SoC02 Mamantilie kisasa inavyoua umaskini Dar es Salaam kwa haraka

Stories of Change - 2022 Competition

Official_lulidahaJR

New Member
Jul 22, 2022
2
1
MAMANTILIE
Hii ni biashara ambayo watu wamekua wakiuchukulia kawaida lakini imetoa ajira kwa watu wengi katika miji mingi na Leo hii watu wamenufaika sana hivo kwa mtu ambae unahitaji kubadili maisha take kwa namna moja ama nyingine anapaswa kufatilia nakara hii ambayo itakujenga na utafanikiwa kwa haraka.

MAMANTILIE KISASA
Hii ni biashara ambayo ukiifanya kisasa na kulingana na mabadiliko katika suala zima la utandawazi lazima mafanikio uweze kuyaona kwa haraka zaidi na kuweza kukidhi mahitaji ya muhimu zaidi ,Nzuri zaidi biashara hii haihitaji mtaji Mkubwa sana na inaweza fanywa na mtu yeyote na jinsia yeyote .
BIASHARA HII JIJIN DAR
Mamantilie tunaenda kuiangazia katika jiji hili kama mfano wa sehemu zingine zenye uhitaji wa vyakula make kila biashara unaianzisha kulingana na uhitaji wa wateja na kwa uhalisia Dar inawahitaji wengi sana.

Kuna vitu vya msingi pale unapotaka kuanza biashara hii ya Mamantilie ya kisasa na ukaweza kufanikiwa zaidi kwa haraka ,usipozingatia hizo taratibu kwako itakua ngumu na itakupa ugumu katika kuianzisha vitu ivyo ni:

01: ENEO LA KAZI
Hapa ndipo kazi itakapoanzia na kwa Biashara hii unapaswa uliandae eneo hili ,eneo hili litatumika zaidi katika kuandaa vyakula tayari kwa kusambazwa kwa wateja ,pia kuna wateja wa karibu na eneo la kazi watahudumika hapa hapa kama kawaida kama Mamantilie ya asili inavofanya kazi.

Eneo hili litamwezesha mmiliki wa biashara hii kuhifadhi chakula na tayari kwa kuwasambaza kwa wateja wa mbali.

02: AINA YA VYAKULA VYA KUUZA.
Katika biashara hii kuna vyakula rahisi unashauriwa kuviuza ambavyo itakua rahisi kuuzika na havitohitaji gharama kubwa. Vyakula hivi ni kama vile :- Ugali -Wali -mihogo ya kukaanga -vitafunwa na chai na supu - karanga za kukaanga

03: NAMNA YA KUPATA MAHITAJI YA VYAKULA
Katika kuandaa chakula unahitaji kuwa na mahitaji kwa kila chakula hivyo katika biashara hii ukitaka kuendesha kisasa kwanza andaa stoo ya Mahitaji ya chakula ili kuondoa gharama na njia rahisi ni kuagiza vyakula katika maeneo yenye bei nafuu mfano kama vile maharage ,mahindi,viazi mviringo ,na viungo vingine vya muhimu na kuvihihifadhi kwenye stoo tayari kwa kupika chakula katika eneo la kazi.

NB: Njia rahisi ya kupata Mahitaji ya vyakula ni kuagiza maeneo ambayo gharama ni nafuu ili kukurahisishia kutengeneza faida kubwa, hapa unaweza kuagiza vitu vya muhimu zaidi kama mahindi na kusaga mwenyewe ,maharage, viungo,vitu vingine vinavyoweza kudumu muda mrefu bila kuharibika

04: KUANDAA SOKO LA KUDUMU. Katika biashara ya manufaa lazma uwe na uhakika wa wateja ili kuuza chakula kwa uharaka na kupata faida za kutosha, hapa unatakiwa kufahamu ni kundi gani la watu linauhitaji wa chakula katika eneo lako hawa ni kama vile bodaboda, wanachuo, wanafunzi, waajiliwa(walimu na wengine), watu wa kufanya kazi za nguvu (wajenzi, Gereji, wafyatuaji na n.k), wamiliki wa biashara zingine kama vile wamiliki wa salooni, Duka, Wakala wa kusajili lakini,Wakala wa kutuma na kupokea pesa ,wauza matunda .NB : kitu cha muhimu cha kukizingatia hapa ni kuangalia watu wenye uhitaji na kuwafanya wawe wateja wa kudumu.

05: NAMNA YA KUFANYA MAKUNDI YA WATEJA KUWA WA KWAKO
Tumeweza kuna makundi au aina ya wateja ambao wanahitaji chakula kila siku na hawa tunawageuza kuwa wateja wa kudumu kivipi nifatilie.
  • Kwanza chukua mawasiliano ya wateja wako na wasapu namba ili kuwajulisha kama wanauhitaji zaidi wa chakula
  • Kwa wateja wanaokaa eneo la pamoja kama wanachuo ,wanafunzi ,walimu tunapaswa kutengeneza kundi LA wasapu au mesenja ili kuwataarifu na kurahisisha wao kupata huduma
  • Wateja kama bodaboda katika vijiwe tofauti chukua namba zao na kuwauliza pale wanapohitaji huduma au oda.
NB: Kitu cha muhimu zaidi Hakikisha unajua na vijiwe tofauti tofauti vya wateja zaidi ya vijiwe 30 vyenye kuanzia wateja 10 wa uhakika kwa kila siku au baada ya siku mbili unakua na uhakika wa kuwahudumia tena hii itarahisisha kuuza chakula kwa wakati na kwa u haraka zaidi.

NB: Hivyo ni baadhi ya vitu vya msingi ambavyo ni muhimu kuvizingatia zaidi Lindi unapotaka kufanya biashara hii kwa manufaa na kwa muda mrefu.

MFANO WA SEHEMU YA KUFANYA BIASHARA HII HAPA DAR
Mfano unakaa kimara katika kutanua biashara yako unatakiwa kutengeneza mtandao wa wateja wa kudumu katika maeneo yanayofikika hapa utahudumuia maeneo ya Kibo, Corner, Korogwe, Bucha, Kimara Mwisho, hadi mbezi .

NB: Hata za kufata katika kutengeneza mtandao kwa wateja katika maeneo tajwa ni kama ifuatavyo:-
I/ Tafuta namba kwa wateja wako wa kudumu katika kila eneo ili kurahisisha kuwasiliana nao pale watakapohitaji chakula.

ii/ Kwa maeneo hayo tajwa japo juu Hakikisha unatengeneza au fahamiana na vijiwe tofauti zaidi ya 30 na kuwa na wateja wa uhakika 10 kwa kila siku.

iii/ Vijiwe vya chakula unaweza kua shuleni, stendi ya bodaboda, chuoni,kwa wafanyabiashara wengine wadogo.

iv/Hakikisha unawapa ofa wateja ili wakuzoee na kukuamini na kupenda vyakula na huduma yako.
NB: Ukishamaliza kutoa kutengeneza mtandao wa wateja wa kudumu utakua tayari umemaliza mchakato wako wa kuanza kuhudumia wateja wako ,japo mchakato huu utaenda pole pole hadi kuja kukamilika na kuzoeleka na wateja wengi hapa unaweza kuchukua wiki tatu hadi nne pia itategemea na namna unavojitangaza kwa wateja na kutoa huduma nzuri kwa wateja.
CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA HII:
Kila kitu hakikosi changamoto lakin katika biashara hii zipo changamoto kadhaa Nazi ni-

1. Inakuhitaji kuwekeza muda wa kutosha na kujituma zaidi.

2. Mchakato huu ni wa kisasa na hivyo huhitaji uvumilivu has a katika kutengeneza mtandao wa wateja wa kudumu kwani huwezi kukuchukua hadi mwezi mmoja kuwa na mtandao Mkubwa zaidi.

3: Inakuhitaji kusafirisha chakula kutoka eneo la kazi hadi maeneo tofauti tofauti hivo gharama za usafiri itakua juu yako.

4. Itakuhitaji uweze kutumia mtandao wa kijamii panapobidi hivo simu kubwa ni muhimu katika biashara hii.

5: Kwa mtaji wa kuanzia unatakiwa uwe na angalau laki tatu na nusu ili kunufaika kwa haraka. NB:hizo ni baadhi ya changamoto lakini kuzitatua inawezekana muhimu kujituma na kujua malengo ya kufanya kazi iyo.

UPEKEE WA MAMANTILIE KISASA.
Biashara hii ya kisasa inajitofautisha na Mamantilie ya asili kwa namna moja ama nyingine tukatazame upekee wake nao ni:-

01: Ni huduma ambayo inaweza kuhudumia watu wengine tena katika eneo kubwa .
02: Mauzo take ni makubwa kwa kuwa inaendeshwa kisasa na huweza kuhudumia watu wengi.
03. Inakuhitaji kutuma teknolojia na ni rahisi kutumia .
04: Inawarahisishia wateja kupata chakula kwa urahisi bila kupoteza muda wa kuhangaikia kufata chakula.

05. Hupunguza hasara kwa kiasi kikubwa kwani huepusha kubakisha vyakula kwa kiwango kikubwa kwani Mara nyingine utaandaa chakula kwa oda.

06: Utaweza kutengeneza faida kubwa zaidi ya milioni mbili hadi kufika milioni nne kwa mwezi.
NB: Hayo ni baadhi ya mambo niliyoyandaa katika nakala hii na napenda kusema kuwa kwa kijana wa Leo hii anapaswa kujituma na kuona kila fursa inamaana kubwa sana katika maisha. Biashara hii unatakiwa kujituma na kuona kila unachotaka kufikia kinawezekanika zaidi ni kujituma kama kijana wa Leo kwa sababu ajira za serikali zimekua za ushundani Mahitaji ni wengi hivo tunapaswa kuotokudharau kazi hizi kwani utatengenezeza pesa za kutosha kuliko waaajiriwa ukiwa makini utatengenezeza kuanzia milioni mbili hadi nne kwa mwezi kitu ambacho kitakua na maana kubwa katika maisha yako yajayo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom