Maaskofu wamezibwa Midomo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wamezibwa Midomo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlengo wa Kati, Jun 2, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Miezi mitatu iliyopita Tanzania ilishuhudia siasa za aina yake kutoka kwa Maaskofu hasa wa Kanisa Katoliki na Mapdre wake kutoa matamko kila siku. Ilikua ni vigumu siku ipite bila Kusikia Padre huyu wa TEC kasema hiki, mara wengine wakisema hawaogopi kufa wataendelea kusema tu.

  Ilikua ni bandika bandua kwa matamko. Kuna watu wenye busara walihoji juu ya Viongozi wa dini kujiingiza moja kwa moja kwenye siasa na wengine waka ambiwa wavue majoho waingie kwenye siasa.

  Kama haitoshi nao mashehe waliendelea kutoa matamko kupinga kinachosemwa na Maaskofu basi ikawa patashika kila kona ya Nchi. Wataalamu wa Masuala ya siasa wanasema naona hasira nyingi zilitokea kwenye uchaguzi wa Mwaka 2010 kwani nao walikua na Wagombea wao maeneo mbalimbali sasa hasira zimeshuka wameendelea na kazi yao ya kulea waumini wao.

  Binafsi nawapa Hongera viongozi wote wa dini Maaskofu, mapdre na Mashekhe kwa kuamua sasa kufuata mambo ya kazi yenu na kuwaachia wanasiasa mambo yao. Hongera sana TEC na Pengo kwa kusikia maoni ya wadau mbalimbali.

  Hongereni Maaskofu wa Arusha kwa kuamua kutulia. Tuna hitaji Tanzania ya Watanzania isiyokuwa na Mashinikizo ya Viongozi wa dini mbalimbali. Basi kila mtu atimize wajibu wake iwe kwa mwanasiasa, mkulima, mfanyakazi na Viongozi wa Serikali.

  Tunahitaji Tanzania yenye amani na Tanzania yenye kutofautiana kwa hoja na sio misingi ya Ubaguzi wa Kidini na Makabila.

  Viva Tanzania.
   
 2. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetulia sanaaaaaa! Hongera sana! Tungepata hoja kama hizi JF ingekuwa hazina ya Fikra!
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naona katoliki wanawasumbua sana akili,wanamambo mengi ya maendeleo wanayafanya na sio kwenda kushinda Manzese kwenye mihadhara na kuichambua bible badala quran.
   
 4. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Bullshitt!! Viongozi wa dini wanawaongoza watu ambao wanaweza kuwa-affected vibaya kama wanasiasa wasipoongoza vizuri nchi. Kwa mfano sasa hivi wananchi wanalia nna maisha magumu yanayotokana na mismanagemnt ya wanasiasa. Kwa hiyo viongozi wa dini hawawezi kukaa kimya wakati wananchi wanaumia, eti kwa vile wao siyo wanasiasa. Huyu John Marwa ni wewe mwenyewe umeji-support
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  serekali sasa imeingilia KKKT kupitia kwa fisadi askofu mdegela......na juzi kule mwanza kwa kanisa la mennonite tumeisoma muvu...katoliki ndio wazee wa discipline hakuna kuyumba....:mimba:
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  duh! kweli JF kuna watu wa kila aina
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuitenganisha siasa na dini ni vigumu kufanya hivyo.Mambo ya dini(Imani)huwa sipendi kuchangia Ila hapa nnapita tu
   
 8. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilitegemea utaonyesha nani/nini kimewaziba lakini sijaona.Pia kama umetegemea kuongelea viongozi wa dini kwa ujumla ungeonyesha hivyo kwenye kichwa cha habari lakini umeonyesha maasikofu kumbe kuna mashekhe pia.
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Haa! Mrengo wa kati aka John Marwa? he he he! wazee wako kazini kwelikweli.
   
 10. i

  isinkini Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini wakati wa uchaguzi? maisha magumu yalitokea wakati wa uchaguzi tu? ndo kusema sasahivi na kabla ya uchaguzi maisha yamekuwa/yalikuwa bora? au hawakuwepo kabla ya uchaguzi au walijisahau kwa miaka kadhaa?
   
 11. R

  Ray Isly Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aluuuuuua kweli watz wamepevuka kumbe mlikua mnaliona hili! Wale waloingilia hz siasa niwale wadau waliokua wanategemea kukinga mikonooo.mana walisema kpnd hk cha awamu ya nne taasis zao zimezalilishwa kwahyo walitaka kumpa shavu mwana,wabongo wakawasoma.dah poa co ishu 2imarishe umoja wa kibongo kimtindo.sor kama haipo poa ndo maisha.
   
 12. K

  Kivia JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Watasema nini wakati walishapewa mabilioni hapo juzijuzi kupitia ''MOU'' sasa njaa kwisha kabsa.
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,745
  Trophy Points: 280
  kaka kwenye kusimikwa upadre hakosekani makanisani, AF KUNA ILE KI2 YA kupitisha mambo bila ushuru,hao makasisi wakichonga sana watageuziwa kibao make nanihii anavisasi ohooo
   
 14. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Dini na Siasa, pouwa!
   
Loading...