Maazimio ya Mwaka mpya 2008

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,733
40,846
Binafsi nataka nihakikishe kuwa KLH News inakuwa ni chombo kinachofikisha habari haraka zaidi kwa Watanzania mahali popote ambapo wana mtandao. Nataka niweze kuthubutu zaidi na kwenda kule ambako chombo kingine cha habari hakijathubutu kwenda. Wakati huo huo nataka kuhakikisha kuwa JF inaongeza mwendo kidogo na kuwa the force to "reckon with" katika Tanzania.

Katika maisha yangu ya binafsi nataka hatimaye nipate ile basikweli ya umeme ya "all terrain". Na zaidi ya yote nataka nihakikishe posa yangu inakubaliwa.

Kwa upande wa serikali yetu sijui ni nini wakiazimie ili mwaka huu ukiisha tusema walifanikiwa?. Na sijui wewe kwa upande wako una maazimio gani.
 
We! Nini unatufundisha hapa Mzee Mwanakiji? Nikiangalia picha ya sura nakutathmini umri wako haundeni na umri wa mtu kujiandaa kutoa bali kupokea mahali. Au ndo kutekeleza usemi wa Ng’ombe hazeeki maini?! (Mimi Mjukuu wako Babu hivyo hii ni utani tu tusijenge chuki tafadhari)

Maana siasa za majukwaa tumeona zimetutoa na kutufikisha wapi. Na tafsiri ya uhusiano kati ya uchumi na siasa imeonekena kuendelea kuwa msamiati mgumu wenye maana isiyotekelezeka kwa Wadanganyika. Kwa kuwa tunakabiliwa na hatari ya kuvunja rekodi ya kuhamisha majukwa ya siasa za adhalani kuhamia janvi la mtandao kisha kujiita wanamabadiliko, wafurukutwa/wakereketwa, wapendamaendeleo, wanaharakati huku tukiongeza maji baharini, udongo juu ya kichuguu, sukari kwenye asali, chumvi kenye nyongo.

Hili limekuwa swali gumu sana kwangu kama mwanachama wa JK 2007. Hivi kwa upeo wa wana JF nani ameyasikia au kuyaona matatizo ya Danganyika tuliyojadili mwaka 2007 kwa mara ya kwanza? au nani kaleta mada mpya kabisa juu ya matatizo ya Danganyika Republic katika 2007? Labda hebu tukumbushane; katika majumuhisho tumejadili yafuatayo kwa urefu:

1. Ubadhilifu na Ufisadi
2. Upendeleo katika zabuni na ajila
3. Udini na ukabila

Mijadala ni muhimu tena sana lakini ni fanisi iwapo inaishia kwenye maazimo yanayotekelezeka. Vinginivyo hizo ni porojo sawa na za wamachinga wa Kigogo Sambusa ama wazee wa balaza la kahawa Yombo Vituka au wacheza pool popote Danganyika Republic. Hivi hawa watajwa hapo juu hawajui haya matatizo japo katika upeo tofauti? Na je tunajitofautisha nao vipi kimatendo?

Somo hilo hapo juu limekuwa ujumbe wangu mara kwa mara hapa JF. Sasa napendekeza mwaka huu 2008 uwe wa mabadiliko yenye kuonyesha tofauti ya waziwazi kati ya wapiga porojo na watendaji waungwana kwa kuhitimisha mijdala yetu kwa Maazimio na kuyatekeleza. Hebu tuweke mpango mkakati wa mwaka 2008.

Utume wangu katika mwaka huu 2008 ni kuanzisha Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Vijana litakalotengeneza mabepari wa ndani baada ya miaka kumi. Kama wewe ni Mfanyabiashara mwenye umri chini ya miaka 32 tafadhari wasiliana nami haraka kupitia 0754 917205. Njooni tupange mikakati ya kumiliki uchumi wa nchi yetu yenye asali na maziwa. Kwa Danganyika Republic Siasa haiwezi kujenga uchumi bali kuuporomosha.
 
Maazimio mazuri hayo. KUishi bila malengo ni kuishi bila mwelekeo. Haiwezekani mtu uhishi kwa kubahatisha. Wengine ni vigumu kuweka malengo ya mwaka mpya lakini kuwa na kitu kinachoongoza mwelekeo wa maisha yako siyo kitu kibaya.

Umesema kitu kimoja ambacho ni muhimu sana na sielewi tutaweza kukifanyia kazi vipi hapa kama Kitila alivyoanzisha mada kuhusu mwelekeo wa JF. Haitoshi kuzungumza na kujadili tu lazima tufikie mahali tunahitimisha mjadala na kutoa maamuzi. TAtizo kubwa liko kwenye utekelezaji.
 
Wakuu wote JF, naomba kutoa heri ya mwaka mpya, na tuendelee kumkoma nyani giladi.

Mzee MMJ, dawa ni kuendeleza libeneke, na heshima mbele na tuendelee kushirikiana!

Ahsante Wakuu Wote JF!
 
Binafsi nataka nihakikishe kuwa KLH News inakuwa ni chombo kinachofikisha habari haraka zaidi kwa Watanzania mahali popote ambapo wana mtandao. Nataka niweze kuthubutu zaidi na kwenda kule ambako chombo kingine cha habari hakijathubutu kwenda. Wakati huo huo nataka kuhakikisha kuwa JF inaongeza mwendo kidogo na kuwa the force to "reckon with" katika Tanzania.

Katika maisha yangu ya binafsi nataka hatimaye nipate ile basikweli ya umeme ya "all terrain". Na zaidi ya yote nataka nihakikishe posa yangu inakubaliwa.

Kwa upande wa serikali yetu sijui ni nini wakiazimie ili mwaka huu ukiisha tusema walifanikiwa?. Na sijui wewe kwa upande wako una maazimio gani.

Changisha JF ununue basikweli hiyo! Hongera mwanakijiji na endeleza mapambano mwaka ujao! Hongera JF kwa jamvi huru hili.
 
Back
Top Bottom