Eberi M. Manya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 743
- 280
Kuna Maandamano fake yanafanywa na CCM hapa Moshi mjini leo kuelekea kwa Mkuu wa Mkoa Amos Makalla.
Maandamano hayo yaliratibiwa na Davis Mosha mgombea ubunge wa chama hicho pamoja na wafuasi wake huku wakilalamika kwamba wanaonewa na kufanyiwa vurugu na chadema. Hali hii imewastua wananchi wote wa Moshi maana wanaofanya vurugu Moshi mjini ni Davis Mosha na wafuasi wake baada ya kubaini kushindwa uchaguzi siku ya tarehe 25 Jumapili hii.
Lengo kubwa la Davis Mosha na wafuasi wake ni kuvuruga amani ya Moshi na kuleta vurugu na kupandikiza chuki na kesi mbalimbali kwa wapinzani wao chadema ili uchaguzi uahirishwe siku hiyo.
Jambo linaloshangaza watu wengi hapo Moshi ni kwamba vurugu hizo za Davis Mosha na wafuasi wake wa CCM zimekuwa zikifanyika mbele ya jeshi la polisi pasipo jeshi hilo kuchukua hatua yeyote na kuonesha wazi kuwa wanamwuunga mkono Davis Mosha.
Kama uchaguzi huo utavurugika na kujawa na fujo na mivutano mikubwa, basii jeshi la polisi watakuwa ni wa kulaumiwa maana hawachukui hatua yeyote dhidi ya Davis Mosha. Inaoonekana polisi wapo pamoja na Davis Mosha na wafuasi wa CCM kuvuruga uchaguzi huu.
Pia Mkuu mpya wa mkoa Kilimanjaro Amos Makalla naye ameonesha kumwuunga mkono Davis Mosha pasipo kuangalia pande zote mbili. Mkuu huyo wa Mkoa ni kada aliyekubuhu wa CCM asiyejua mipaka ya mamlaka yake hasa wakati huu wa uchaguzi.
Davis Mosha amekuwa akiingilia mikutano za kampeni za Chadema na kuwapiga wafuasi wa chadema na hata kuzichana bendera zao mbele ya jeshi la polisi pasipo jeshi hilo kumchukulia hatua yeyote.
Wafuasi wa Chadema wameionya polisi na mkuu wa mkoa wasipochukua hatua madhubuti ili kuzuia vurugu hizo watajibu mapigo haraka iwezekanavyo, na kuwa wakijibu mapigo Moshi hakutakalika tena.
Wakazi wote wa msnispaa ya Moshi wanataka uchaguzi wa amani na utulivu ili haki ya kidemokrasia ichukue mkondo wake. Davis Mosha, Wafuasi wa CCM, Mkuu wa mkoa na viongozi wa CCM wasiwe sehemu ya kuvuruga mwenendo wa uchaguzi na kuleta fujo na adha zote hapa Moshi mjini. Tunawaomba waheshimu sheria na taratibu za uchaguzi.