ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Jukwaa la Katiba latangaza uamuzi mgumu
Jijini Dar es Salaam, Jukwaa la Katiba limetangaza maandamano makubwa yasiyokoma nchi nzima, kama hatua ya kupinga hatua hiyo ya serikali baada ya jitihada zao za kuishauri serikali kwa njia za mazungumzo kushindikana.
Akizungumza mara tu baada ya uamuzi wa serikali kuruhusu muswada huo kusomwa kwa mara ya pili huko Dodoma, mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba, alisema kwa kuwa wabunge wa CCM wameamua kuwadharau Watanzania na kupuuzia mawazo yao, sasa taifa litashuhudia maandamano ambayo hayajapata kuwapo nchini.
Sasa tutawaonyesha watawala wetu ya kuwa sisi Watanzania ndio wenye nchi. Tutaagiza maandamano kutoka kila kona ya nchi kuelekea Dar es Salaam, na tutakusanyika katika uwanja mkubwa ambapo tutakaa kwa siku zote hadi serikali itakapoamua kuondoa muswada huo bungeni, alisema Kibamba.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni masikitiko makubwa na mshangao kwa wapenda amani kuona jinsi serikali na wabunge wa CCM wanavyoweza kuwadharau wananchi wake katika mambo mazito ya taifa.
Mapema juzi, jukwaa hilo liliitahadharisha serikali kuwa isiposikia kilio cha Watanzania, wataamua kuandamana nchi nzima bila kukoma na wakalitahadharisha jeshi la polisi na majeshi mengine, kukaa pembeni kwa sababu Watanzania wanalilia haki yao ambayo haiwezi kuzuiwa kwa wingi wa askari, silaha na mabomu
Source: Gazeti la Mwananchi
naamini hata askari watunga mkono, watakuwa wakimaliza malindo yao kama wajibu wao unavyowataka, watakuwa wanajumika pamoja