hivi hadi hawa watoto wamefikia kumkumbuka Nyerere na siyo Mwinyi waliyekua chini yake au Mkapa na kumruka kabisa Kikwete.. basi huko twendako siko.
hivi hadi hawa watoto wamefikia kumkumbuka Nyerere na siyo Mwinyi waliyekua chini yake au Mkapa na kumruka kabisa Kikwete.. basi huko twendako siko.
nyerere Bado Anabaki Juu....!jibu Langu Kwa Kifupi Ni Kwamba: Pamoja Na Failures Kadhaa Katika System Ndani Ya Uongozi Wake, Mwl. Nyerere Ni Ishara Pekee Ya Kiongozi Wa Juu Aliyeonekana Kuipenda Nchi Yake Na Utaifa Wake Kupita Viongozi Wengine Kama Si Wote Katika Ngazi Hiyo Hiyo Waliofatia.
waliojitolea magari yao yamevunjwa vioo, wafanyeje...?
baadhi ya mabango yalisomeka
SERKALI GANI HII, INAKABA MPAKA PENATI.
MAISHA BORA KWA KILA FISADI
Na jingine
KIKWETE HUONI KUWA SERIKALI IMEKUSHINDA?
NAURI KUPANDA TOKA 50 MPAKA 100 KWA LIPI LILILOBORESHWA
SUBIRI KIHAMA CHAKO 2010
na mengine mengi.
Dah vijana wananikumbusha enzi zangu, pale Aza boy!
ningekuwa bongo ningekurupua uniform zangu za kale, ili kuonesha mshikamano nao.
nauli jiti, hataaa, haikubaliki!!, besides kama nauli jiti hela ya kununua mhogo wa kukaanga itatoka wapi?(naongea kwa experience yangu pale dsm), halafu hapo baadhi ya madenti mfano mzuri wana aza boy, hawajapiga ruti kwenda tuition, mwenge, magomeni , ubungo ,n.k,halafu wapande tena daladala kurudi home!!, hiyo hela yote wataafford vipi wakati kazi hawana?.
Jamani imenisikitisha sana tumefikia huku? Serikali haina hata huruma kwa watoto wake?.. wataipata wapi huruma wakati watoto wa wakubwa wanapelekwa shuleni na mashangingi ( kama wanasoma nchini).
Eti walipe shilingi 100 and then wakalie siti... Hivi aliyetoa kauli hii anayo akili kweli??? makonda watakubali kweli ......... yaani nalia peke yangu