Maandamano kupinga ripoti ya tume ya Uhamiaji

Maandamano kupinga ripoti ya tume ya Uhamiaji

CT SCan Mchina

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
1,311
Reaction score
289
Wakuu nimepokea simu mbalimbali usiku wa kuamkia leo vijana zaidi ya 50 wamekubaliana kuandamana mpaka ofisi za UHAMIAJI wakitaka kujua hatma yao.

Lengo la maandamano ni kuitaka TUME ieleze WANGAPI walipita KIHALALI...

Kama wewe si MZANDIKI tafadhali ungana nasi kwenye haya MAANDAMANO siku ya JUMATANO wiki Hii.
Huu UJUMBE tayari umesambazwa kwenye majina ya waliokuwa wameitwa kwenye AJIRA.
 
Maandamano Jumatano 27/8/2014... SMS mbalimbali zimeanza kutumwa kwa wahusika.
 
Mna hamu ya kupigwa nyie.
Chadema wameshindwa kuandamana nyie ndo muandamane,
Wanafunzi hawajapewa hela zao hawajaandamana wewe ndo uandamane.
Kama umekosa kazi umekosa tu
 
Hehehe, FFU hawajafanya kazi siku nyingi, na hivi watakuwa wanawashwa.... Kila la kheri
 
Haki ya mtu haipotei, Ila inacheleweshwa tu! Eee Mungu twakuomba uibariki nchi hii Tz.
 
Cha msingi mukutane mpange malalamiko yenu then muwe na mwakilishi kwa kuanzia musije mukavunjwa miguu bure kama mulipata kialali na next time mutapata ni kama enzi zile mwaka,98 mitihani ilifutwa kwa wote waliofaulu na waliofel but waliofaulu walifaulu tena unakua umecheleweshwa tu
 
USISEME HAIWEZEKANI WAKATI HUJAJARIBU...USISEME UMENYIMWA WAKATI HUJAOMBA..PENYE NIA PANA NJIA...napenda kutoa ushauri wangu kwa wadau wote mnaotaka kwenda kudai haki yenu..Ni kweli mna sababu zote za msingi kutokana na ripoti ya tume kuwa ya kutokuridhisha..mimi binafsi sikuwahi kuwaza kama majibu yanaweza kuwa hivyo..kama ni ishu ya upendeleo hoja ni je wote walipendelewa..mbona kamati imefanya general na sio specific conclusion..natoa mapendekezo yafuatayo..1.Msiandamane mana mna dai nafasi ya kuingia jeshi la uhamiaji hivyo tayari mtakuwa mmekiuka taratibu za kiuaksari na mtaonekana hajui sheria hivyo mnaweza kupoteza haki kwa njia unayoidai hiyo haki..2..Tafuteni mwanasheria(wakili awaandalie barua ya madai yenu iyakayoeleza kutokiridhika na ripoti ya tume..huyu atakuwa muakilishi wenu..3.tafuteni muandishi wa habari atakaye publish hii habari ili iwashtuw na wengine..na mwisho ni kwamba fanyeni hili jambo haraka iwezekanavyo kabla nafasi hazijatangazwa upya ili mpate considaration mapema...NB.HAKUNA ALIYEWAHI KUSHINDANA NA HAKI AKASHINDWA..YEYOTE ALIYEWADHULUMU WENGINE HAKI YAO ALISHINDWA..
 
Ukisema waliofaulu mwaka 1998 na mitihani kufutwa then wote walifaulu tena mwaka uliofata si kweli..kwanza mitihani ya NECTA huwa ni tofauti kila mwaka then unaweza kupita mwaka huu ila mwaka ujao ukipewa mtihani mwingine utashangaa matokeo..then mfano wa mtihani na Ajira ni tofauti kidogo..Ajira wakati mwingine ni bahati ya mtu..si kweli kila aliyeitwa kwenye usaili uliopita anaweza kuitwa tena hali kadhalika kupata kazi..hivyo kudai haki yako kwenye hili la uhamiaji ni sawa mana kwanza ni kweli ulifaulu na ulikuwa na haki kwani usipewe haki yako eti kisa kuna walioharibu mchakato..NI SAWA NA KUWAADHIBU WATOTO WAKO WOTE KWA KOSA LA MTOTO MMOJA..WAKUU NENDENI MKADAI HAKI YENU MKIKAA KIMYA HAKUNA ATAKAYEWASAIDIA
 
Tumieni njia ya kidiplomasia ni nzuri zaidi unapata ushindi mezani kwa hoja..unaweka hoja zako mezani mpaka kieleweke..napenda kuwaasa tena wadogo zangu msiandamane hata kama mna haki..tafuteni wakili akawateteebona hiyo ishu ipo wazi...diplomasia ni njia nzuri zaidi
 
....MAANDAMANO yanaendelea kuratibiwa mpaka kufikia KESHO kila kitu kitawekwa wazi... Wapo wanaotoka MIKOANI kuja kudaia HAKI zao...
 
...yaani TUME imefanya UDHALILISHAJI kwa kutoa maamuzi ya JUMLA hata kwa WALIOPITA kihalali... Tunataka HAKI yetu.
 
Maandamano Jumatano 27/8/2014... SMS mbalimbali zimeanza kutumwa kwa wahusika.

Badala ya kuandamana,nendeni Tume ya Usuluhishi mkafungue shauri la kusimamishwa kazi haswa kwa kuegemea kifungu cha 9(b) cha Sheria ya Kazi na Mahusiano kazini ya mwaka 2004
 
Badala ya kuandamana,nendeni Tume ya Usuluhishi mkafungue shauri la kusimamishwa kazi haswa kwa kuegemea kifungu cha 9(b) cha Sheria ya Kazi na Mahusiano kazini ya mwaka 2004

....TATIZO la hii NCHI yaani WASOMI wamefanywa kama MAZUZU wasiojua mambo.... Ngoja Tukusanyane Ndipo hao waliojifanya wametoa UAMUZI wa kutufuta WATAFANYAJE...
 
Back
Top Bottom