizur vikiiva ni pilau tayar halina mbwembee chukua nyanya moja kata kata piga shushia na maji

Mm nilijenga urafiki na wale wamama wanaouza mboga za majan so nikitaka nampigia simu ananikatia katia kabisa nikichukua nikuosha weka kwenye jungu chukua nyanya moja kitunguu changany vyote na mafuta wela vyote zungusha dk 6 had 8 tayar



Sent using Jamii Forums mobile app
Mbiga usioshe baada ya kuikatakata, unaondoa viinilishe. Ioshwe kabla
 
nunua box la tambi, weka getto.

kutoka mishe, chap chemsha maji toa hapo vikombe viwili vya chai

then tia chumvi kijiko cha chai nusu, weka tambi kiasi chako, dak 5 toka chuja maji kama yamepaki.

then weka mafuta kidogo kwa sufuri then unga tambi zako kwa suka au nyanya na kitungu (utakavyo penda siku io)

and that's it.

#chai na tambi
 
Vyakula visivyo na mlolongo mrefu wa kuandaa na vyombo vichache sana vitumike. Nimechoka ubwabwa (wa rice kuka)/tambi/ugali na nyama au mainiau mchemsho. Vitu gani vingine huwa mnapika?

Asanteni
Bamia ,unachukua nyanya na kitunguu ,unakaanga kama dakika tano hivi unalumangia na sembe lako na samaki wa gengeni kama kilainishi
 
Kupika kila siku kunachosha fanya hivi kama una jokofu, wewe tenga siku upike vyakula tofauti tofauti kisha hifadhi kwenye jokofu, kazi yako inakua kuchota kidogo na kupasha kwenye Microwave tu.

Mtembelee Aroma of Zanzibar YouTube atakupa muongozo wa kupika vyakula mbali mbali mimi huyu ni mkombozi wangu.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Dah.... Utakuwa unakula viporo maisha yako Yote. Hatari Sana 😀
 
Ugali na mayai..
Unapiga ugali, unapika mayai. Ugali unalia kwenye sufulia na mayai unachanganya umo umo.. Flampeni kwa mwezi inaoshwa mara moja sababu huwa haichafuki.
Unakuwa na kazi ya kuosha sufulia tu
Tabia yangu hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom