Maandamano ya Amani Nchi Nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya Amani Nchi Nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Dec 22, 2010.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  GrEaTthinkers,

  Think kiasi gani tumepoteza kama taifa,
  Kwa nini jasho letu linatumika vibaya hivi!
  • TICTS
  • RADAR
  • NDEGE YA RAIS
  • SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
  • TWIN TOWERS BOT
  • MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Madini)
  • KAGODA(EPA)
  • MEREMETA
  • RICHMOND/DOWANS
  • WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
  • IPTL
  • KIWIRA COAL MINES
  • NETGROUP SOLUTIONS
  • MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
  • ALEX STEWART
  • BEI YA BIDHAA ie. UMEME (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
  • RITES
  • ALLIANCE AIR
  • KUJENGA BARABARA KUPITIA MBUGA YA SERENGETI(Matumizi mabaya ya kodi zetu)
  • LOLIONDO
  • BARABARA YA KILWA NA MANDELA KAZI KURUDIWA(Matumizi mabaya ya kodi zetu
  Nasema hawa si wa kuchekea wanaiumiza Nchi,

  Kwa Asili ni sisi ni matajiri, tunafilisiwa na wapuuuzi

  Haiwezekani madudu yote hayo, hakuna hata mwenye hatia ukitoa Liyumba.

  Ukinunua soda ya 500Tsh umetoa 90Tsh. kama kodi.

  Amkeni, Toeni sauti, Nchi inakwisha.:target:
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  At last.

  Sasa wewe ndio unaongea vile wanaume (not being disrespectful to our mamas pls) inatakiwa waongee!!
   
 3. l

  lwangwa Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono tuandamane kupinga kwanini watanzania tunakuwa mabwege nasema nikotayari kuandamana hata kufa
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni nani atakayeanzisha ndugu yangu ila kimsimsingi binafsi nimechoka na madudu ya nchi hii.
   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nani aanzishe?!!! Kikwete ana msemo unaokwenda kwa jina la ''It is possible, Take your part!''
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kabla ya maandamano napendekeza kutengenezwe kajarida kanakotoa mutahsari wa madudu yote hayo na kasambazwe nchi nzima hasa huko vijijini
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Si woga ila kwa sheria zetu hizi na utawala huu mwanzilisha wa jambo hili hatakuwa salama yatamkuta makubwa - anaweza kupotezwa hata kabla ya tarehe ya maandamano kuijafika.
   
 8. l

  lwangwa Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkakati ni huu tuma ujumbe wa simu kwa watu unao wafahamu kama walivyofanya msumbiji kwa njia ya simu hili tunaliweza kuingia mitaani hatuna sababu yakuchelea andika hivi wote maandamano ya amani ya kudai vyote vilivyoorodheshwa hapo siku ya jumanne nchi nzima
   
 9. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  We Elnino, Unafahamau maana maana ya maandamano ya Amani??

  Mbona unakuwa muoga bila kutishwa,

  Taratibu zote za kisheria zitafuatwa ikiwemo kupata kibali.
   
 10. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  El nino! the only thing to fear is fear! yap! it's good move na hicho kijarida, asilimia kubwa ya wananchi vijijini, hasa watu wazima hawajui kusoma, na asili ya mtanzania hapendi kujisumbua kusoma. good Idea lakini think about the content, all in all what we need is only the motivation, read the lines.
   
 11. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwani sasa wanapotezwa wangapi. Ule muda wa kuogopa umeshakwisha ishue ni kwamba wakimpoteza mtu nasi tunawapoteza watu wao kimya kimya. Hakuna kuogopa tushatishwa sana na kama kunyanyaswa tushanyanyaswa sana na tatizo ni kwamba makali ya manyanyaso hayapungui yanaongezeka sisi tutafanya nini?
   
 12. l

  limited JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  sawa tutafuata sheria lakini mpaka hicho kibali cha kuandamana kitoke i will be dead .,,,,,,,,,,,,,,,,,,system haiko sawa ndio maana ina takiwa katiba mpya watu watoe dukuku zao kwa haki na usalama
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  NAUNGA MKONO hoja lakini mpaka upate kibali patachibika

  lakini issue kama hizi haziitaji kibali
   
 14. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  pamoja sana,naunga mkono, na hata sisi ambao hatupo tz tutumiane emails na kuwajulisha wote waliopo huko kufanya hivyo,pia mi nipo tayari hata kutoa pesa kufanikisha hilo, rafiki yangu msomali ambae colonel mstafu wa jeshi amenishauri kua sometimes inabidi kujitoa ili dunia ijue ukweli na uoga wa kifo ni upumbavu wa hali ya juu,kwani kila aliezaliwa nilazima atakufa,sasa kwanini tusiamue kufa kiume?mapambano yanaendelea kwani hatuna uhuru wa kumiliki rasilimali zetu zimezo taifishwa na mafisadi. Tusiogope kufa kwa kudai haki zetu.
   
 15. t

  tbetram Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi wa serikali wote na mashirika ya umma wanalipa p.a.y.e.
  Maduka yote yanalipa kodi.
  Ukienda super market angalia risiti uone kodi unayolipia kila bidhaa unayonunua.
  Maduka yetu ya uswahilini hayatoi risiti. Ila ukweli ni kwamba kila bidhaa unayonunua dukani unalipia kodi.
  Katika bandari za Tanga, DSM na Mtwara magari, makontainer yote yayoingia yawe ya Tanzania au nchi za jirani kama Zambia, Rwanda na Burundi yote yanalipia kodi kubwa.
  Magari yote yanayotembea barabarani yanalipiwa kodi.
  Achilia mbali fedha zinazotolewa na wahisani.

  Fedha zote hizi zinazo kusanywa zinatumika kugharimia maisha ya kifahari ya viongozi waliowekwa madarakani na sisiemu na wale waliostaafu.

  Sisi walipa kodi tunabaki tukigharimia wenyewe matibabu, usafiri, elimu n.k

  Ushauri wangu, ufanyike mpango wa kusitisha ulipaji wa kodi mpaka hapo serikali itakapotoa realistic justification ya mapato na matumizi ya fedha za serikali na pia serikali ionyeshe namna walipa kodi wanavyonufaika na fedha za serikali kuanzia mijini mpaka vijijini
   
 16. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili ni wazo zuri sana, linatakiwa lifanyiwe kazi, tunahitaji kuuonyesha ulimwengu madhaifu ya ccm na makada wake, nini wanafanya kuifilisi nchi hii iliyojaliwa asali na maziwa.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Wazo lako ni zuri, zuri sana!

  Nani ata-coordinate maandamano hayo?

  Nategemea jawabu ya," wote wanaochukia ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi"

  Ugumu wa kulitekeleza wazo lako.(Kama nilivyosema ni wazo zuri,mimi naliunga mkono)
  Katika Tanzania ya leo, nakusudia nchi ambayo wananchi wake wengi hawana elimu ya uraia(civic education) na hakuna juhudi za makusudi zinazofanywa ili kurekebisha udhaifu huu.kuwafanya watu watambue haki zao na wajibu wao kwa taifa.

  Kwenye nchi ambayo muamko wa wananchi juu ya haki zao katika taifa ni mdogo sana.
  Kwenye nchi ambayo kila mmoja wetu anasubiri mwenzake afanye, aanzishe jambo la kuwanufaisha wananchi wote.

  Kwenye nchi ambayo serikali iliyopo madarakani kwa miongo zaidi ya minne inachukulia udhaifu huo nilioutaja hapo juu kama mtaji wa kukinufaisha kikundi kidogo cha jamii kumiliki, kuharibu, kujitwalia kila kitu,kurubuni mlalahoi wakati wa kura, vyombo pekee ambavyo tungetegemea vingefanikisha wazo lako ni Asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, jumuia za wananchi, na vyama vya siasa.

  Hapa sitaji,vyama vya wasomi na wanasheria kwani hivi kazi yao nikuitisha makongamano, warsha waalikwa ni wavaa tai na suti, si mlalahoi, kuandika magazetini, au kusubiri kuhojiwa watoe mawazo yao halafu wanakwenda zao bar kupata bia na kiti moto au soda na chipskuku, siku inakuwa imepita!

  Asasi nyingi zinaanzishwa sio kwa lengo la kumnufaisha mwananchi. Mwananchi mlalahoi hutumiwa tu kama kisingizio cha kuombea fedha kutoka kwa mfadhili,wafadhili ili watu wamege donge nono,watunishe mifuko yao na fedha kidogo humfikia mlengwa na huwa geresha tu.

  Sina nia ya kusema kuwa ni asasi zote ila majority ziko hivyo. Kwa hiyo asasi hizi hazitajibebesha jukumu hili la kuandaa maandamano ya amani kwa nchi nzima. Hali kadhalika jumuiya za wananchi na vyama vya wafanyakazi havina ubavu huo, ziko weak sana.

  Kimbilio pekee ni vyama vya siasa vya upinzani. Vyama hivi vikiamua,vikiweka manung'uniko ya wananchi na maslahi ya taifa mbele vinaweza kuthubutu kuitisha maandamano kwa nchi nzima. Ni bahati mbaya kuwa havijitambui kuwa maslahi ya taifa ni superior kuliko kujitangaza kichama.

  Kukosekana kwa ujasiri na utashi kwa vyama hivi kuwa na sauti ya pamoja katika kuiwajibisha serikali inayokumbatia uoza,ufisadi,ubadhirifu wa mali ya umma ni ufinyu wa mawazo wa viongozi wa vyama hivyo.


  Tusitegemee CCM kuitisha maandamano ya nchi nzima kuitaka serikali iwajibike kwa wananchi.

  Lakini hili la vyama vya upinzani kushindwa kufanya hili ni uwendawazimu. Kama lugha hii ni kali basi niseme viongozi wa vyama vya upinzani wana muono finyu kama vyama vya siasa.

  Wao wanapokuja kuomba kura hutuambia tuwachague ili wakatutumikie, wakatuwekee mambo sawa, ok, siku ya kushika hatamu haijafika lakini wanataka tuamini kuwa hata ku-coordinate na ku-organise maandamano ya wananchi kwa nchi nzima kunawashinda ?

  Ubinafsi wa kila chama kuwa kinataka kionekane kuwa ndio chama dume,chama kikuu cha upinzani kisiwe kikwazo cha kushirikiana katika mambo, au jambo linalowaunganisha wananchi wote.

  Mkuu, mchango wangu katika kuunga mkono wazo lako, ni kuwaomba wanaJF ambao wanaweza kupata sikio la hawa viongozi wa vyama vya upinzani wawapitishie ujumbe huu. Halafu baada ya miezi mitatu tuone kama watapata utashi na ujasiri wa kuja pamoja kama nguvu moja itakayowakilishia vilio vya wanyonge.

  Kama wao watashindwa, kwa mazingira ya Tanzani yalivyo hii leo, basi kuitisha maandamano ya nchi nzima itabaki kuwa ni ndoto. Hatuko tayari, bado jamii inapiga mbonji ! na kukoroma.
   
 18. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  1. Shomari, nani kakudanganya huo msemo kwenye nyekundu ni wa Kikwete??

  2. Swali lako....."nani aanzishe" = very simple, tuanze kujiorodhesha hapa hapa:
  - M-mbabe
  - Spencer
  - Iwanga
  - Ezan
  - Stein
  - Byendangwero
  - King of Kings
  - Bruce Lee
  - Wewe mwenyewe (Shomari)
  - El Nino (huyu tutambeba juu juu kibabe maana anataka kuleta logic nyingi)
   
 19. m

  mams JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sijui itumike njia gani kuwaelimisha walioko vijijini kuhusu haya unayoyasema. Wangi hawajui hayo, na hao ndiyo waliokipatia ushindi chama tawala kikangia madarakani. Haohao ndiyo wenye shida x 100 kuliko wewe uliye mjini.


  Maandamano yatakayo kuwa na manufaa ni yale yatakayowahusisha hao wengi lakini kuhusika kwao ni mpaka waelimike juu ya hujuma hizo. Ni lini? Labda mimi na wewe katutakuwepo wakati huo nikimaanisha ni vizazi vijavyo ambavyo havitapozwa kwa Tshirts, kofia, pilau au buku tano
   
 20. Ngoreme

  Ngoreme Senior Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nasema tuamue tusiende kazini siku moja kwa kila mmoja awe mkulima hadi mfugaji lakini hii hamasa tukiiweka kwenye ballot box si tosha kabisa
   
Loading...