Maaskofu ndio wasaliti

Maaskofu ndio wasaliti

Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?
Wewe ni muumini wamashaka na kwa kua ni mambo ya imani nitasema tuu Mungu akusaidie

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

Huu ni unafiki, hukukereka kwenye BMK walivyo endesha bunge na kura!, serekali inavyo fanya kampeni za ndio, ukereke ushauri ya kura ya hapana!!

Nakubaki mtoa hoja, ana hoja za msingi, ila sina uhakika kama huu waraka watu wameusoma na kuuelewa kwa hoja na fikra zilizomo.
Hii nikatiba na si uchaguzu. Huu ndio msingi wa Taifa na si serekali. Hebu tu chambue mambo kwa hoja pevu.

Kimsingi na heshim Sanaa uwezo wa kufikiri wa maaskofu wa Kiroma, na uvumilivu wenye weledi mkubwa. Ila hapa kuna mambo ya msingi ya ya liyo wafikisha hapa. Tuusome waraka wao na kuuelewa neno kwa neno kabla ya kuu unga mkono au kuu kosoa. y
 
Hivi nyote ni vipofu? Anayetaka kuingiya mahakama ya kadhi kwenye katiba hamuoni anaye lazimisha katiba bila maridhiano huyo hamuoni!!
 
Tatizo Lako Mkuu Bado Hujamuelewa Vizur MUSAMI Kwa Ufupi ilitakiwa Maaskofu Wakae Pamoja Na Mashekhe Wajadil Msimamo Wao Ndo Wautoe Hadharani. Lakin Kusema Maadhimio Ya Maaskofu Tz Ni ... Juu Ya Katiba. Swali, Je Masheikh Nao Wakija Na Msimamo Wao Kinyume Na Maaskofu Huoni Kama Itatokea Balaa Kubwa?.

Hakuna hoja kuwaambia maaskofu hawawezi kujadili jambo la kitaifa bila ya mashehe, au mashehe bila maaskofu.

Hakuna balaa lolote litokanalo na kutofautiana kimawazo au misimamo. Kimsingi kunatofauti kubwa Kati ya misimamo ya kiimani na kimtazamo Kati ya madhehebu ya kikristo au kiislam na Kati ya dini hizi na hata dini nyingine.

Kuanzishwa kwa mjadala wa Mahakama ya kadhi kama hoja ya kitaifa ama kikatiba ulikuwa mwito wa kuonyesha hadharani tofauti hizi za misimamo ya kidini,

Chamsingi hapa ni kuangalia namna ya ku harmonise hii misimamo kwa mjadala mpana usio na maneno au vitendo vya uvunjifu waamani.

Msimamo wa maaskofu, umetumia lugha ya kisomi na hekima kubwa, Ila kuwakilisha msimamo dhabiti na wenye ishara ya onyo kwa uendeshaji wa taifa kwa namna hii ya watu wachache kuamua mambo ya kitaida kwa kivili cha madaraka Yao (Serikali).

Tunajitaji pia kusikia msimamo ya mashehe na wanazuoni wao na ikiwezekaka kuingia kwenye debait.

Kuna hoja wanatofautiana kwa misimamo ya kidini ila zipo hoja wanaweza kukubaliana na kuwa na nisimamo sawa.
 
Mimi hapo sioni ushindani wowote. Mbona serikali hiyo hiyo inahimiza viongozi wa dini kuwalea watu wake katika maadili na kupelekea nchi kupata viongozi wazuri? Huwezi kutenganisha dini na serikali. Utasali wapi kama hakuna amani? Hapa Maaskofu walimaanisha kuikubali katiba hii ni sawa sawa na kutenda dhambi kwa maana wanajua hii katiba itaathiri vizazi miaka mingi mbele na hii dhambi itatokana na maamuzi ya leo. Tukubaliane hivi, serikali ikiipigia kampeni hii katiba ili ipite acha na wengine waipinge. Kwanini serikali inalazimisha watu kuipigia kura ya NDIYO hii katiba? Nijibu hilo swali langu ndo nitaendelea kuchangia hii thread.

Serikali na kanisa ni vitu viwili tofauti havichangamani,serikali inahusika na utawala wa duniani wakati kanisa linahusika na ufalme wa Mungu ambapo mtawala wake anaitwa Yesu Kristo Yohana 18:36,Hii nchi ni mkusanyiko wa watu wenye imani tofauti,jambo la kujiuliza na wao wakiinuka na msimamo wao hatima ya umoja wa Taifa itakuwaje
 
Maaskofu wako ni waoga, ndiyo maana wewe unadhani ni wasaliti kumbe ulipaswa kuwabatiza jina la wanafiki !
 
Wewe musami niambie kadnari Pengo amechukua hatua gani kwa walio chini yake kuhusu ufisadi wa Escrow na Mkombozi benki?
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo wewe unakubali serikali inavyoipigia debe katiba? Serikali yenyewe ina ajenda gani inapowaambia watu wapige kura ya NDIYO? Kwa nini serikali wasitoe tu uhamasishaji wa kusoma katiba wakawaacha watu kuamua wenyewe? Mifano halisi ninayo. Waziri Mh Mary Nagu juzi kati alikuwa na wamasai akawaambia hii katiba ni nzuri wapige kura ya NDIYO (Hiyo ni kampeni ya serikali) Makamu wa pili wa rais kule Zanzibar naye hivi majuzi kule Zanzibar aliwaambia wananchi kuwa wapige kura ya NDIYO. (Pia hiyo ni kampeni ya serikali) Sasa inakuwaje vibaya Maaskofu kuwaambia waumini wao wapige kura ya HAPANA wanapoona inatakiwa kuwa hivyo? Jamii forum ni ya watu wenye akili wanaoweza kuchambua mambo lakini nasikitika kuona watu wengi wanashindwa kuielewa vizuri hii nchi yetu. Tukubaline hapa kama Maaskofu wamekosea basi na serikali ishakosea zamani na hakuna wa kumlaumu mwenzie...

Mimi katika katiba hii pendekezwa wala kurayangu sio ya siri niwazi tu kwamba nitapiga kura ya H.
Lakini siwaungi mkono maaskofu kwa kauliyao ya kutuelekeza aina ya kura tutakayo piga, wana siasa wanaweza kuwaelekeza wanachama na wana nchi wote aina ya katiba wanayoona kwamba ina faa, na kuwaelekeza wana nchi wapige kura ya namna gani.

Viongozi wa dini wasijiingize kwa undani sana katika maswala ya kisiasa.
 
Mimi katika katiba hii pendekezwa wala kurayangu sio ya siri niwazi tu kwamba nitapiga kura ya H.
Lakini siwaungi mkono maaskofu kwa kauliyao ya kutuelekeza aina ya kura tutakayo piga, wana siasa wanaweza kuwaelekeza wanachama na wana nchi wote aina ya katiba wanayoona kwamba ina faa, na kuwaelekeza wana nchi wapige kura ya namna gani.

Viongozi wa dini wasijiingize kwa undani sana katika maswala ya kisiasa.

huko sahihi mkuu,Mimi mwenyewe hii katiba inayopendekezwa siikubali kwa sababu ni kweli imeacha mapendekezo yetu mengi,tatizo ni pale mjadala huu unapoletwa na Maaskofu kanisani na kutuambia tuukatae wakati humu makanisani tuko watu wenye mitazamo tofauti,kwangu mimi naona ni kukaribisha migogoro,haya mambo tuyajadili nje ya nyumba za ibada,kanisani pabaki sehemu ya kumuabudu Mungu si kampeni za mambo ya kidunia Luka 19:46
 
Wewe musami niambie kadnari Pengo amechukua hatua gani kwa walio chini yake kuhusu ufisadi wa Escrow na Mkombozi benki?

Hayo mambo ya Escrow yana uhusiano gani na tunachokijadili?
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimeusoma ule waraka wa maaskofu, wamepinga katiba kwa fact, fact ambazo ziko wazi tu, sema tanzania tumekua wanafiki mno kulingana na maslahi yalipo kuliko maendeleo ya nchi na future ya tz
 
Taifa bila uongozi wa kiroho linaangamia. Shida serikali yetu inafanya mambo madogo inaacha makubwa. Badala ya kufikiria jinsi kusimamisha umwagaji wa damu isiyo na hatia ya alibino wanaandaa semina Dodoma kuzungumzia issue ndogo sana ya mahakama ya kadhi. Hii akili ya ajabu sana.
 
Kwanza naishangaa serikali yetu kubadilisha siku ya ibada kuwa ni siku ya kupiga kura. Ni kukosa maono kabisaaaaaaaa.
 
maandiko hayana maana km unavyofikiria wewe,hivi Maaskofu wakitulia pasipo kusema chochote huku mambo yanaharibika,kesho na kesho kutwa nchi isipokalika huo Ufalme wa Mungu watauhubirije?,Na je watu wakianza kukimbia machafuko huo Ufalme wa Mungu watamhubiria nani??? KAA FIKIRI KWA KINA.

Nimeipenda hii. hata hivyo gwajima alikuwa na hoja ya msingi kabisa, tatizo kubwa ni jinsi alivyoiwasilisha kwenye jamii. lugha aliyotumia siyo nzuri kwakweli.
 
Sio kila mtu anaelewa maana ya KATIBA. wengine wanafikiri labda ni kitabu cha shule km vingine. Hivyo mtu km MAASKOFU wamekaa wakajadili na kiona haifai mimi naona ni sawa. Km ipo sawa hii KATIBA Kwanini walioshoka dola washawishi kupiga kura ya NDIYO? Hata aliyepo Madarakani aelewe kabisa nae atakuwa raia wa Kawaida japo atakuwa ananeemeka na Pension. Viongozi wa SERIKALI watafakari ktk pande zote za KURA YA NDIO na HAPANA ina maana yake.
Na km ingewezekana leo hii kuleta RASIMU YA KATIBA ya mh. WARIOBA na KATIBA INAYOPENDEKEZWA NA BUNGE lililopita halafu zote zitolewe ELIMU, halafu tuzipigie KURA.
Majibu ya maswali yaliyopo mtaani yangepata majibu
 
Tokea Kardinali Pengo atoe kauli ya kupinga mapendekezo ya Maaskofu juu kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa,amekuwa akiitwa msaliti hata kufikia kutukanwa na akina Gwajima,lakini nionavyo mimi wasaliti ni maaskofu.
1.Wameusaliti wito wao wa kuutangaza Ufalme wa Mungu badala yake wamekaa wakipoteza muda kuujadili ufalme wa duniani Luka 9:2 Yohana 18:36 labda watuambie wameongozwa na andiko gani
2.Wamesaliti umoja wa Taifa la Tanzania maana unapotoa tamko la wakristo kupiga kura ya hapana unawaambia nini watu wa imani nyingine?je na wao wakikutana kupiga kura ya ndio,mustakabari wa Taifa utakuwaje?
3.Je huu sio mwanzo wa kutumia umoja huu kufanya kampeni za viongozi wanaoona wao wanafaa kuongoza kipindi cha uchaguzi?
4.Makanisa yanahusisha watu kutoka makundi mbalimbali,wapo wanaoipinga katiba inayopendekezwa na wapo wanaoikubali,je huu sio mwanzo wa kukaribisha migogoro ya kiitikadi ndani ya makanisa.
Mungu atusaidie

Japo una haki juu ya maoni yako; mimi sikubaliani na mtazamo wako kwa sababu moja kubwa; Kama Cardinal Pengo alishiriki kikao tajwa kama tunavyosikia na akalitia mkono lile tamko ina maana kwa dhana ya "uwajibikaji wa pamoja" hakuwa na haki tena ya kutoka pale na kwenda hadharani kukinzana na tamko rasmi; huo ndio msingi wa Kardinali kuitwa "msaliti" mithili ya Zitto Kabwe; yeye mwenyewe kwa kauli yake hiyo "public" akasema; namnukuu: "Mimi ni nani kukataa waraka ule usisomwe makanisani"!! Wengi wapewe lakini wachache wasikilizwe; ndio lakini alitakiwa kunyamaza baada ya kushindwa kuwashawishi maaskofu wasifikie uamuzi ule!

na pia tetesi kwamba alishawishiwa na "homeboy" wake Pinda kuwaendea kinyume maaskofu nazo zinamuweka pabaya Pengo kimsimamo; kimaadili, kama kiongozi wa kiroho na mkuu wa kanisa katoliki hapa nchini!!!!

Pili sikubaliani na tafsiri yako "finyu" kuhusu majukumu ya Viongozi wa Kiroho; aka Wachungaji; Viongozi wa kiroho hawatakiwi na haiwezekani waone "kondoo" wao wanaangamia kisha wanyamaze au waangalie pembeni simply because eti wasiingilie mambo ya Kisiasa! nani kasema hayo; kwa kifungu kipi cha Biblia; au Korani au Katiba ipi na ya nchi gani; kifunghu gani kaka?!; wanaosema hivyo kutaka Viongozi wa Kidini wanyamaze ni wanasiasa waovu wanaoogopa "mamlaka ya kimaadili" ya viongozi wa kidini ili waendelee na maovu yao bila kuingiliwa; wanaogopa ushawishi wa viongozi wa kiroho kwa wafuasi wao:

Na dunia hii ina mifano mingi ya viongozi wa Kidini katika karne hii hii tuliyopo; waliosimama imara kuirejesha jamii kwenye utengamano; nitakutajia baadhi hapa uka_google upate uelewa wa michango yao katika mustakabali wa nchi zao"
Martin Luther King Jr; USA, Desmond Tutu wa South Africa; Pope John Paul II wa Catholic church, Cardinal Jaime Sin wa Philipines, Padre Aristide wa Haiti; fanya primary research kidogo utawapata wengine!!

In the same vein; matamshi ya Askofu Gwajima dhidi ya Kardinali Pengo nayo yanamuweka pabaya kimaadili; kauli kama zile kutoka katika kinywa cha kiongozi wa kiroho tena hadharani; hazifai; kulikuwa na njia bora zaidi za kuonyesha msimamo wake kuliko alivyofanya; ambazo zingemuacha na heshima yake intact!
 
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.

Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?

Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?

Wamenikera sana hao maaskofu.

Inawezekana wewe ni mkatoliki ila mpaka sasa hujaelewa sababu KUBWA iliyofanya maaskofu wote Tanzania waipinge hiyo katiba, sasa nakushauri ufuatilie SABABU KUU iliyofanya hiyo katiba ipingwe kisha uje upost tena humu ndani!..
 
Basi kama unaona kazi ya kanisa ni kiroho naomba kuanzia leo husiende hospitali za Kanisa, usimpeleke mtoto wako shule na vyuo vya kanisa, maana hivyo vitu vinatakiwa kufanywa na serikali na kanisa kutangaza mambo ya kiroho? Kwa nini unapata huduma hizo na husipende za serikalini.

Haya ne maneno yaliyowahi kutolewa na Kardianli Pengo: ["Viongozi wanapenda tu habari za kuwafurahisha wao na wapambe wao. Wanapenda kusikia tu mambo mazuri hata kama ni ya kipumbavu….. mimi nimeyasema [nayasema] haya leo, maisha yangu yamo mikononi mwenu [Viongozi mnaotaka kusikia mazuri tu]; lakini kwa kuwa ni Mungu kanituma nitasema tu. Mkiniua kesho sijali; mkisikia, msiposikia shauri yenu".

Akiendelea kuzungumza kwa hisia kali, Kardinali Pengo aliongeza: "Mkiniua damu yangu iko mikononi mwenu, kwa sababu mtakuwa mmemwaga damu isiyo na hatia. Nasema hivi si kuwa naropoka, [bali] najua ninachokisema. Akaonya akisema: "Nasema haya leo na nyie [viongozi] mkiwa hapa; kama kuna chombo kitakachokuwa na ujasiri wa kuandika, mtaona yatakayotokea".

Awali, akiwaasa viongozi wenzake wa dini juu ya kilichomkera zaidi, Kardinali Pengo alisema: "Ni kosa kubwa kwa viongozi wa dini kukubali kila jambo lililo kinyume na ukweli bila kulitolea neno lolote. Simameni daima katika ukweli; liwalo na liwe. Ukiogopa kufa leo, utakufa kesho; ukiogopa kusema ukweli leo eti kwa kuogopa kufa, utakufa kesho".
musami
 
Last edited by a moderator:
Mwananchi

Kwa hiyo utafurahi ukiona maaskofu wanakuja na Jina la mtu wanayeona anafaa kuwa rais mwezi oktoba,kwa hoja ya kutoa elimu kwa waumini wao?Ukristo msingi wake ni Yesu Kristo anayesema utawala wake si wa dunia hii,ukristo msingi wake sio hekima na misimamo ya kidunia.

Swali la msingi iwapo na watu wa imani nyingine wakiunda umoja wao na kutoa kauli tofauti na maaskofu,huoni kama tunajiweka kwenye wakati mgumu kama nchi?
 
Last edited by a moderator:
Kwani nimekwambia nataka kuchaguliwa au natumia hiari yangu kuchagua. Hapa tunaongelea Katiba kama sheria mama ambayo inamgusa hata Askofu na mimi na wewe kama waumini. Askofu kama mguswa na kiongozi wa kiroho hawezi kuona serikali inalazimisha kuleta katiba mbovu akakubali kusema chagueni kwa hiari yake.

Yeye ni kiongozi na kama kiongozi anayo mamlaka kukemea na kusema baya. Katiba ni mbaya kwa hiyo kama kiongozi wa kiroho anayo mamlaka kuwambia watu wachague hapana. Vinginevyo hasiposema hivyo na nchi ikaingia kwenye vurugu atakuwa mshiriki wa dhambi hiyo.

Ni kiongozi huyo aliyewakana maaskofu wenzake hapa chini anasema:

"Kamwe kanisa haliwezi kufumbia macho uovu ili kundi moja liweze kukaa kwenye mamlaka na uovu wao. Hata kama mamlaka hiyo itatoa vitisho kwa viongozi wakuu, Kanisa Katoliki halitakaa kimya," alisema Pengo

Alisema kuwa kukemea uovu kusionekane kuwa ni udini na ifahamike kuwa Kanisa Katoliki halimsimiki mtu awe rais, diwani au mbunge wa mahali popote, hivyo uovu wowote unaofanywa na mamlaka utaendelea kukemewa bila uoga.

"Katoliki linafahamu madhara yanayoweza kujitokeza katika jamii iwapo kanisa litampendekeza mtu kuwa kiongozi," alisema Pengo.

"Tuliombee taifa letu liepushwe na vitu vinavyotaka kuibuka katika taifa na kamwe kanisa haliwezi kumsimamisha mtu na kusema mumpigie kura," alisema.

Alisema hawawezi kuwanyamazia wanasiasa wakati hata maaskofu pia wanakemeana wanapotenda uovu. "Uovu lazima ukemewe, si kitu ambacho mtu anafikiri kwamba mtu anaweza kutishia kwamba maaskofu wasikemee uovu," alisema Pengo.

Pengo alisema kuwa kutokana na kumbukumbu ya hapo zamani wakati wafalme walikuwa wakichaguliwa na mapadri na maaskofu, madhara yake yalijitokeza kwa kuwa jamii ilichaguliwa kiongozi asiyekubalika.

"Viongozi wa Katoliki wataendelea kukemea uovu huo kwa kuwa unaweza kusababisha mafarakano katika taifa linalotafuta ukweli na haki kwa ajili ya wote," alisema Pengo.

Kwa hiyo utafurahi ukiona maaskofu wanakuja na Jina la mtu wanayeona anafaa kuwa rais mwezi oktoba,kwa hoja ya kutoa elimu kwa waumini wao?Ukristo msingi wake ni Yesu Kristo anayesema utawala wake si wa dunia hii,ukristo msingi wake sio hekima na misimamo ya kidunia.Swali la msingi iwapo na watu wa imani nyingine wakiunda umoja wao na kutoa kauli tofauti na maaskofu,huoni kama tunajiweka kwenye wakati mgumu kama nchi?
 
Tokea Kardinali Pengo atoe kauli ya kupinga mapendekezo ya Maaskofu juu kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa,amekuwa akiitwa msaliti hata kufikia kutukanwa na akina Gwajima,lakini nionavyo mimi wasaliti ni maaskofu.
1.Wameusaliti wito wao wa kuutangaza Ufalme wa Mungu badala yake wamekaa wakipoteza muda kuujadili ufalme wa duniani Luka 9:2 Yohana 18:36 labda watuambie wameongozwa na andiko gani
2.Wamesaliti umoja wa Taifa la Tanzania maana unapotoa tamko la wakristo kupiga kura ya hapana unawaambia nini watu wa imani nyingine?je na wao wakikutana kupiga kura ya ndio,mustakabari wa Taifa utakuwaje?
3.Je huu sio mwanzo wa kutumia umoja huu kufanya kampeni za viongozi wanaoona wao wanafaa kuongoza kipindi cha uchaguzi?
4.Makanisa yanahusisha watu kutoka makundi mbalimbali,wapo wanaoipinga katiba inayopendekezwa na wapo wanaoikubali,je huu sio mwanzo wa kukaribisha migogoro ya kiitikadi ndani ya makanisa.
Mungu atusaidie

Mkuu umemaliza 👏
 
Back
Top Bottom