Maandamano ya kumsindikiza Lema alipotoka Lupango, Polisi walifyata mkia...

Hakuna lolote kuwa jeshi la polisi limejifunza kitu, jana hawakupata order toka juu hivyo viongozi wa polisi hawakujua wafanye nini maana wamezoea kusimamia wanayoambiwa na viongozi hao na ndiyo maana wanaviburi.

Kweli mkuu, viongozi wa jeshi letu la polisi hawajui kazi zao, wao wanasubiri kupokea amri kutoka kwa magamba na wao wanazitekeleza bila hata kufikiria, ndio maana mpaka waziri aongee ndio mtu anahojiwa japo ana kosa. Mpaka leo wameshindwa kuwakamata wezi wa EPA kwasababu hawajaambiwa!!. Nilikuwa na imani sana IGP Mwema nikitegemea angetumia uzoefu wake wa interpool lakini masikini naye ameingia kwenye mkumbo uleule.
 
Hebu cheki gazeti la habari leo kama naota vile,

BAADA ya kukaa mahabusu kwa siku 14, hatimaye Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ameachiwa kwa dhamana.
Baada ya kutoka mahakamani wafuasi wa chama chake cha Chadema waliokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha walimbeba huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kukisifu chama hicho.
Lema alipata dhamana jana baada ya awali kukataa dhamana na kutaka kwenda mahabusu.
Siku chache baadaye uongozi wa juu wa Chadema ulifanya jitihada za kuhakikisha anatoka, lakini Novemba 7 Mahakama ilimnyima dhamana hiyo.
Hakimu Judith Kamala alisema dhamana ya Lema ipo wazi, hivyo wadhamini wake wahakikishe anafika mahakamani kadri kesi itakapopangwa na kama hatafika, basi wadhamini hao watoe taarifa.
Alikubali kumpa dhamana Mbunge huyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 14, mwaka huu.
Lema anashitakiwa pamoja na wenzake 18 wakikabiliwa na kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali.
Alidhaminiwa kwa kutolewa kwa barua mbili zenye vitambulisho na ahadi ya Sh 500,000 kila mmoja, ambapo Mwajuma Manonga na Sara Mohamed Kara walimdhamini Mbunge huyo.
Akitoka nje ya mahakama, alilakiwa na wafuasi wa chama hicho ambao hawakujali kama wapo ndani ya mahakama na kumbeba juu huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu na kulibeza Jeshi la Polisi.
Shangwe hizo hazikuishia hapo, ziliendelea huku wakiwa wameshika matawi ya miti na majani na baadhi wakiwa wamembeba Lema na kuanza msafara kwenda ofisi za Chadema Mkoa zilizopo Ngarenaro na kusababisha baadhi ya benki kusitisha shughuli zao kwa muda na nyingine zikifanya kazi; huku ulinzi ukiimarishwa na Benki ya NMB Clock Tower ikifunga kwa muda kutokana na maandamano hayo.
Lema aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikwenda mahabusu si kwamba alikosa dhamana, bali kuonesha namna ya kupinga unyanyasaji wa Polisi aliodai wanabambikia watu kesi hasa wa Chadema.
Alimgeukia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, akimtaka aachane na siasa za Arusha kwani chimbuko la mgogoro wa Arusha ni umeya, hivyo akae chini kutatua tatizo hilo na si kutamka kuwa yeye ni RC hivyo ana wajibu wa kutuliza amani na utulivu.
Source HabariLeo | Lema aachiwa kwa dhamana, wafuasi wambeba
 
Nyie mkiendelea kuwa na adabu basi hamtaona polisi lakini mkileta za kuleta kipigo kitaendelea. Si mliona Lema alivyo kua na adabu safari hii, jeuri yote kaiacha jela.
Jeuri wapi wewe..!hebu toa pumba zako hako hapa.Hata aibu huoni?Kazi kutetea upuuzi tu.Idit.
 
Kwanini siku zingine huwa hawatumii akili hivyo?Ama tuseme akili za polisi ni za msimu sio?Ama za mwandamo wa mwezi?

Akili za polisi sio za mwandamo wa mwezi, ni kwamba huwa wanazikusanya wakitoka depo. Wanagaiwa kidogokidogo wawapo kazini. Sasa we fikiria kufanya kazi kwa akili za kushikiwa inakuwaje hapo.
 
Polisi wametumia akili sana wafuasi wa Lema, walitaka polisi wawakamate waanzishe fujo...

RPC hakawaambia nyie andamaneni mkitaka hata mfike Kia sisi hatuwagusi

Siku nyingine wanatumia Masaburi yaliyo pevuka kwenye fikra zao
 
Siku zote polisi ndio wanaosababisha vurugu kwenye mikutano na maandamano.... Wakiacha watu wakiandamana wenyewe hakuna vurugu zinazotokea...... Hili lapaswa kuwa somo kwa polisi ingawa sijui uwezo wao wa kujifunza maana yawezekana umeshafikia kikomo..

hili ndilo neno la mwaka!!! message of the year 2011
 
Arusha ni beghazi na dar ni tripoli........kwa mpango lazima kieleweke lema upo juuuuuuu
 
Gaddafi aliita raia wake waliokuwa wanataka haki kuwa panya, huyu nae kawaita watz panya, redio na mihadhara ya waislamu inaita wasio waislamu kuwa makafiri mie nadhani hata viongozi wengine wengi wa nchi hii wa mlengo ama imani ya gaddafi wanawaona wasio waislamu ni mapanya na makafiri. Hainishangazi sana kwani sasa naamini dini yao huwafundisha hivyo. Cha maana hapa viongozi wa dini hiyo hata mnapoomba kura msimamapo jukwaani ombeni kura zote mbili yaani waislamu wenzenu na kura za mapanya na makafiri waziwazi

MKUBWA! Yani nimeilike sana hii ngoja kidogo tu! Ntarudi.
 
Sikuelewa kilichotokea baada ya Mh Lema kupata dhamana. Pengine katika hali kama ile akili na macho vimeshazoea kuona polisi wakiwa na mabunduki yao. Hata hivyo pamoja na maandano yasiyo rasmi. Sikuona polisi hata mmoja. Inaonekana jeshi letu sasa linaanza kukua na kupata akili..

wamechoka hao, wanakesha usiku kucha kulinda mkesha wa wananchi bila malipo ya night wala nini, wamechoka hao!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom