Maandamano ya kumsindikiza Lema alipotoka Lupango, Polisi walifyata mkia...

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Sikuelewa kilichotokea baada ya Mh Lema kupata dhamana. Pengine katika hali kama ile akili na macho vimeshazoea kuona polisi wakiwa na mabunduki yao. Hata hivyo pamoja na maandano yasiyo rasmi. Sikuona polisi hata mmoja. Inaonekana jeshi letu sasa linaanza kukua na kupata akili..
 
Polisi wa nchi hii ni wakorofi sana hawatumii hekima, busara wanapenda nguvu hata pasipo sitahili haya nimejifunza MBY wakitumia nguvu hata kama hali imetulia Kwa ushauri wangu si lazima sana pasipo lazima nguvu zitumike kama amani inavunjika
 
Chadema wampokea Lema kwa kishindo Send to a friend
Monday, 14 November 2011 21:45
0diggsdigg

juu-juu-lema.jpg
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema,akiwa juu ya gari lake nje ya uwanja wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha,baada ya kupata dhamana katika kesi ya kufanya maandamano na kufanya mkusanyiko bila kibali cha polisi. Picha na Filbert Rweyemamu

Peter Saramba na Mussa Juma, Arusha
SHUGHULI mbalimbali za kibiashara na kijamii katika Jiji la Arusha jana zilisimama kwa muda kupisha mapokezi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema baada ya kutoka rumande katika Gereza la Kisongo alilokaa kwa siku 14.Oktoba 31, mwaka huu, Lema na wenzake 18 walifikishwa mahakamani wakidaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali na kukaidi amri ya polisi iliyowataka watawanyike yeye na wenzake.Walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kudhaminiwa lakini Lema akikataa dhamana akisema ameamua kutangulia gerezani kudhihirisha kwamba haogopi gereza.Lema alitoka kwa dhamana na kuandaliwa mapokezi makubwa ya wafuasi wa Chadema ambayo yaligeuka kuwa maandamano ya amani.Shamrashamra za mapokezi hayo zilisababisha kusimama kwa muda kwa shughuli kadhaa kama huduma za kibenki hasa zile zilizo katika Barabara ya Sokoine.

Wakati wa maandamano hayo wafuasi hao wa Chadema walikuwa wakipeperusha majani na matawi ya miti.
Mahakimu, mawakili na makarani wa mahakama nao walilazimika kuacha shughuli zao kwa muda na kutoka nje kushuhudia mapokezi ya mbunge huyo yaliyokuwa yakipambwa kwa nyimbo mbalimbali nje ya mahakama hiyo.

Sehemu ya nyimbo hizo zilimgusa Mkuu wa Polisi Wilaya hiyo ya Arusha, Zuberi Mwombeji ambaye hivi karibuni aliingia kwenye mvutano mkubwa na chama hicho cha upinzani akituhumiwa kutumia nguvu kuwadhibiti viongozi wake.Waliimba: "Tunamtaka….panya wetu… tunamtaka mbunge wetu… Zuberi (OCD), aondoke. Mlituvizia usiku, leo sasa ni mchana hapatatosha. Hatuandamani, tunampokea shujaa wetu."

Shamrashamra hizo pia ziliambatana na mabango mbalimbali huku pia kukiwa na fulana maalumu zilizokuwa zimevaliwa na baadhi ya mashabiki zikiwa na maneno yaliyosomeka: "Lema kaonyesha njia mbadala ya kudai haki. Jela ni mahali pa kuishi kama sababu ya kwenda huko ni vita
dhidi uonevu, ukandamizaji wa haki na utu wa binadamu."

Mahakamani
Lema aliyefika mahakamani Saa 3:20 asubuhi akiwa ndani ya gari maalumu ya polisi, alipewa dhamana na Hakimu Mkazi, Judith Kamara baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho na barua za utambulisho ambao walisaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni kila mmoja.

Alidhaminiwa na Sarah Mohamed na Mwajuma Manonge na kutoka eneo la Mahakama Saa 5:15 asubuhi akiwa amebebwa juujuu na wafuasi wake baada ya juhudi zake za kutaka kuondoka kwa kutumia gari lake kushindikana.Wafuasi hao walimzuia kuingia katika gari lake na kumtaka atembee kwa miguu hadi eneo la Ngarenaro ziliko Ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha.
Mbunge huyo hakuwa na budi kukubaliana na agizo hilo la wafuasi wake kuongozana hadi Ngarenaro lakini aliwasihi wamruhusu apande na kusimama juu ya gari lake, ombi lililokubaliwa.

Licha ya mashabiki hao wa Chadema kulazimisha kumbeba Lema juujuu na kuanza kutoka naye eneo la Mahakama huku wakiimba, Kamanda wa Operesheni Maalumu za Polisi Mkoa wa Arusha, Peter Mvulla aliwaamuru askari wake waliokuwa wakilinda amani eneo hilo kutowaingilia.

"Waacheni waandamane na mbunge wao, msiwapige mabomu. Subirini tuangalie kitu gani kitatokea. Kama hawafanyi vurugu msiwaingilie hadi nitakapotoa amri nyingine. Muhimu hakikisheni mmejipanga sawasawa kila eneo," alisikika Mvulla akitoa maelekezo kwa simu.
Busara za Mvulla aliyekuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi katika shughuli ya jana, zilisaidia kuepusha vurugu katika mapokezi hayo yaliyoishia kwa Lema kuwahutubia wafuasi wake nje ya ofisi za chama hicho mkoa huku amani na utulivu vikitawala.

Mkutano hadhara
Akihutubia umati mkubwa wa watu nje ya ofisi hizo, Lema alisema Serikali isidhani kuwa ina uwezo kutumia dola kusaidia CCM Arusha na kuonya kwamba, yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ili kuruhusu uchaguzi mdogo akiahidi kunyakua tena kiti hicho kwa kura zaidi ya 56,196 alizopata kwenye uchaguzi uliopita.

"Maisha yangu siyo kwa ajili ya kuishi leo, bali kufa kwa faida. Ndiyo maana kila siku nasema ni heri vita inayotafuta haki, kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mtu," alisema huku akishangiliwa.Alisema jana usiku alipanga kuelekea Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kushiriki mjadala wa Katiba Mpya akionya kuwa iwapo kutakuwapo uchakachuaji ataanzisha balaa jingine kubwa kuliko la Arusha.

Amjia juu RC
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano hayo, Lema alisema suluhu ya mgogoro wa Arusha utapatikana kwa uchaguzi wa umeya kurudiwa na kumuonya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo kuacha kudandia gari asilojua linakoelekea akimaanisha mgogoro unaoendelea.
"Bila haki kupatikana, sasa tutaanza maandamano kwenda majumbani mwa viongozi wanaokandamiza haki zetu. Waandae risasi na mabomu ya kutosha kwani mapambano ndiyo kwanza yameanza. Eti RC anauliza kwa nini hatuandamani sehemu nyingine, tukaandamane sehemu kama Tabora ambako hakuna sababu ya kufanya hivyo? Arusha tuna sababu ya kuandamana," alisema Lema.

Kuhusu kauli aliyodai ya vitisho kutoka kwa Mulongo aliyeonya wanaopanga kuvuruga amani na utulivu Arusha, Lema alisema kiongozi huyo bado anakabiliwa na ugeni ndiyo sababu anatoa kauli bila kuzifanyia utafiti.

Jiji la Arusha limekuwa likigubikwa na vurugu za kisiasa mara kwa mara tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ambao pamoja na mambo mengine, uliacha majeraha yanayotokana na matokeo ya uchaguzi wa umeya ambao Chadema umekuwa ukiyapinga.

Sikuelewa kilichotokea baada ya Mh Lema kupata dhamana. Pengine katika hali kama ile akili na macho vimeshazoea kuona polisi wakiwa na mabunduki yao. Hata hivyo pamoja na maandano yasiyo rasmi. Sikuona polisi hata mmoja. Inaonekana jeshi letu sasa linaanza kukua na kupata akili..
Hakuna lolote kuwa jeshi la polisi limejifunza kitu, jana hawakupata order toka juu hivyo viongozi wa polisi hawakujua wafanye nini maana wamezoea kusimamia wanayoambiwa na viongozi hao na ndiyo maana wanaviburi.
 
Naweza kusema ya kwamba! Huyu RC anaweza akaacha hili jiji kama alivyoikuta,nasema hivyo kama hata jirekebisha mapema iwezekanavyo,hapa siyo huko alikotoka na ajuwe kbs ya kwmb yeye kachaguliwa na kidole kimoja hilo ajuwe kabisa,kama hata hapitii mitandao tunaomba wapambe wake wakamweleze ya kwmb raia wanataka ajirekebishe mara moja,pamoja na huyu OCD aliyewaita raia panya,hakika huyu tutahakiki ya kwmb ataenda kufanya kazi mahala asiyetaka tena si nyingi na kama anataka raia wamsikie yeye angewaomba raia msamaha (radhi) kwa hali ile ya kuwaita raia panya. Kamwe hatutasahau ila hatutakoma ktk hali yoyote itakayobidi kutokea hapa Arusha maana tuna haki na tuna kila sababu ya kufanya kila linalojiri kwa AMANI na siyo tuzuiwe na mafisadi kwa manufaa ya mapapa na matumbo yao. KAMWE HATUTAKUBALI NA HAWA POLISISISIEM WAENDELEE KUJITUMA ZAIDI NA KUUA NA KUWEKA VILEMA RAIA INGALI WANATUMWA NA MAFISADI NA WANAJUA HILO LAKINI WATAKUJA JUTA NA HALI ILE ITAWARUDIA TENA SIKU SI NYINGI.
 
Jana polisi waliishiwa mabomu, waliyatumia kuwapiga wanafunzi wasio na hatia wa Makumira Uni.
 
Siku zote polisi ndio wanaosababisha vurugu kwenye mikutano na maandamano.... Wakiacha watu wakiandamana wenyewe hakuna vurugu zinazotokea...... Hili lapaswa kuwa somo kwa polisi ingawa sijui uwezo wao wa kujifunza maana yawezekana umeshafikia kikomo..
 
Naweza kusema ya kwamba! Huyu RC anaweza akaacha hili jiji kama alivyoikuta,nasema hivyo kama hata jirekebisha mapema iwezekanavyo,hapa siyo huko alikotoka na ajuwe kbs ya kwmb yeye kachaguliwa na kidole kimoja hilo ajuwe kabisa,kama hata hapitii mitandao tunaomba wapambe wake wakamweleze ya kwmb raia wanataka ajirekebishe mara moja,pamoja na huyu OCD aliyewaita raia panya,hakika huyu tutahakiki ya kwmb ataenda kufanya kazi mahala asiyetaka tena si nyingi na kama anataka raia wamsikie yeye angewaomba raia msamaha (radhi) kwa hali ile ya kuwaita raia panya. Kamwe hatutasahau ila hatutakoma ktk hali yoyote itakayobidi kutokea hapa Arusha maana tuna haki na tuna kila sababu ya kufanya kila linalojiri kwa AMANI na siyo tuzuiwe na mafisadi kwa manufaa ya mapapa na matumbo yao. KAMWE HATUTAKUBALI NA HAWA POLISISISIEM WAENDELEE KUJITUMA ZAIDI NA KUUA NA KUWEKA VILEMA RAIA INGALI WANATUMWA NA MAFISADI NA WANAJUA HILO LAKINI WATAKUJA JUTA NA HALI ILE ITAWARUDIA TENA SIKU SI NYINGI.

Gaddafi aliita raia wake waliokuwa wanataka haki kuwa panya, huyu nae kawaita watz panya, redio na mihadhara ya waislamu inaita wasio waislamu kuwa makafiri mie nadhani hata viongozi wengine wengi wa nchi hii wa mlengo ama imani ya gaddafi wanawaona wasio waislamu ni mapanya na makafiri. Hainishangazi sana kwani sasa naamini dini yao huwafundisha hivyo. Cha maana hapa viongozi wa dini hiyo hata mnapoomba kura msimamapo jukwaani ombeni kura zote mbili yaani waislamu wenzenu na kura za mapanya na makafiri waziwazi
 
CCM wanadhani polisi ndo kama kila kitu, tujiulize Kenya, Somalia, Libya, Egypt na kwingineko hawakuwa na polisi? Kama tumeshindwa kuwaletea wananchi kile walichokitarajia basi tuache wao wachague njia nyingine ya kuwaletea maendeleo na sio kuwalazimisha wakipende ccm wakati hata hao ccm wenyewe hawakipendi chama chao kwa kunuka ufisadi.
 
Gaddafi aliita raia wake waliokuwa wanataka haki kuwa panya, huyu nae kawaita watz panya, redio na mihadhara ya waislamu inaita wasio waislamu kuwa makafiri mie nadhani hata viongozi wengine wengi wa nchi hii wa mlengo ama imani ya gaddafi wanawaona wasio waislamu ni mapanya na makafiri. Hainishangazi sana kwani sasa naamini dini yao huwafundisha hivyo. Cha maana hapa viongozi wa dini hiyo hata mnapoomba kura msimamapo jukwaani ombeni kura zote mbili yaani waislamu wenzenu na kura za mapanya na makafiri waziwazi

Kaka hapa umewaambia ukweli yahani msumali umechoma, nimetafuta alama ya like sijaiona.
 
Nyie mkiendelea kuwa na adabu basi hamtaona polisi lakini mkileta za kuleta kipigo kitaendelea. Si mliona Lema alivyo kua na adabu safari hii, jeuri yote kaiacha jela.
 
Polisi wametumia akili sana wafuasi wa Lema, walitaka polisi wawakamate waanzishe fujo...

RPC hakawaambia nyie andamaneni mkitaka hata mfike Kia sisi hatuwagusi
 
Polisi wametumia akili sana wafuasi wa Lema, walitaka polisi wawakamate waanzishe fujo...

RPC hakawaambia nyie andamaneni mkitaka hata mfike Kia sisi hatuwagusi

Kwanini siku zingine huwa hawatumii akili hivyo?Ama tuseme akili za polisi ni za msimu sio?Ama za mwandamo wa mwezi?
 
Maandamano yote huwa na objective. Kwa hili la kuandamana kwa kuachiliwa mtu aliejipeleka rumande sitakaa nilielewe kamwe!
 
Hawa polisi sijui wanapewa mafunzo ya namna gani hapo moshi ila kuna ulazima wa kuyabadilisha.
Haiwezekani tunafika mahali tunawaogopa zaidi polisi kuliko majambazi.
 
Back
Top Bottom