Maandamano ya Amani Nchi Nzima

Maandamano ya Amani Nchi Nzima

Nonda,

Anza na wadau huko huko Gongo La Mboto Mwisho wa Lami,SunguraTex(KIU), Mombasa, Mzambarauni, Mzizini na Majohe

Nategemea Viongozi pia wamesikia muda umekaribia, Rais Wangu amesema Januari analianzisha la katiba.

Ishu ya katiba ifunguliwe Rasmi na Maandamano haya ili watu wafahamu, kIsha Operation Katiba Ianze.

Hawa ni wezi na Mafisadi wanaokumbatiana, hakuna kuwaogopa Tena.

Namuogopa MUNGU pekee, hivyo namtiii- Mafisadi siwaogopi nikifa mimi najua Elfu watasimama badala yangu
:whoo:
Peoples......Power
 
GrEaTthinkers,

Think kiasi gani tumepoteza kama taifa,

Kwa nini jasho letu linatumika vibaya hivi!
  • TICTS
  • RADAR
  • NDEGE YA RAIS
  • SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
  • TWIN TOWERS BOT
  • MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Madini)
  • KAGODA(EPA)
  • MEREMETA
  • RICHMOND/DOWANS
  • WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
  • IPTL
  • KIWIRA COAL MINES
  • NETGROUP SOLUTIONS
  • MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
  • ALEX STEWART
  • BEI YA BIDHAA ie. UMEME (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
  • RITES
  • ALLIANCE AIR
  • KUJENGA BARABARA KUPITIA MBUGA YA SERENGETI(Matumizi mabaya ya kodi zetu)
  • LOLIONDO
  • BARABARA YA KILWA NA MANDELA KAZI KURUDIWA(Matumizi mabaya ya kodi zetu
Nasema hawa si wa kuchekea wanaiumiza Nchi,

Kwa Asili ni sisi ni matajiri, tunafilisiwa na wapuuuzi

Haiwezekani madudu yote hayo, hakuna hata mwenye hatia ukitoa Liyumba.

Ukinunua soda ya 500Tsh umetoa 90Tsh. kama kodi.

Amkeni, Toeni sauti, Nchi inakwisha.:target:

umesema vyema. tatizo ni hapo kwenye red. pananikumbusha hadithi ya dada niliyemuona leo barabarani akifagia lami huku akiwa amevalia kofia ya CCM.

nchi yetu ina matatizo kweli. lakini hata sisi watanzania tuna matatizo
 
Nonda,

Anza na wadau huko huko Gongo La Mboto Mwisho wa Lami,SunguraTex(KIU), Mombasa, Mzambarauni, Mzizini na Majohe

Nategemea Viongozi pia wamesikia muda umekaribia, Rais Wangu amesema Januari analianzisha la katiba.

Ishu ya katiba ifunguliwe Rasmi na Maandamano haya ili watu wafahamu, kIsha Operation Katiba Ianze.

Hawa ni wezi na Mafisadi wanaokumbatiana, hakuna kuwaogopa Tena.

Namuogopa MUNGU pekee, hivyo namtiii- Mafisadi siwaogopi nikifa mimi najua Elfu watasimama badala yangu
:whoo:
Peoples......Power

Mkuu,

Nimekufahamu vizuri tu.

Usisahau wazo ni maandamano nchi nzima, sio Dar tu.

Kwa hiyo, kutokana na wananchi wengi kutokuwa na muamko ndio maana nikashauri kutumia network ya vyama vya upinzani,katika kila mji,wilaya ,mkoa Tanzania kuna at least network ya chama kimoja cha upinzani ,hii itafanya kazi ya kuelimisha wananchi juu ya haya uliyoyaorodhesha kuweza kufafanuliwa kwa wananchi.

Wananchi wakishaelimika juu ya hili basi ugumu utakuwa umepungua, atakapotokea kuandamana atajuwa mtu anaandamana kwa sababu gani. Sio kuja kusema nimeeambiwa na kiongozi wangu au mtu fulani niandamane.

Ili maandamano yawe na impact tunayoitegemea basi ni lazima yapangwe, yapangike yasiwe ad hoc ! yakiwa adhoc ni rahisi kuwa branded « wahuni wachache ! ». na polisi hii tuijuavyo, watapata kazi wanayoipenda, kuwadhalilisha wananchi. Tusiwape nafasi hiyo au kisingizio.

Unless hapa hatuzungumzii tena « maandamano ya amani » bali ni unrest ! au fujo!

Wazo lako ni zuri mkuu,ila tusikurupuke tu kwa jazba.
 
mkakati ni huu tuma ujumbe wa simu kwa watu unao wafahamu kama walivyofanya msumbiji kwa njia ya simu hili tunaliweza kuingia mitaani hatuna sababu yakuchelea andika hivi wote maandamano ya amani ya kudai vyote vilivyoorodheshwa hapo siku ya jumanne nchi nzima

Anza kutuma wewe kwa maneno hayo hayo uliyoandika tuone mwitikio utakuwaje!
 
Mimi nasema tuamue tusiende kazini siku moja kwa kila mmoja awe mkulima hadi mfugaji lakini hii hamasa tukiiweka kwenye ballot box si tosha kabisa

Watanzania mbona tuna ogopa nimetoa mwelekeo wa nini kifanyika jumanne ,ni kwamba kila mmoja mwana harakati mzalendo wa afrika mtanzania halisi uchukue jukumu andike ujumbe mfupi wa simu kumtaarifu mtu yeyeyote sms zimeanza kutembea kuwa jumanne kutakuwa na maandamano ya amani kudai haki na kupinga hujuma zinazofanywa na mafisadi kupitia serikali ya kikwete sasa unataka nini zaidi ya hili.acheni uoga wakti umefika kama alivyoamua adolf hitlier wa ujerumani ,benitho mussollin huko italia hawa walipambana kiume ndiyo maana leo mataifahayo yana nguvu kiuchumi na mambo mengine
 
Nonda, Ninaposema anza na Karataka na Banana, namaanisha

Aliye shinyanga atadeal na Mejengo mapya, Korandoto, Maganzo nk

Aliye Mwanza aanze na Mkolani, Kitangiri,Bwiru, Igoma nk

Aliye Musoma aanze na Makoko, Mukendo, nyakato nk

Aliye Mbeya aanzia Mafiati,Mwanjelwa,Meta, mbarizi nk,

Aliye Arusha aanza na Sanawari, Kijennge, Kisongo,ngarenaro nk

Aliye Morogoro aanze na Kihonda, mikese, msufini nk

Aliye Babati aanze na Magugu,Endasaki, Dareda nk

Aliye Tanga aanzie Nguvumali, Kisosora, chumbageni, mabawa nk

Namaanisha kila sehemu NOnda.
 
Mkuu,

Nimekufahamu vizuri tu.

Usisahau wazo ni maandamano nchi nzima, sio Dar tu.

Kwa hiyo, kutokana na wananchi wengi kutokuwa na muamko ndio maana nikashauri kutumia network ya vyama vya upinzani,katika kila mji,wilaya ,mkoa Tanzania kuna at least network ya chama kimoja cha upinzani ,hii itafanya kazi ya kuelimisha wananchi juu ya haya uliyoyaorodhesha kuweza kufafanuliwa kwa wananchi.

Wananchi wakishaelimika juu ya hili basi ugumu utakuwa umepungua, atakapotokea kuandamana atajuwa mtu anaandamana kwa sababu gani. Sio kuja kusema nimeeambiwa na kiongozi wangu au mtu fulani niandamane.

Ili maandamano yawe na impact tunayoitegemea basi ni lazima yapangwe, yapangike yasiwe ad hoc ! yakiwa adhoc ni rahisi kuwa branded « wahuni wachache ! ». na polisi hii tuijuavyo, watapata kazi wanayoipenda, kuwadhalilisha wananchi. Tusiwape nafasi hiyo au kisingizio.

Unless hapa hatuzungumzii tena « maandamano ya amani » bali ni unrest ! au fujo!

Wazo lako ni zuri mkuu,ila tusikurupuke tu kwa jazba.

Binafsi nakubaliana na unachosema ni sahihi kwa kiasi kikubwa (i.e theoretically speaking).

Lakini tunahitaji zaidi a much stronger nucleus (kiini) ya huu mkakati. You need think tanks (si vyama vya siasa pls - too unpredictable, these).

Vyama na makundi ya kijamii, NGO, media, etc vitakuwa na guvu zaidi kuliko vyama vya siasa.

Just look at the resulting impact if a certain Sheik Simba or Bishop Pengo makes a statement. Compare and contrast that reaction if a similar (or even stronger) statement is made by the likes of Lyatongas, Mbowes, Mbatias, Zittos, etc.

Sina haja ya kukumbushia impact iliyoletwa na statement za akina Mgaya/Tucta wakati ule.
Nadhani hizi ndizo effective platforms za kutumia. Zinalipa!
 
Naunga mkono maandamano na kama ikiwezekana MAANDAMANO YAWE HATA UINGEREZA ILI UJUMBE UWAFIKIE TOKA KWA WATANZANIA ASILIA PIA. TUMECHOKA INABIDI TUPAZE SAUTI ILI DUNIA NZIMA IPATE HABARI
 
Naunga mkono tuandamane kupinga kwanini watanzania tunakuwa mabwege nasema nikotayari kuandamana hata kufa

Just a few weeks ago we had an election, and the voters have decided...):bump:
Please, Please, Please...you need to be patient till 2015 so that you can voice your anger in the ballot!
Good luck
 
1. Shomari, nani kakudanganya huo msemo kwenye nyekundu ni wa Kikwete??

2. Swali lako....."nani aanzishe" = very simple, tuanze kujiorodhesha hapa hapa:
- M-mbabe
- Spencer
- Iwanga
- Ezan
- Stein
- Byendangwero
- King of Kings
- Bruce Lee
- Wewe mwenyewe (Shomari)
- El Nino (huyu tutambeba juu juu kibabe maana anataka kuleta logic nyingi)

Heshima mbele
mkuu! nilikuwa nakumbushia enzi za Tanzania bila ukimwi. anyway naungana na wewe kuhusu suala la kujiorodhesha, cha muhimu vitu kama hivi vinahitaji muda katika kuvipangilia sababu si vitu vya kukurupuka tu, Ndani ya Jf na kwenye serikali ya Kikwete kuna wasomi wengi tu ambao wanaweza kuandaa rasimu na kisha kufanyiwa kazi, ila sema kwamba Watanzania pamoja na kwamba inawezekana elimu tukawa nayo kichwani sio ile ya jando, tukipata mtu mwenye ujasiri wa kutosha kama yule mwandishi , anaitwa Kubenea, angalau hata mmoja basi tunaweza kuomba maandamano ya amani, pia naungana na mchangiaji mwingine hapo juu aliyegusia suala la kuhusisha taasisi za kijamii n.k . ni kweli kabisa hili suala linawezekana kabisa, suala ni mpangilio tu.
 
Kuandama nchi nzima kudai nini?

Assume maandamano yameruhusiwa yakafanyika what next?

Tuache uchafu kwanza tuufanyao wenyewe (popote ulipo) then utaaminiwa na wengine?

Frankly sioni anayeweza kunishawishi kuandamana wakati najua hata tukiandamana hana jipya atakalofanya?

Heri "afadhali" kuliko "shauri yako"...ushauri tuu
 
JK anakubali ushauri jengeni hoja kwa kutumia njia sahihi kuliko rabsha, rais wetu anasikiliza vizuri tu.
 
nakuunga mkono mkuu huu ukondoo wa watz utatufikisha shimoni, lets send the message to these scum
 
Tuwe wakweli jamani. Migomo yenyewe ya wafanyakazi ambao atleast wamesoma inatushinda kuiandaa. Hivi kweli maandamano ya nchi nzima tutaweza??

Hivi nguvu ya Mgaya imeishia wapi??? Au ndiyo washa m-corrupt??
 
Ni kweli na ni appropriate action,lakini hiyo enormous brainwashing na mind control ambayo imeshafanyika watanzania wana ubavu tena wa ku-rise up against the rulers,I doubt it.

Hata kama ikitokea, it will be limited without much effect. Frankly the ellite have done it we are their zombies. Can a zombie raise up againt the master? Extremely rare, and if it does, the rebellion is crushed with brutal force. Inauma sana, lakini ukweli unabaki kwamba it's too late.

Kumbukeni kwamba huu ni mtandau wa kimataifa,and what is happening in Europe has a strong correlation with what is happening in Tanzania, it's not an isolated incident.
 
Tukiyaita "maandamano" tutalazimika kuomba kibali kwa S. Mwema. Tuyaite " Matembezi ya Amani Nchi Nzima". Mwishoni mwa matembezi hayo tunapeana mikakati ya kuiboresha nchi kiutawala. Faida ya kuyaita "Matembezi" ni kuwa wale ambao walikuwepo tangu enzi za TANU itakuwa rahisi kuelewa somo kwani watakumbuka "Matembezi ya Mshikamano"
 
Tukiyaita "maandamano" tutalazimika kuomba kibali kwa S. Mwema. Tuyaite " Matembezi ya Amani Nchi Nzima". Mwishoni mwa matembezi hayo tunapeana mikakati ya kuiboresha nchi kiutawala. Faida ya kuyaita "Matembezi" ni kuwa wale ambao walikuwepo tangu enzi za TANU itakuwa rahisi kuelewa somo kwani watakumbuka "Matembezi ya Mshikamano"

Hilo nalo neno, matembezi ya amani yakishafanyika next? Nimron ataendelea kutesa, lowassa ataendelea kupanga kuchukua ikulu, RA ataendlea kupewa tender...sijui..manufaa yake..

Hao watakaoandaa (leaders) watapewa vyeo (platform za kufahamika), yale yale ya mwakyembe na sitta wamepiga kelele we ili wawe mawaziri..watanzania mind set is more of a problem than matembezi...
 
Mkuu,

Wazo lako ni zuri, zuri sana!

Nani ata-coordinate maandamano hayo?

Nategemea jawabu ya,” wote wanaochukia ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi”

Ugumu wa kulitekeleza wazo lako.(Kama nilivyosema ni wazo zuri,mimi naliunga mkono)
Katika Tanzania ya leo, nakusudia nchi ambayo wananchi wake wengi hawana elimu ya uraia(civic education) na hakuna juhudi za makusudi zinazofanywa ili kurekebisha udhaifu huu.kuwafanya watu watambue haki zao na wajibu wao kwa taifa.

Kwenye nchi ambayo muamko wa wananchi juu ya haki zao katika taifa ni mdogo sana.
Kwenye nchi ambayo kila mmoja wetu anasubiri mwenzake afanye, aanzishe jambo la kuwanufaisha wananchi wote.

Kwenye nchi ambayo serikali iliyopo madarakani kwa miongo zaidi ya minne inachukulia udhaifu huo nilioutaja hapo juu kama mtaji wa kukinufaisha kikundi kidogo cha jamii kumiliki, kuharibu, kujitwalia kila kitu,kurubuni mlalahoi wakati wa kura, vyombo pekee ambavyo tungetegemea vingefanikisha wazo lako ni Asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, jumuia za wananchi, na vyama vya siasa.

Hapa sitaji,vyama vya wasomi na wanasheria kwani hivi kazi yao nikuitisha makongamano, warsha waalikwa ni wavaa tai na suti, si mlalahoi, kuandika magazetini, au kusubiri kuhojiwa watoe mawazo yao halafu wanakwenda zao bar kupata bia na kiti moto au soda na chipskuku, siku inakuwa imepita!

Asasi nyingi zinaanzishwa sio kwa lengo la kumnufaisha mwananchi. Mwananchi mlalahoi hutumiwa tu kama kisingizio cha kuombea fedha kutoka kwa mfadhili,wafadhili ili watu wamege donge nono,watunishe mifuko yao na fedha kidogo humfikia mlengwa na huwa geresha tu.

Sina nia ya kusema kuwa ni asasi zote ila majority ziko hivyo. Kwa hiyo asasi hizi hazitajibebesha jukumu hili la kuandaa maandamano ya amani kwa nchi nzima. Hali kadhalika jumuiya za wananchi na vyama vya wafanyakazi havina ubavu huo, ziko weak sana.

Kimbilio pekee ni vyama vya siasa vya upinzani. Vyama hivi vikiamua,vikiweka manung’uniko ya wananchi na maslahi ya taifa mbele vinaweza kuthubutu kuitisha maandamano kwa nchi nzima. Ni bahati mbaya kuwa havijitambui kuwa maslahi ya taifa ni superior kuliko kujitangaza kichama. Kukosekana kwa ujasiri na utashi kwa vyama hivi kuwa na sauti ya pamoja katika kuiwajibisha serikali inayokumbatia uoza,ufisadi,ubadhirifu wa mali ya umma ni ufinyu wa mawazo wa viongozi wa vyama hivyo.

Tusitegemee CCM kuitisha maandamano ya nchi nzima kuitaka serikali iwajibike kwa wananchi.

Lakini hili la vyama vya upinzani kushindwa kufanya hili ni uwendawazimu. Kama lugha hii ni kali basi niseme viongozi wa vyama vya upinzani wana muono finyu kama vyama vya siasa.

Wao wanapokuja kuomba kura hutuambia tuwachague ili wakatutumikie, wakatuwekee mambo sawa, ok, siku ya kushika hatamu haijafika lakini wanataka tuamini kuwa hata ku-coordinate na ku-organise maandamano ya wananchi kwa nchi nzima kunawashinda ?

Ubinafsi wa kila chama kuwa kinataka kionekane kuwa ndio chama dume,chama kikuu cha upinzani kisiwe kikwazo cha kushirikiana katika mambo, au jambo linalowaunganisha wananchi wote.

Mkuu, mchango wangu katika kuunga mkono wazo lako, ni kuwaomba wanaJF ambao wanaweza kupata sikio la hawa viongozi wa vyama vya upinzani wawapitishie ujumbe huu. Halafu baada ya miezi mitatu tuone kama watapata utashi na ujasiri wa kuja pamoja kama nguvu moja itakayowakilishia vilio vya wanyonge.

Kama wao watashindwa, kwa mazingira ya Tanzani yalivyo hii leo, basi kuitisha maandamano ya nchi nzima itabaki kuwa ni ndoto. Hatuko tayari, bado jamii inapiga mbonji ! na kukoroma.

Mkuu Nonda
umeelezea mengi muhimu..
Labda nikuulize swali:
unavyosema vyama vya upinzani vibebe hili jukumu unamaanisha nini hasa?
I mean, unazungumzia vyama vipi hasa?
 
1. Shomari, nani kakudanganya huo msemo kwenye nyekundu ni wa Kikwete??

2. Swali lako....."nani aanzishe" = very simple, tuanze kujiorodhesha hapa hapa:
- M-mbabe
- Spencer
- Iwanga
- Ezan
- Stein
- Byendangwero
- King of Kings
- Bruce Lee
- Wewe mwenyewe (Shomari)
- El Nino (huyu tutambeba juu juu kibabe maana anataka kuleta logic nyingi)

gsana ujamtaja,hatokosa kuandamana na bango kubwa,"WACHUUZI WAGENI WARUDI MAKWAO!"
 
Back
Top Bottom