Maandamano ya SOPA na PIPA, tafsiri yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya SOPA na PIPA, tafsiri yangu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Jan 19, 2012.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama ulitembelea tovuti kubwa kama Google, Wikipedia na hata Facebook, nadhani uliona kuna ujumbe uliokuwa unaonesha kupinga miswaada miwili ambayo serikali ya marekani inatizamia kuipitisha kuwa sheria. Miswaada hiyo ni SOPA na PIPA.
  Lakini unaweza kujiuliza hii SOPA na PIPA ni vitu gani? SOPA ni kifupi cha Stop Online Piracy Act (SOPA) na ile nyingine ya PIPA ni Protect Intellectual Property Act , ni muswaada ya huko marekani ambayo lengo lake ni kukazia zaidi haki miliki kwenye sheria za marekani, kwa sheria hii lengo kubwa ni kulinda wamiliki wa vitu au huduma zinazotolewa online pia kutoa adhabu kali kwa watakaokubwa na kosa hilo. Kwan sheria hii itampa mamlaka zaidi mmiliki wa haki miliki kuweza kuwasilisha suala lake kwa mapana zaidi huku yakiwaweka kizuizini makampuni au tovuti zote zitakazo vunja sheria hii, iwe ni ya marekani au ya Tanzania.

  [​IMG]
  Picha inaonesha mtandao wa Wikipedia ukipinga sheria hiyo.

  Swali kuwa ambalo unaweza kujiuliza ni kuwa kwanini wamiliki wengi wa tovuti wameigomea? Je sheria hii haimaanishi kitu kizuri? La hasha, sio kila kitu kizuri lazima kikubaliwe. Kupitishwa kwa sheria hii kutaondoa uhuru wa kujieleza ambao ndio umejenga ulimwengu wa tovuti za leo. Kwa mfano, mtandao wa Facebook na Wikipedia umejengwa kwa misingi ya watu kugawana maarika au taarifa. Sasa ndani ya sheria hii hutoruhusiwa kugawa taarifa au kumbukumbu ambayo sio yako au bila ruhusa ya mwenye taarifa. Kinyume chake mmiliki wa tovuti atachukuliwa hatua. Hapa tunaenda kwenye kile kitu kilichowafanya Google kutimka Uchina( censorship). Chukulia mfano leo hii unataka kuweka habari kwenye Facebook, ni lazima uhakikishe ile habari ni yako au mmiliki anaruhusu kuiweka kule, la sivyo itakuwa ni kosa.

  [​IMG]
  Wananchi marekani wakipinga sheria hiyo

  Kutokana na maelekezo yaliyomo kwenye sheria hiyo,tovuti zote za marekani zinatakiwa zisifanye biashara wala kuionesha tovuti yoyote ambayo itapatikana na kosa na kwenda kinyume na sheria hii, hii inamaanisha kila tovuti inatakiwa kuwa makini katika mambo mawili

  1. Kuangalia kila taarifa wanayoweka haijavunja sheria ya haki miliki(censorship)
  2. Kutofanya biashara ya namna yoyote na kampuni yoyote iliyo nje ya Marekani ambayo imeorodheshwa katika wakiukaji wa sheria hii.
  Kwa muono wa mbali, hatua hizi ni kuzuia uhuru wa intanet kama wenyewe wanavyouita( Internet Democracy)

  Je sisi inatuhusu?

  Swali ambalo unaweza kuanza kujiuliza, sheria ya marekani inatuhusu vipi sisi Watanzania? Ukweli ni kuwa sheria hii haitoishia marekani tuu, kwani makampuni ya marekani hayatoruhusiwa kufanya biashara na kampuni yoyote duniani ambayo imevunja sheria ya Marekani na kutofanya hivyo ni kutenda kosa. Pia wasajili wa majina, wahifadhi tovuti(hosting) watatakiwa kuiondoa tovuti yoyote iliyokiuka sheria hii toka kwenye seva zao na mengine mengi. Sheria hii itakuwa na athari kubwa mno kwa mataifa yanayoendelea kama Tanzania ambao hatuna vitu vya kwetu wenyewe.
  Hivyo basi, kwa mtazamo wangu naona sheria hii ni changamoto kwetu kujitahidi kuwa na vitu vyetu wenyewe kitu ambacho kitatufanya tuweze kusimama bila shaka kwani kila taifa huleta sheria ambazo zina faida kwao. Ingawa sheria hii imepata upinzani mkubwa toka kwa wamarekani, lakini haukutungwa kwa ajili ya kuwashambulia wamarekani, ni kwa ajili ya mataifa ya nje ila kwakuwa tunaishi katika ulimwengu ulioungannika hivyo kwa njia moja au nyingine wamarekani nao wataathirika. Si unakumbuka waziri mkuu wa uingereza alivyoshikia bango mambo ya jinsia moja na kuzilazimisha nchi zetu kufuata matakwa yake?


  Kutokana na sababu hizo, makampuni mengi ya ya intaneti yanaod=na sheria hii ni kama kuwaziba midomo na kuanza kuwa China ya pili.

  Chanzo: Ughaibuni.com
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hii ishu ililetwa na FF sijaona watu wakiichangamkia ngoja tuone maoni ya wengine..
   
 3. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Sheria hii ni mwendelezo wa kile WAMAREKANI wanachokiita VITA DHIDI ya UGAIDI, kwa kumbukumbu zangu Rais OBAMA alipata kusema maneno haya "kwa sasa hatuna tena uwezo wa kupigana VITA MBILI, badala yake tutafunga vita ya IRAQ na AFGHANISTAN na kutilia mkazo kwenye ULINZI wa ANGA na VITA YA UGAIDI KATIKA MITANDAO"
  PIPA na SOPA ni mkakati madhubuti wa kupata taarifa kamili za Muhusika juu ya kile anachofanya
   
 4. r

  rebeca Senior Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  he at list nimepata kapicha,nilivyoizowea facebook...leo naona kama mwaka.lol
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Je wataweza?? HIli ndilo linabaki swali langu kuu
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Intaneti ulikuwa ni mtandao unaotumika katika jeshi la US pekee baada ya kuvumbuliwa, kwa ajili ya urahisi wa mawasiliano yao (kama ilivyokuwa kwa GPS), baada ya majeshi ya US kupata mtandao mwingine wa haraka zaidi na "secure" zaidi wakaamuwa wautoe huu uwe public na uzalishe, hapo hapo idara za intelijensia na propaganda zitautumia kwa manufaa ya US.

  Baada ya muda kupita na kila kitu kuwa shwari kama matarajio yao, imefikia wakati uvumbuzi wa mambo ya mtandao umezidi kwa kiasi cha haraka sana kuliko ilivyotegemewa na kuna njia mbadala za kukwepa kugundulika na ni nani, watu wametengeneza "programs" chungu nzima za kuweza amma kubadilisha kujulikana kwa urahisi chanzo kiko wapi amma kuweza hata kuwa na mitandao ndani ya mtandao ambayo iko "highly encrypted" kiasi cha kuweza kui "secure" na ku i "monitor" yote imekuwa ni vigumu sana kwa intelijensia za US. Kilichobaki na njia rahisi na ya mbadala ni kuweka sheria za kuweza kubana inapobidi na kuwachia inapobidi bila Serikali kuingia matatani kwa kushtakiwa na kulipa gharamma zisizo mfano.

  Hii ni moja katika kuendeleza ubabe na kuendeleza kula uliwe.

  Mtandao ambao ulikuwa mkubwa baada ya huu wa jeshi US (kwa enzi hizo) na ambao ulikuwa "independent" ulikuwa ni wa shirika la usafirshaji barua na vifurushi FeDex.

  Huku tukitaka tusitake tupo monitored na controlled, iwepo SOPA na PIPA ama isiwepo. Hatuna ka "private" na "independent" mtandao hata kajeshini tu au Kaserikalini tu. Tunategemea huu huu ambao atakae anatuchungulia.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kama ilivyo piracy kukaa bungeni kutunga sheria ni kazi rahisi lakini utekelezaji wake na monitoing ni kazi au gharama kubwa sana. So Kisiasa ni rahisi wameshakula posho lakini utekelezaji ..............................................

  chukulia mfano wa Piracy ambayo hao hao wamarekani wameweka sheria kali na ipo toka zamani . Kwa mujibu wa alexa (wanaotathmini matumizi ya tovuti) hata USA hii site ipo kwenye site 100 zinazotombelewa sana na watu walioko USA..... Unaona hapo??????

  Uzito mwingine unakujua kwenye monitoring. Nani atafanya monitorng. Hapa ni wazi utekelezaji wake ni mpaka mtu alalamike. So Muhusika mpaka ajue Jammiforum au media fire kuna member wameweka article ya kitabu au kitabu chake bila ruhusa ipo kazi. Ok inaweza kuwa ugumu kidogo kwa USA lakini kwa upande wa nchi zetu ugumu wa utekelezaji wake unaongezeka.

  Tatizo lingine naona USA itopoteza share kubwa ya makampuni yanayofanya biashara yaku Host tovuti wakiendelea hivi. Wawekezaji wataanza kukimbilia nch zinazofagilia sana Sharing na Openess kama Sweeden, Finland na kwingineko.

  Makampuni kama facebook yataaithirka kuna facebook ya kichina na version nyinginezo nyinginezo kwao itakuwa kicheko. Sababu Itakuwa kama kuwafukuza wateja kwenye fab USA wanweza kukimbiia sehemu nyingine. Site kama wikipedia ni user wanaafafanua mambo kutoka kwenye vitabu mbali mbali walivysoma na kunukuu Lakin isio user wote wanaoreference source. Sasa kwa case ukiwaadhibu wikipedia kwa kosa la mtazamaji kuplagrise nayo si sawa. ..... lol

  Lakini kwa upande mwingine sheria ina faida zake
   
 8. marregal

  marregal Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kusoma online yaweza kuja kuwa ndoto, na pia expert wa kuhack watapata difficultiness,, maujanja yatapungua, economization of credit will be difficult when downloading or copyrighting items. this is due to the proposal of establishing a network wall that will only allow legal and authorised entries, illegal ones like downloading and copyright will be check and if nt valid, access is burned,,
  according to the us reporters, they say there is no possibility for it to happen this year but as tyms pass by, the necks of the government are about to be tied with the bill to grant it, the opposers are seeking votes to crash down the bill before it gets worse, how will the world be inforecoming years without this networking,, ni tabu kwelii maana no freedom kabisa..:A S-coffee:
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Shukrani sana mkuu kwa hii taarifa. Nilikuwa nahitaji sana information kuhusu hii SOPA na PIPA sasa nimepata jibu
   
 11. HT

  HT JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Populist Protest Kills SOPA (Again) - Haya muswada wa SOPA umeshindwa hata kabla haujafikikishwa "bungeni"

  Sehemu ya Nukuuu

  So SOPA kwa sasa inaweza kuwa interest kwa USA na mataifa machache lakini sio kwa China India na mataifa kama .Tanzania.
   
Loading...