Maandishi yanayokuja baada ya movie kuisha

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
Wadau nimeona movie/film nyingi zikiisha yanakuja maandishi kama majina ya cast na directors na mambo mengine.
Maranyingi hata mtoto wa miaka michache akiyaona hayo anajua movie au film imeisha.
Huwa yana-move faster kweli katika movie nyingi hata huwez kuyasoma.

Hivi wanayaweka kwa maana gani kama wanayamovuzisha faster? Hem tujulishane wajuvi
 
Maandishi yale yanajulikana kama "Credits". Ni majina ya watu WOOTE ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika hatua mbali mbali za utengenezaji wa movie husika. Kwa kawaida majina ya wahusika wakuu wa movie kama vile main actors, actresses, script writers, directors, producers, editors, director of photography etc hutokea mwanzo wa filamu (ingawa kuna baadhi ya filamu hutokea mwishoni). Majina yanayotokea mwishoni ni cast ( Majina halisi ya wote walioigiza pamoja na majina waliyoyatumia katika filamu husika), kama nilivyosema hapo juu majina ya wooote walioshiriki katika kufanikisha utengenezaji wa movie, awe msaididizi wa director mpaka mtu aliyekuwa akisafisha cabin za mastar (ndio maana yanakuwa majina mengi). Pia hutajwa waliotoa huduma mbalimbali kama malazi, chakula, mavazi, vifaa kama kamera, taa, vifaa vya sauti n.k. Pia nyingi ya filamu za siku hizi hutajwa nyimbo zilizotumika kwenye filamu hiyo. Kuhusu kwenda mbio sijui ulikuwa unaangalia zile movie zetu za kuchovya, maana kwenye movie orijino credits huwa hazikimbii kihivyo unaweza kusoma bila matatizo.
 
Maelezo yameshiba. Ila kwa mfano, Isidingo the need, ikiisha maandishi yanakimbizwa kama nini. Au watu wa TV wanayakimbiza ili kuokoa muda, Sijui nahisi tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom