Maandamano ya wanavyuo kuelekea nyumbani kwa Lowassa

Maandamano ya wanavyuo kuelekea nyumbani kwa Lowassa

Kwa nguvu anazotumia kukabidhiwa ufunguo wa magogoni, nadhani atatumia miaka 5 ya kwanza kushushia maadui zake nyundo
Ni urais anaouota ni aina hiyo basi hatufai kabisaaa, achilia mbali ufisadi wake.
 
Lowassa hana sifa ya kulipiza kisasi, ana sifa kubwa za utendaji, uwajibikaji, utumishi, umoja na uzalendo
Hiyo sifa ya kutolipiza kisasi unaipimaje? Na kwa nini kisasi kwani kafanywa nini kama siyo kujishtukia?
 
Mh!nchi hata intellectuals wana ombwe la kisiasa upumbavu huu hauwezi kuukuta pale UDSM!
 
Hata iweje, Lowassa hatufai. Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza, LOWASSA anajitembeza

Wanaomfuata ni watanzania,wanamfahamu uchapakazi wake na sifa ya kuwaongoza.
 
kama CCM hawatompitisha Edward Ngoyai Lowassa kugombea Urais ni bora tumchague Dovutwa atawale hii nchi
 
ivyo vyuo ni vya darasa LA 7 ndo maana akili zao ni km za madereva bodaboda
 
Ccm safari hii lazima mgawane vyombo kudadeki............
 
Mh!nchi hata intellectuals wana ombwe la kisiasa upumbavu huu hauwezi kuukuta pale UDSM!

Mkuu unazungumzia UD ipi? kama kuna vitu hauvifahamu usiwe na kiherehere cha kuongea.Kimya kitakupa heshima.
 
uyu EL naamini anaijua Ccm nje ndani na uchafu wake woooooote ,,
sasa kitu gani kitamtofautisha yeye na hao vigogo/mafisadi wengine wa ccm..
maana naamini wanajuana wooote
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, aliyekuwa waziri Mkuu Mh. Edward Lowassa nyota yake imezidi kung'ara na na kuonekana mwenye kuhitajika kuwatumikia Wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza nyumbani kwake na kumshawishi achukue fomu ya kugombea Urais.

Makundi tofauti tofauti yamejitokeza hadharani na kumchangia kiasi cha fedha ili atangaze nia ya kugombea Urais ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu mwezi Octaba 2015.

Jana tarehe 22/03/2015 vijana wapatao 800 wakiwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walionekana wakiwa katika misululu wakiwa wanaelekea nyumbani kwa Mh. Lowassa maeneo ya Area D wakiwa na mabango yanayosema, tulinyimwa elimu lakini wewe umejenga shule za kata na Chuo cha UDOM, tangaza nia.

Huu umekuwa ni mfululizo wa makundi ya Wananchi ambao wamekuwa wakimshawishi Mwanasiasa huyo kutangaza nia ya kugombea Urais.

Siku za hivi karibuni kundi kubwa la wamachinga walijitokeza nyumbani kwa LOWASSA huko Monduli na kumchangia kiasi cha pesa wakimsisitiza kutangaza nia na kumwomba agombee.

Siku chache baadae Vijana kutoka mikoa ya Arusha, Tanga Kilimanjaro na Manyara wapatao 700 walijitokeza na kumuomba atangaze nia na kumchangia pesa za kuchukua fomu.

Kundi la Mashekhe wapatao 70 wakitokea Wilaya ya Bagamoyo nao hawakubaki nyuma na wakaamua kutoa yao ya moyoni na kumfuata Dodoma ambapo nia yao ni kumtaka atangaze nia.

Ama kweli LOWASSA anahitajika, "Tumeona wengi wakitangaza nia ya kugombea Urais lakini wewe ndiye chaguo letu" Alisikika mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma akisema hayo.

VIVA LOWASSA
VIVA TANZANIA
TWENZETU na LOWASSA 2015.
George Sylvester Wambura.

Poleni sana. EL ni kiongozi mwandamizi wa chama na serikali ya CCM. Nchi hii ina raslimali nyingi lkn bado ni kati ya nchi maskini sana duniani huku baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali yake akiwemo yeye wakiogelea ndani ya utajiri mkubwa, kwa maneno yangu haya sioni kama EL ana jipya kwa taifa hili zaidi ya yeye binafsi kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kukaa ikulu ya Tanzania pale Magogoni DSM. Tafakari. .....
 
Back
Top Bottom