Maandamano makubwa kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano makubwa kesho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by STALLEY, Sep 10, 2012.

 1. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nimesikikia tetesi kuwa kesho kutakuwa na maandamano makubwa ya amani nchi zima ya waandishi wa habari kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao aliyeuawa huko iringa.NI WAKATI WA WAANDISHI WA HABARI KUUNGANA KUPINGA UKATILI HUU ULIOFANYA NA JESHI LA POLISI. \ /
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Taarifa za kiitelijesia zinaonesha kesho kuna mashambulizi ya bokoharam,hivyo maandamano yamezuiliwa
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  waangalie asije akauawa mwandishi mwingine
   
 4. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sio tetesi karibu magezeti yote ya kiswahili yameandika. Nunua ukasome
   
 5. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii sio tetesi jamani vp? Basi useme umepata wapi hizi tetesi maana karibu watz wote wanajua kuwa kutakuwa na maandamano....kwani lazima uanzishe sredi?
   
 6. commited

  commited JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  MWANANCHI.Waandishi kuandamana kimyakimya nchi nzima[TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 10 September 2012 10:34[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  NI KESHO ASUBUHI, LENGO NI KULAANI MAUAJI YA DAUD MWANGOSI, KUTOA MATAMKO
  Frederick Katulanda
  WAANDISHI wa habari nchini kesho wataandamana nchi nzima kwa amani kulaani kuuawa kwa mwandishi mwenzao, Daud Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Iringa.

  Maandamano hayo ambayo yatakuwa ya kimyakimya yatafanyika katika mikoa yote nchini kuanzia saa 2:00 asubuhi na waandishi watakaoshiriki katika maandamano hayo watavaa ama nguo nyeusi au watafunga vitambaa vyeusi mkononi ikiwa ni ishara ya kuomboleza na kulaani kuuawa kwa mwenzao.
  Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), Theophil Makunga alisema kuwa uamuzi wa kufanyika kwa maandamano hayo ulifikiwa katika kikao cha jukwaa hilo kilichofanyika Dar es Salaam juzi.
  Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, maandamano hayo yamepangwa kuanzia katika Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Mtaa wa Jamhuri ambacho Mwangosi alikuwa akikitumikia na kupita katika Mtaa wa Azikiwe, Barabara ya Bibi Titi hadi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambako maandamano hayo yatahitimishwa.
  Alisema baada ya kufika katika viwanja hivyo, yatapokewa na viongozi wa TEF na kisha baadhi ya waandishi waliokuwapo katika eneo la tukio watatoa ushuhuda wa kilichotokea na kufuatiwa na mjadala kuhusiana na mauaji hayo na kutoa tamko la pamoja.
  "Kutatolewa ushuhuda kutoka kwa waandishi wa habari ambao walishuhudia tukio la kuuawa kwa mwandishi mwenzao, wataeleza kwa kina hali halisi na ukweli waliouona siku ya tukio," alisema Makunga.
  Alisema tayari wamekwishawasiliana na Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ambako wamepeleka barua ya kuomba ulinzi kesho wakieleza njia watakazopitia siku hiyo.
  "Tunafanya matembezi ya amani, kimyakimya kwa lengo la kulaani tukio la kusikitisha la kuuawa kwa Mwangosi. Ni mwandishi wa kwanza hapa nchini kuuawa akiwa kazini na doa kubwa kwa nchi yetu na vyombo vya dola, hivyo lazima tulilaani tukio hilo."
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema, hajapokea barua hiyo na kusema kwamba inawezekana ipo kwa wasaidizi wake na hivyo kuahidi kuifanyia kazi.
  "Sijaiona barua yao, inawezekana ipo kwa maofisa wangu au wameipeleka kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, nitafuatilia kujua ili kuona jeshi langu litafanya nini," alisema.
  Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji alisema kwamba lengo la maandamano hayo ni kulaani mauaji ya Mwangosi na zaidi ni kufikisha ujumbe kwa Serikali.
  "Hatukupendezwa na mauaji hayo, yametuumiza na hatutopenda yatokee tena, tunayalaani na kuomba hatua kali zichukuliwe," alisema Mihanji.

  Maandamano mikoani
  Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema, sambamba na maandamano hayo Dar es Salaam, pia waandishi wengine mikoani nao wataandamana kuungana na wenzao kulaani mauaji hayo ya mwenzao.

  Maandamano ya mikoa yote nchini yatasimamiwa na klabu zote za waandishi wa mikoa husika na kwamba maandalizi yake ni pamoja na kubainisha njia watakazopitia kwa upande wa mikoani, yamekwisha kamilishwa. Alisema maandamano hayo yatapokewa na wenyeviti wa klabu ambao watatoa matamko mbalimbali kuhusiana na kifo cha Mwangosi.
  "Kila mkoa hapa nchini utashiriki maandamano, wataandamana kwa amani kuungana na wenzao kulaani kifo cha mwandishi mwenzao, nao kama ilivyo kwa Dar es Salaam watavaa nguo nyeusi au vitambaa vyeusi mkononi," alisema.
  Alisisitiza kwamba kama itakavyokuwa kwa yale ya Dar es Salaam, maandamano hayo hayatahusisha kiongozi yeyote wa Serikali, chama cha siasa au wanaharakati, bali waandishi wa habari wenyewe viongozi wao.
  Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yamekamilika. Alisema yataanzia katika Viwanja vya Ghand Hall, kupitia Barabara za Uhuru, Mlango Mmoja, Nyerere na kuingia katika Barabara ya Miti Mirefu, Pamba, Barabara ya Kenyatta hadi Uwanja wa Nyamagana.
  Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali alisema, ofisi yake ilikuwa katika maandalizi ya kufanikisha maandamano hayo akisema kwamba hadi leo jioni watakuwa katika nafasi nzuri ya kutangaza njia watakazopitia na mahali yatakapoishia.
  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Christopher Nyenyembe alisema kwamba pia wako katika maandalizi ya kukamilisha maandamano hayo.
  "Tunazo sababu za kuandamana kuungana na wenzetu nchi nzima, tulikwisha toa tamko letu kulaani mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kususia kuandika habari za polisi, lakini katika maandamano hayo tutatoa tena tamko," alisema.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Je waandishi wa habari wa Radio imaan na gazeti la al-nuur na Al-huda watashiriki kwenye maandamano?

  Msaada wakuu.
   
 8. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  waandishi wa clouds tv na redio watakuwepo?!!!
   
 9. commited

  commited JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu Shardcole hao ni ndugu na jk, na amri yoyote ya mauaji ya polisi au usalama wa taifa jk lazima ajue na atoe go ahed so hawatatokea katika maandamano na wanaweza anzisha kipindi cha kuwaponda hao waandishi watakaoandamana, lakini pia wanaweza mlaumu hata marehemu kuwa alikuwa akitumika na makafiri. chezea hao jamaa wanaolindwa na jk
   
 10. commited

  commited JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hao watoto wa LUGE?, best yake JK wazee watotozi hawana huo muda wa kuingia barabarani labda yangekuwa mashindano ya fiesta, au kupaka mapoda ungewaona
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi naunga mkono maandamano yenu,
  Hakikisheni waandishi wa magazeti yote hasa ya chama na ya makada wa Chama wanashiriki.
   
 12. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  umeona eheeeeeeeee sasa wa TBC je watakuwepo?!!!!!!!!! maana hata kuonesha habari hii walikuwa wanasuasua
   
Loading...