Maandamano makubwa leo Arusha

Maandamano makubwa leo Arusha

Filipo

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
9,347
Reaction score
5,555
Jiji la Arusha litapata mtikisiko wa maandamano asubuhi hii yatakayoanzia Majengo, kuzunguka viunga mbalimbali vya jiji, hatimae kuishia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta. Maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa waongoza watalii, Tato, na yataongozwa na Waziri Nyalandu. Lengo lake ni kupinga mauaji ya Tembo nchini.

Itakumbukwa kwamba mauaji ya tembo yamekuwa ni janga hapa nchini tangu uongozi mpya wa Chama cha mapinduzi uingie madarakani na licha ya watuhumiwa mbalimbali kutajwa, akiwemo Katibu mkuu wa chama hicho, bado takwimu zinaonesha Tembo mmoja anauawa kila siku nchini na itakapofika mwaka 2025 Tembo watakuwa historia hapa nchini.

Nawasihi wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano haya na kulaani kwa nguvu zote mauaji ya Tembo wetu!
 
Siwezi kushiriki huo upuuzi nyalandu andamana mwenyewe na aunt ezekiel na faraja kota na wanao maana ndo mnafaidika na hap tembo pia kumbukeni kuandamana kuelekea kwa kinana......
 
Kwatarifa nilizo zipata ni kuwa kwa takribani miezi mitatu sasa hakuna taarifa ya tembo kuuwawa wachunguzi wa mambo wanatabanisha kuwa ni kutokana na katibu mkuu wa
ccm Kinana kuwa busy na shughuli za kiasa akijitutumua kuokoa chama chake
kinachozidi kukataliwa na watanzania kwa nguvu
kila kukichana...hii imekuwa ahueni kwa taifa kwani wanyama hao sasa pengine wako salama kuliko kipindi chochote, wachunguzi wa mambo wameenda mbali zaidi kwa kuwashukru watu wa wili pengine wakawa wamechangia 1. Ni mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumpa ukatibu mkuu hali iliyopelekea sasa kuwa busy na mambo ya siasa na kupumzika mambo ya ujangili na mtu wa pili ni Mch. Peter Msigwa kwa kumwambia ukweli kuwa yeye ni jangili na ndiyo anae maliza tembo wetu nchini...
Ni watanzania tumpongeze kamanda Peter Msigwa na Kikwete kwa kazi waliyofanya...
KINANA WEKA MBALI NA TEMBO
 
Watu wa Arusha kwa ujasiri wenu ambao maCCM yanaujua, naombeni msaidieni Nyalandu kazi ambayo tunajua haiwezi. Maana hajafikia kiwango cha kujitoa kwa dhati...

Kazi yenyewe ni NAME n SHAME.

Majangiri wakubwa wanajulikana. Vigogo wa Serikali ya CCM na mawakala wao au maswahiba wa biashara hiyo.

Chukueni hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni mwaka 2012 na 2013, vigogo wa CCM walitajwa Kwa majina. Wakiongozwa na weka mbali na tembo.

Name n shame them...
 
Jiji la Arusha litapata mtikisiko wa maandamano asubuhi hii yatakayoanzia Majengo, kuzunguka viunga mbalimbali vya jiji, hatimae kuishia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta. Maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa waongoza watalii, Tato, na yataongozwa na Waziri Nyalandu. Lengo lake ni kupinga mauaji ya Tembo nchini.

Itakumbukwa kwamba mauaji ya tembo yamekuwa ni janga hapa nchini tangu uongozi mpya wa Chama cha mapinduzi uingie madarakani na licha ya watuhumiwa mbalimbali kutajwa, akiwemo Katibu mkuu wa chama hicho, bado takwimu zinaonesha Tembo mmoja anauawa kila siku nchini na itakapofika mwaka 2025 Tembo watakuwa historia hapa nchini.

Nawasihi wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano haya na kulaani kwa nguvu zote mauaji ya Tembo wetu!

Msiache Mabango ya kulaani katiba ya CCM, kulaana CCM na katibu mkuu Kinana kwa mauji ya tembo, jitokezeni kwa wingi na mpenyeze ajenda za wananchi kupitia mabango.
 
Watu wa Arusha kwa ujasiri wenu ambao maCCM yanaujua, naombeni msaidieni Nyalandu kazi ambayo tunajua haiwezi. Maana hajafikia kiwango cha kujitoa kwa dhati...

Kazi yenyewe ni NAME n SHAME.

Majangiri wakubwa wanajulikana. Vigogo wa Serikali ya CCM na mawakala wao au maswahiba wa biashara hiyo.

Chukueni hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni mwaka 2012 na 2013, vigogo wa CCM walitajwa Kwa majina. Wakiongozwa na weka mbali na tembo.

Name n shame them...

Ndo maana magazeti ya England yaliwaambia serikali imekumbatia wezi wa meno ya tembo. Yale majina 40 mheshimiwa zaidi aliyasema kule ughaibuni yako wapi!
 
Hivi hawa wauwaji wa tembo si walitajwa nawaziri kivuli wa upinzani Bungeni? Imefikia wapi
 
Tanzania ya Leo kwa kweli Mi natazama kivingine kabisa kwani maharamia,,wahujumu uchumi wanaendelea kukumbatiwa mpaka lini.........!

Ni Imani ya kwamba hata huko walipo watawala WA Nchi hii waliotutangulia wanajua kabisa huku wamewaacha mafisadi full na tunaweza kumbuka kauli ya Marehemu Julias Kambarage Nyerere akisema ya kwmb Watanzania wanahitaji mabadiliko ndani ccm nawasipoipata ndani ya utawala huo wataitafuta kwingine.......mimi naona kabisa ya kwamba muda umefika wa mageuzi ya kweli!

Watu ingependeza tusirudi nyuma hata kidogo ni kukomaa tu mpaka kieleweke kudadekiii!

Filipo uko anga zipi muda huu??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom