Maandamano ya Wanahabari kesho Ruksa!

Status
Not open for further replies.

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
705
440
Hatimaye jeshi la polisi limeruhusu kufanyika kwa maandamano ya
waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kesho,kilele chake kitakuwa ni katika viwanja vya Jangwani, awali yalikuwa yaishie viwanja vya mnazi mmoja.

Hayo yamo kwenye Taarifa ya Suleiman Kova aliyoitoa hivi punde.
 
wamegutuka usingizini hao. lakini kazi mdundo! Sisi hatuhitaji kuhamasishwa kwa kilicho wazi, kwamba Jeshi la Polisi badala ya kulinda usalama wa raia na mali zao wamejeuka wauaji! Waandishi endeleeni kuwandika katika mbao za dunia, sio hapa kwetu maana twalijua. Uncle akifahamu haya atamwita mtalii amwonye, ndio pona yetu!
 
Hatimaye jeshi la polisi limeruhusu kufanyika kwa maandamano ya
waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kesho,kilele chake kitakuwa ni katika viwanja vya Jangwani, awali yalikuwa yaishie viwanja vya mnazi mmoja.

Hayo yamo kwenye Taarifa ya Suleiman Kova aliyoitoa hivi punde.

Asante mkuu maana kuna mtu ameleta hapa kuwa yamezuiliwa. Kweli ingeleta tafrani ambayo si ya lazima.
 
Mbona kuna mwingine amekuja na uzi wa kusema maandamano yamepigwa stop?
 
Policcm!!!wamekosa weredi wa kazi yao,wamekuwa chinja chinja na miungu watu wasiosikia la mtu,wala la mhazini!
 
wamepima upepo wameona unaelekea wapi heheh nao ni wajanja siku hizi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Awali walikuwa wamezuia lakini baada ya 'Vuta nikuvute' wamekubaliana kwa sharti la kubadilisha location na sasa watakutana Jangwani (Taharir Square).
 
Kumbuka kuna mabom yatakuwa yanatafuta watu kesho namjua Kova.
Kuweni makini jamaa zangu hasa wale wanaoshukiwa na kutafutwa.
 
Ilitakiwa iandikwe hivi; HATIMAYE JESHI LA POLIS LIMETAARIFIWA JUU YA MAANDAMANO YA WANAHABARI NA LITATOA ULINZI. Zaidi ya hapo ni policcmtics
 
Hata Wanachadema wanaruhusiwa kuungana na wanahabari hapo kesho kulaani mauaji ya Mwanahabari mwenzao

Hapo ndipo kwenye tatizo. Polisi wakiona bendera za cdm kwenye maandamano wanajisikia kama wameguswa na kitu kigumu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom