Maandamano makubwa leo Arusha

Maandamano makubwa leo Arusha

Katibu mkuu wa chama chake nyalandu ndo mhusika wa mauaji ya tembo,anazuga kuandamana
 
Jiji la Arusha litapata mtikisiko wa maandamano asubuhi hii yatakayoanzia Majengo, kuzunguka viunga mbalimbali vya jiji, hatimae kuishia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta. Maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa waongoza watalii, Tato, na yataongozwa na Waziri Nyalandu. Lengo lake ni kupinga mauaji ya Tembo nchini.

Itakumbukwa kwamba mauaji ya tembo yamekuwa ni janga hapa nchini tangu uongozi mpya wa Chama cha mapinduzi uingie madarakani na licha ya watuhumiwa mbalimbali kutajwa, akiwemo Katibu mkuu wa chama hicho, bado takwimu zinaonesha Tembo mmoja anauawa kila siku nchini na itakapofika mwaka 2025 Tembo watakuwa historia hapa nchini.

Nawasihi wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano haya na kulaani kwa nguvu zote mauaji ya Tembo wetu!
endeleeni tu na nyimbo wakati comrade kinana anachanja mbuga nchi nzima bila kuchoka kuhamasisha maendeleo na utawala bora.
 
Jiji la Arusha litapata mtikisiko wa maandamano asubuhi hii yatakayoanzia Majengo, kuzunguka viunga mbalimbali vya jiji, hatimae kuishia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta. Maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa waongoza watalii, Tato, na yataongozwa na Waziri Nyalandu. Lengo lake ni kupinga mauaji ya Tembo nchini.

Itakumbukwa kwamba mauaji ya tembo yamekuwa ni janga hapa nchini tangu uongozi mpya wa Chama cha mapinduzi uingie madarakani na licha ya watuhumiwa mbalimbali kutajwa, akiwemo Katibu mkuu wa chama hicho, bado takwimu zinaonesha Tembo mmoja anauawa kila siku nchini na itakapofika mwaka 2025 Tembo watakuwa historia hapa nchini.

Nawasihi wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano haya na kulaani kwa nguvu zote mauaji ya Tembo wetu!

MKUU FILIPO haya maandamano yalenga nini na kumlenga nani?.Si majangili walisha fahamika tayari? na Bunduki za kisasa kununuliwa ilikuyadhibiti pamoja na msaada wa helkopta. Tunachokitaka kwasasa ni kuona na kusikia majangili mangapi yamekamatwa na hatua gani zimechukuliwa dhidi yao. Kwanini kupoteza muda wa wananchi kwenye maandamano wakati majangili yana julikana kwa majina na mahali wana poishi na hata idadi yao kwamba ni arobaini. Na inakuwaje Waziri ambaye anazembea kwa kutochukua hatua stahiki na anayetakiwa kuwajibika kwa Uzembe wa Wizara yake ndiye akaongoze Maandamano husika ina maana hayo maandamano yana mtaka nani hasa kuwajibika. Hii tabia ya kufanya maigizo na usanii sanii katika masuala ya msingi yanayohusu nchi ni ya kukemewa na waungwana wote.Maandamano haya ni moja ya Vioja na Viroja katika Nchi hii.

Hawa majangili ni wahalifu kama wahalifu wengine ,nchii hii sijui nani katuloga nina wasiwasi na Polisi nao sasa wataandaa maandamano ya kupinga kuongezeka vitendo vya uhalifu...kwasababu ndiyo njia pekee na rahisi ya kukwepa wajibu na kuwajibika.

Orodha aliyosema anayo Mkuu wa nchi ishughulikiwe kwanza .Wahusika wote wakamatwe na wautaje mtandao wao.Sheria ichukue Mkondo wake na baada ya Hukumu kutolewa na Majangili yote kuswekwa korokoroni ndipo tuandamane kupongeza na kusherehekea ushindi mkuu katika kunusuru maliasili zetu.MAANDAMANO YA AINA YA HAYO WANAYO TAKA KUYAFANYA ARUSHA NI MAANDAMANO YENYE ASILI YA UVIVU,UWOGA,UNAFIKI NA DAIMA YANAKUWA YA WAPIGA DILI NA USISHANGAE MDHAMINI MKUU AKAWA MMOJA WA MAJANGILI MASHUHURI.
 
Utajikuta uko jela kisongo

KWA NINI MNAPENDA KUFANYA MAMBO YA LAANA SANA MNAUWA TEMBO BILA HURUMA MNAPATA PESA MNAAZINSHA MAKUNDI YA LAKI SI PESA KANGA MOKO MNAZIDI KUJIONGEZEA MADHAMBI NA LAANA 😡
 
Kinana msomali tembo wetu una mpango Wa kuwamaliza lini kwasbbu wamebaki 200
 
Ni ujinga kuweka mtandaoni picha ya familia ya watu!!!!ni haki mh kumpiga wife wake kiss!Mod ondoeni hiyo picha coz ni privacy ya mtu!!
 
Yaani mtu akimpiga busu mke wake inakuuma sana - na hapo nyuma hiyo ni familia yake - Ulitaka uolewe wewe nini!

Mwenyekiti hana maadili kabisa. Huyo ni mke wake yupi jois au kuna mwingine?
 
Back
Top Bottom