hii ni mara ya tatu anatuletea fujo, mara ya kwanza kahamisha msiba kutoka geita na kuuleta mwanza bila sababu za maana nayo ikaleta taharuki kweli, mara ya pili kaja kwenye kesi ya wenje wakati anajua kabisa huyo jamaa yake alishindwa uchaguzi bado akatuletea jam mjini, kaja tena! hapana uvumilivu umetushinda.
Ujue panapotokea kurupushani za kisiasa tunaoumia wa kwanza ni wafanyabiashara, maduka yanavunjwa bidhaa zinaporwa wateja wetu wanakimbia kwa hofu na mauzo yanadorora wakati huo huo marejesho ya bank yako palepale, kodi zinatusubiri wafanyakazi wetu wanataka mishahara na makanisani tunatakiwa tuwakilishe zaka. sasa mji wetu wakati wa amani tu tumebanana bado mjinga mwingine atuletee jam za kipumbavu, kaacha kujadili budget anakuja kutuletea jam mjini.
hakuna cha katiba hapa anatetea pesa kutoka chama cha centre party cha Norway kupitia TDC, anafanya show apeleke clip kwa wafadhili apate mpunga, safari hii huyo mwakili wao lazima tumkamate airport anajifanya kutumia passport ya Tanzania.Ndo hivyo tena katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa nafasi mtanzania kufungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu popote ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.
Labda Bunge lifanye marekebisho ya sheria kwa hati ya dharura kwa kutumia wingi wa wa-Bunge wa CCM bungeni lakini katika hali ilivyo sasa hakuna jinsi kesi imefunguliwa Mahakama Kuu jijini Mwanza na imetimiza mahitaji yote kisheria na kikatiba kusikilizwa katika mji wenu wa Mwanza.
Jumatatu tunapeleka shauri mahakama ihamishie shauri lao Bariadi kwa sababu za kiusalama wakakae huko na majaji wao watuache tufanye biashara.Dah! Nimekuelewa mkuu changamoto mlionayo ila kuwa mpole na mvumulivu ili sheria na katiba ''tuliyojiwekea'' kupitia Bunge ichukue mkondo wake kupitia tafsiri sahihi itakayotolewa na waheshimiwa ma-Jaji wa Mahakama Kuu itakayotupa mwelekeo wa kesho .
Jumatatu tunapeleka shauri mahakama ihamishie shauri lao Bariadi kwa sababu za kiusalama wakakae huko na majaji wao watuache tufanye biashara.
Aulizwe tu ataandamana vipi wakati Polisi wamepiga marufuku mikutano na maandamano nchi nzima?Jamaa umekomaa kweli, sasa ni hivi, hakuna mtu wa kuacha shughuli zake afanye maandamano.
Mtu ana haki ya kufungulia kesi popote anapoona inafaa!Kuanzia Ijumaa kutakuwa na Maandamano ya kupinga mwenyekiti wa chadema kuendesha kesi Mwanza kwa sababu za kiusalama. Yeye anamatatizo yake na polisi kule kahama hajaenda kufungua kesi Tabora kaja kufungulia mwanza kama sio kuleta fujo za kijinga. Tutaandamana kuhakikisha anaondoka hatukubari kutuharibia mji wetu.
Watu waachwe wafanye biashara zao na shughuli za kujipatia kipato, siaende moshi arusha na dar aliko na wafuasi wengi, siakafungue kesi shinyanga mjini, kinachomleta mwanza ni nini kama sio kuleta fujo za hovyo tu, hapana. Sasa tutaandamana na kufurumusha wafuasi wake hadi nyashishi. Hatutaki ujuha.
Mwenye hekima hunyamaza akiwa hana la kusemanani kakwambia mbowe ni mwananzengo wa mwanza? hatumtaki na wenje wake tumeshamtupa kule sijui anatutafutia nini huyu baba? hiyo kesi yake akaifungulie mahakama ya mwanzo ibinzamata, safari hii lazima ziumane tu tumechoka sasa.
Kabisa huyu mtu anataka kuhalibu mji wa mwanza ...naunga mkono hoja
Mistari yote hiyo hakuna hata neno Ufisadi...chadema hampingi tena ufisadi,ufisadi mmeupa mgongo....chadema mmekuwa chanda na pete na ufisadi...chadema nyinyi Mungu anawaonaNi Fujo Gani Mbowe alifanya Mwanza? Kwa Hiyo Maandamano ya Propaganda za Magufuli ni sawa Lakini ya Vyama Vingine ni haramu?. Mi Nasema Kuwa Kuna Rafiki yangu Mmoja amemsifia sana Magufuli akasisitiza apewe Uwenyekiti wa CCM. Ni haki yake kusema Hivyo, Ila Tunatofautiana, Mimi Niliamini Katika Mabadiliko Tanzania, Mabadiliko ya Kuboresha Huduma za Jamii, Mabadiliko ya Kuimarisha haki, Uhuru na Demokrasia, Kwa Mtazamo wangu Magufuli hana Uwezo wa Kuwa Rais, hana Hekima ya Ustahimilifu wa Kufikiri kwa Makini Kubeba Mzigo mzito wa Maamuzi magumu ya Nchi kwa Kutenda haki. Mimi Nilimpenda sana, Lakini Nilikuwa Chongo, Pamoja na Kuwa Magufuli ni Mchapakazi, asiyependa mchezo, Urais haumfai, anapenda sifa, anakurupuka na Ni dictator. CCM Walikosea Kumpa Tikiti, lakini Watakuwa Wametenda dhambi ya Mauti Kumpa Umwenyekiti. Lazima awepo wa Kumdhibiti huyo Mh.
Gari lako aina gani? Kwanini usipeleke hoja hiyo mahakamani kama Kahama jiografia yake ya kimahakama ni Tabora? Hebu anzisha hayo maandamano yako ya kwenye keyboard tuone!usukuma unatoka wapi hapa? wacha kuhamisha hoja ya msingi? nani kakwambia wakazi wa mwanza ni wasukuma pekee, wenje mjaluo tulimpa ubunge kiwia mchagga tulimpa ubunge, huyu anayekuja kutuvunjia vioo vya magari hata kama ni mnyantuzu hapana, ujinga huo apeleke hukoo!
naona unapalilia ukabila hapa. mwanza sio mji wako wewe binafasi bali wa watanzania wote.nani kakwambia mbowe ni mwananzengo wa mwanza? hatumtaki na wenje wake tumeshamtupa kule sijui anatutafutia nini huyu baba? hiyo kesi yake akaifungulie mahakama ya mwanzo ibinzamata, safari hii lazima ziumane tu tumechoka sasa.