Maandamano ya wanavyuo kuelekea nyumbani kwa Lowassa

Maandamano ya wanavyuo kuelekea nyumbani kwa Lowassa

Nawasalimu wana jamvi!
Kwa muda sasa kila mmoja wetu ameshuhudie kile kinachoitwa makundi mbalimbali ya kijamii na wasomi "mimi nawaita wanafunzi wa vyuo" kujaribu kuonyesha uma wa watanzania kwamba wanamhitaji waziri mkuu aliejiuzuri bwana lowasa agombee urais wa tanzania 2015. Iwe kwa kushinikizwa, kwa kushawishiwa na fedha au kwa namna yeyote ile nivema makundi haya yakatuambia kwa vitendo kwa nini lowasa awe rais na si mtu mwingine???lowasa ana nini cha ziada "what so special" kwake na si kwa mtu mwingine????je nikweli tanzania inahitaji mtu kama lowasa awe rais atakaefuata??? Baada yakushika nyadhifa mbalimbali nchini mpaka cheo cha uwaziri mkuu na kisha kujiuzuru kwake kwa kashfa ya richmond ameifanyia nini nchi hii? Kama majibu ya maswali haya yatakua mepesi basi na mimi nitakua mmoja kati ya wale akina nanihii pamoja na january makamba wanaoamini kwamba makundi haya yote yanatumwa kwa nguvu ya fedha na ulafi wao kucheza sinema inayoendelea.
Maoni yangu binafsi:
Kwa sasa tanzania haihitaji tena kuongozwa na ccm kwa ujumla wake kwani hakuna alie msafi ndani ya chama hiki.miaka 53 sasa matatizo ya watanzania ni yaleyale miaka nenda miaka rudi.hapa simaanishi kwamba ukawa kuna wasafi na malaika wote la hasha ila ninaamini katika mfumo ambao hakuna chama kitajiona kina milki ya nchi hii kama ambavyo ccm inaamini kwa sasa. Lazima tuweke mfumo wa watanzania kuwa na milki ya nchi yetu sote na si chama kimoja iwe ccm, cuf au chadema na vyama vingine kuamini hii nchi ni yakwako. Tumeongozwa na ccm kwa miaka yote hii wamefanya kwa uwezo wao na sasa ni muda muafaka kufanya mabadiliko ili tuone na hawa wengine uwezo wao. Wasomi njaa ndiyo ambao wataigharimu nchii hii kutopiga maendeleo kwa kuweka mbele maslahi binafsi. Ni mtazamo tuu.
Wasalaam
 
ueleweki Mkuu, stick kwenye hoja issue ni Lowassa au CCM?...... Mods thread zingine zinajaza server tu
 
Hao wanafunzi hawana lolote , watakuwa wamepewa posho ya kujikimu tu.
 
Hawa wanavyuo ni majanga matupu!! Zao la shule za kata za huyu jamaa ni vituko vitupu! Mitihani yao tokea Mtihani wa drs la saba, frm four, na chuo ni multiple choice! sijui kwa form six inakuwaje? na mbaya zaidi multiple choice yenyewe wanagoogle kwenye mitandao wanakutana na maswali ambayo ndio mitihani yenyewe ya vyuo! hatuna watu wa kufikiri bali watu wa kukariri maswali na majibu ya kwenye mitandao!
 
nyota njema huonekana asubuhiii!! EL NDO HABARI YA MUJINI!!!
 
hawakawii kusema zamu ya mwanamke, kadili siku zinavyoenda ni dhairi Nape ana pressure kuliko Lowasa na maji ya shingo yamewafika wenye chuki na Lowassa.

sisi wapenda mabadiliko tunaona ni rahisi kupambana na Lowasa au Makinda kama Nape na Mwenyekiti wenu wakiamua ni zamu ya mwanamke
 
Katika Hali ya kushtukiza maandamano makubwa ya wanavyuo wote wa mkoa wa Dodoma wanaandamana sasa kuelekea nyumbani mwa aliekuwa Waziri Mkuu mstaafu Ndg. Edward Lowassa.

Hali ya mambo inaonyesha ni zaidi ya wanavyuo 8000 Muda huu wakiwa katika misururu ya maandamano Area D na kufunga barabara za Majirani zake bwana Edward Lowassa kama Mh. sumaye na Samwel sita kuwafanya wachelewe Misa muda huu.

Aidha pia jeshi la polisi limeamua kuwapa ulinzi baada ya kuona wanaandamana kwenda kumuomba aokoe kuporomoka kwa soko la ajira

Hii nchi inapoelekea sasa siko kabisa hembu tujiulize kwa ni lazima lowasa kuwa raisi ni kwa nini anatumia nguvu zote kuupata urais angalizo ikulu si mahala pa kukimbilia ukimwona mtu anakimbilia ikulu huyo ni wa kuogopa kama ukoma sisi ni wepesi sana wa kusahau mwaka 2015 tulimwona Ndg J.Kikwete ndie mkombozi wetu watu wakatoa muda wao na kumpa kura za ndio asilimia 80 na wengine wakaja na kauli mbiu ni chaguo la Mungu kinachoendelea kwa sasa kila mtu anajua kama kweli ni kasi mpya nguvu mpya na ari mpya ila sitashangaa manake hata ndani ya Kitabu Kitakatifu BIBLIA imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa , Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apatae ufahamu.
 
Ndio maana mimi huwa nawakubali sana wanafunzi wa udsm huwezi kusikia wamejinasibu na chama fulani au mgombea fulani.they'r trully great thinkers.hawakurupuki.kwa kweli wanafunzi wa vyoo huko dodoma mmejidhalilisha sana.msomi unahongwa ili kumchagua kiongozi?
 
Naona na waandishi wako busy kweli hizi bahasha zinapofusha.Hii ni kama kujitekenya na kucheka mwenyewe!!
 
Team lowassa njooni haraka,tunataka ufafanuzi,hivi adhabu ya huyu bwana imekwisha au?hivi pia siku hizi maandamano bila kibali cha polis ni ruksa?
 
UDOM NAO CHUO,EMBU UDSM NAO WAENDE,UNAKUTA WALIOENDA HAPO WENGI WANA SIFA HIZI
1.ni CCM
2.wamesoma shule za kata,na sasa wapo chuo cha kata
3.Hawajitambui
4.wamepewa 5000,na wamefuata mkumbo
5.wengi wanatoka kaskazini
6.wengi wana aslimia ndogo za mkopo.
7.wanapenda kuonekana kwenye media kwani hawajawahi kuonekana.
8.na wale wa diploma na certificate waliobebwa na ccm hivi karbuni kusomea ualimu.
9.Hawana historia ya kutosha kumhusu Lowawa.
10.Hawajui hatima ya maisha yao,na zaidi hawatajiandikisha kwenye daftari la kupiga kura!!,kwani mda mwingi wapo tu na MABANGO BARABARANI
 
Wangeandamana kumpelekea Slaa kwa mfano Maboomu yangerindima NIGERIA ISINGEONA NDANI
 
Back
Top Bottom