Maandamano makubwa Arusha tar 24/07/2011

Malboro

Member
Jun 24, 2011
23
11
Wana jf, leo nilikuwa nasikiliza RADIO FIVE ya Arusha wananchi wenyewe bila kiongozi wa chama chochote wameazimia kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa tarehe tajwa. Lengo la maandamano hayo ni kudai UMEME. Kwa mujibu wa wananchi walioohojiwa, maandamano hayo hayatahusisha chama chochote ili kuepuka kile kinachoitwa lawama kwa baadhi ya vyama hasa vya upinzani. Maandalizi yanafanyika kwa kutafuta kibali na hata kibali kisipopatikana wataandamana hata damu ikamwagika. Nafikiri ni kusubiri tuone.
 
Waandamane tu maana nasikia mgao wa Arusha ni kama wanawakomoa wana Arusha maana ni mkali mno wansema yaani ni kama hamna umeme kabisa pale Arusha mjini
 
Maandamano ni njia ya kufikisha ujumbe hasa kwa serikali ambayo siyo sikivu,thus naunga mkono kabisa na naahidi kuwepo siku hiyo!
 
Hali Kadhalika Mbeya mjini wazee, mgao ni mkali mno, ni kama hamna umeme kabisa.
Nadhani wanafanya makusudi kwa majimbo yaliyochukuliwa na Chadema.
 
Wana jf, leo nilikuwa nasikiliza RADIO FIVE ya Arusha wananchi wenyewe bila kiongozi wa chama chochote wameazimia kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa tarehe tajwa. Lengo la maandamano hayo ni kudai UMEME. Kwa mujibu wa wananchi walioohojiwa, maandamano hayo hayatahusisha chama chochote ili kuepuka kile kinachoitwa lawama kwa baadhi ya vyama hasa vya upinzani. Maandalizi yanafanyika kwa kutafuta kibali na hata kibali kisipopatikana wataandamana hata damu ikamwagika. Nafikiri ni kusubiri tuone.

Sio kwamba wananchi semeni CHADEMA a.k.a Magwanda ndio wanao andaa wananchi kuandamana na kumwaga damu
 
Leo naona tangu jana saa kumi na mbili mpaka sasa umeme upo au mvua imenyesha kule mtera...?
 
Kweli arusha hali ni mbaya, umeme wa TANESCO sijui unapatikana saa ngapi? wiki moja nimekaa nimebahatika kuona umeme siku moja tena saa nane usiku. Mchana ni majenereta tu yanaunguruma.
 
Arusha tutaandamana hata kama watapiga risasi za moto hatuogopi! Tumeshazoea kuuawa hovyo na polisi wa ccm
 
Ilitakiwa ifanyike nchi nzima.wamenikatia umeme then niisapoti serikali huu ni wehu kabisa.
 
Lazima tuandamane no way out. Mpaka kieleweke, hapa nasikia Ngeleja anaja miradi tu wakati hakuna umeme.
 
Nawashangaa wanazunguka wakati kila kitu kipo waz!!Chadema ni chama cha Vurugu
ndugu yangu wewe ni mtanzania tena m1 wa waathirika wa umeme. Huoni sababu ya kuuhitaji umeme? Usiangalie itikadi dai haki yako ya msingi? Maandamano ni njia ya pili baada kwnza ya mijadala na maswali kushindikana! Kwani wewe unajua faida ya hata huo umeme? Ucwe mpuuzi angalia ghali ya nchi yako na ondoa itikadi za chama
 
Sio kwamba wananchi semeni CHADEMA a.k.a Magwanda ndio wanao andaa wananchi kuandamana na kumwaga damu

Wewe ni mgonjwa wa akili, unashindwa kuona na kuelewa kuwa mgao unawahusu watanzania wote na wageni waioko? Inakuwa Chadema sasa? Chadema kinawezaje kuwahamasisha wananchi walitoa allegiance zao kwa wana Magamba? That line of thinking is pure mediocrity....sharpen your mind and think about mateso ya wananchi instead of kuhusisha kila kitu na chadema
 
Mgao wa umeme ni nchi nzima jamani hili ni janga linawashinda viongozi kulitatua watawezaje kuwasaidia? Umeme sio bidhaa inayopatikana dukani tuseme tukiandamana tutanunuliwa tupewe tutulie. Nashauri tuyageuze maandamano haya yawe ya kuing`o serikali legelege madarakani iliofanya uvundo huu wa miaka 50. Mm pia nipo arusha na nitaandamana hata nipigwe moto wengine wapone.
 
Wana jf, leo nilikuwa nasikiliza RADIO FIVE ya Arusha wananchi wenyewe bila kiongozi wa chama chochote wameazimia kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa tarehe tajwa. Lengo la maandamano hayo ni kudai UMEME. Kwa mujibu wa wananchi walioohojiwa, maandamano hayo hayatahusisha chama chochote ili kuepuka kile kinachoitwa lawama kwa baadhi ya vyama hasa vya upinzani. Maandalizi yanafanyika kwa kutafuta kibali na hata kibali kisipopatikana wataandamana hata damu ikamwagika. Nafikiri ni kusubiri tuone.

Maandamano hayo bado yataonekana ya kisiasa kwani Lema,Mbowe na viongozi wengine wa chadema wataingia kwa title ya wananchi.
 
Back
Top Bottom