Hakuna lolote kuwa jeshi la polisi limejifunza kitu, jana hawakupata order toka juu hivyo viongozi wa polisi hawakujua wafanye nini maana wamezoea kusimamia wanayoambiwa na viongozi hao na ndiyo maana wanaviburi.
Kweli mkuu, viongozi wa jeshi letu la polisi hawajui kazi zao, wao wanasubiri kupokea amri kutoka kwa magamba na wao wanazitekeleza bila hata kufikiria, ndio maana mpaka waziri aongee ndio mtu anahojiwa japo ana kosa. Mpaka leo wameshindwa kuwakamata wezi wa EPA kwasababu hawajaambiwa!!. Nilikuwa na imani sana IGP Mwema nikitegemea angetumia uzoefu wake wa interpool lakini masikini naye ameingia kwenye mkumbo uleule.