Maandamano dhidi ya Sofia Kawawa Zanzibar, 1988

Maandamano hayo hayakuwa na msingi wowote bali yalikuwa ni chanzo tu cha kuchochea hasira za kisiasa kupitia dini kwani ilitakiwa ijulikane wazi kwa waislamu wote kuwa maoni ya Sofia kwenye UWT hawawezi kubadilisha msaafu unaotumiwa duniani pote. Yalichangia kuonyesha sense of insecurity kwa wafuasi wa dini hiyo.
Kichuguu,
Naelewa kwa nini kwako unaona kauli ile ni nyepesi.

Wala sikulaumu.
 
Kichuguu,
Naelewa kwa nini kwako unaona kauli ile ni nyepesi.

Wala sikulaumu.
Sasa mzee mwenzagu nawe unaamini kweli kuwa maneno ya Sofia yangeweza kubadilisha msaafu.?

Tuliokulia vichochoroni tunaamini kuwa kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kupapa usingizi, au kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Kwa nini hawakuona kuwa hizo ama zilikuwa kelele za mlango au ni kelele za chura tu wakaendelea na shughuli zao kuliko kuanza kufanya vurugu?
 
Elimu duni kwa waislam ni janga Sana kwa dunia iliyostaarabika.
Geb,
Kwa asiyekuwa Muislam atapata tabu sana kuelewa kwa nini Muislam anapokwenda haja kubwa au ndogo lazima ajikoshe kwa maji tena yanayotiririka.

Halikadhalika atapata tabu kujua kwa nini anaposwali lazima atawadhe kuchukua udhu.

Hivyo hivyo asiyekuwa Muislam hawezi kuelewa kwa nini ilipoguswa Qur'an mara moja na bila kuchelewa Sheikh Ali Ani, Sheikh Nasser Bachu na masheikh wengine walitoa matamko ya tahadhari.

Qur'an ni kauli yake mwenyewe Allah SW.

Ningeweza kueleza mengi lakini naamini nimeeleweka.
 
Sasa mzee mwenzagu nawe unaamini kweli kuwa maneno ya Sofia yangeweza kubadilisha msaafu.?

Tuliokulia vichochoroni tunaamini kuwa kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kupapa usingizi, au kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Kwa nini hawakuona kuwa hizo ama zilikuwa kelele za mlango au ni kelele za chura tu wakaendelea na shughuli zao kuliko kuanza kufanya vurugu?
Kichuguu,
Yasingeweza kubadili chochote.

Walichochelea Waislam kitendo chake kingefungua mlango wa kuichezea Qur'an.

Baada ya siku ile hali imetulia hadi leo.
Somo limesomeka na kueleweka.
 
Kichuguu,
Yasingeweza kubadili chochote.

Walichochelea Waislam kitendo chake kingefungua mlango wa kuichezea Qur'an.

Baada ya siku ile hali imetulia hadi leo.
Somo limesomeka na kueleweka.

Hakika Sheikh Mohammed wao wanaona ni maneno mepesi aliyosema Sofia lakini kwetu sisi Waislamu tuliona kama ni dhihaka ya kiwango cha juu. Leo yeye alianzisha lile na kesho yake angekuja mwingine kusema makubwa zaidi.
 
Biti...
Nimeishi na Wazungu sote vijana wanafunzi katika mazingira ya Ukristo wa Ulaya wakati huo Salman Rushdie ndiyo katoa kitabu chake.

Fatwa ya kuuawa imetolewa na Khomeini.

Hawa wenzangu wanataabika wanashindwa kuelewa lipi kubwa alilofanya Rushdie hata auawe.

Wanataka maelezo kutoka kwangu.

Ndipo nilipotambua kuwa hawajui utukufu wa Allah na Mtume wake.

Hii ndiyo hali waliyonayo baadhi ya wenzetu hapa.
 
Dini ni imani, kauli ya Sophia Kawawa ambaye pia ni mwislam iligusa imani ya waislam wenzake na inawezekana aliitoa sababu yeye alikuwa mwathirika kwani mmewe ambaye pia alikuwa ni mwislam alioa mke zaidi ya mmoja na yeye akiwa mke mkubwa.
Kauli za mashehe kukemea kauli yake zilikuwa sahihi na hata kuandamana pia ilikuwa sahihi ila kushambulia maofisi inaonyesha kulikuwa na ajenda nyingine iliyojificha
 
Kipande kipi hicho mkuu

Jinsi Kawawa alivyoanzisha UWT..
Na kumpa mkewe Uenyekiti wa kwanza
Kawawa akaongeza mke.. Anna Abdalla..
Ambae nae alikuja kuwa Mwenyekiti wa UWT wa pili...vita Kati ya wake wawili wa Kawawa
Ndo ilipelekea Mke mkubwa kusema Quran ibadilishwe ili imzuie mumewe asioe Mke WA pili...
 
Dini ni imani, kauli ya Sophia Kawawa ambaye pia ni mwislam iligusa imani ya waislam wenzake na inawezekana aliitoa sababu yeye alikuwa mwathirika kwani mmewe ambaye pia alikuwa ni mwislam alioa mke zaidi ya mmoja na yeye akiwa mke mkubwa.
Kauli za mashehe kukemea kauli yake zilikuwa sahihi na hata kuandamana pia ilikuwa sahihi ila kushambulia maofisi inaonyesha kulikuwa na ajenda nyingine iliyojificha
Rodrick,
Katika siasa za Zanzibar hicho unachoita agenda ni kinyongo kilichoko miaka mingi ndani ya jamii.
 
Dini ni imani, kauli ya Sophia Kawawa ambaye pia ni mwislam iligusa imani ya waislam wenzake na inawezekana aliitoa sababu yeye alikuwa mwathirika kwani mmewe ambaye pia alikuwa ni mwislam alioa mke zaidi ya mmoja na yeye akiwa mke mkubwa.
Kauli za mashehe kukemea kauli yake zilikuwa sahihi na hata kuandamana pia ilikuwa sahihi ila kushambulia maofisi inaonyesha kulikuwa na ajenda nyingine iliyojificha
Hilo la vurugu ni kawaida hasa kwa vijana ambao huwa wanaona sifa kufanya vitendo viovu kama vile kuvunja maduka na kuiba vitu, kupiga mawe ovyo, na kadhalika. Na hii hutokea sehemu nyingi duniani na hasa pale polisi wasipokuwepo katika eneo la tukio.

Hebu ona ambavyo wafuasi wa Trump walipovamia white house, wengine waliingia mpaka kwenye ofisi ya Spika na kuiba computer yake.
 
Kumbe huyu mama alishawahi kuolewa na Kawawa?

Ni mke wa Pius Msekwa kwa sasa huyu nadhani!

Kesi ya Msekwa kumnyanga'nya Mke Kawawa
Ilipelekwa Kwa Rais Mwinyi kipindi hiko...

Hii nchi ina historia
 
Geb,
Kwa asiyekuwa Muislam atapata tabu sana kuelewa kwa nini Muislam anapokwenda haja kubwa au ndogo lazima ajikoshe kwa maji tena yanayotiririka.

Halikadhalika atapata tabu kujua kwa nini anaposwali lazima atawadhe kuchukua udhu.

Hivyo hivyo asiyekuwa Muislam hawezi kuelewa kwa nini ilipoguswa Qur'an mara moja na bila kuchelewa Sheikh Ali Ani, Sheikh Nasser Bachu na masheikh wengine walitoa matamko ya tahadhari.

Qur'an ni kauli yake mwenyewe Allah SW.

Ningeweza kueleza mengi lakini naamini nimeeleweka.
hilo lakujisaidia haja ndogo na maji tlilika nakupinga mbona wengi nawaona hata vichakani wanaenda bila maji
 
Mwanamke alitetea wanawake wenzake kwa kusema kitabu kinachowakandamiza kibadilishwe

Mwanaume huko zanzibar Ambaye kitabu kinampa pawa ya kukandamiza wanawake akaamua kuchochea maandamano .

Ni kweli hicho kitabu kinawakandamiza wanawake

Badala ya wanaume kujibu hoja wakaandamana ili waendelee kutetea kitabu kinachowapa pawa ya kuwakandamiza wanawake.

Swali kwa mtu mwerevu mwenye busara na aliye neutral(asiye na upande)
Nani alikuwa hero kwenye hii story?
Sofia Kawawa.
 
Yani mtu aibuke akosoe andiko la Biblia Takatifu Eti wakristo waandamane na taharuki?!

Watu watampuuza na kuendelea na maisha yao na hiyo haiwezi kuathiri Ukristo kamwe.

Mfano ni yule Nabii Tito na vituko vyake lakini werevu wanampuuza na kumuona mwehu na kumhurumia.

Sijui dini nyingine kwanini wana react kwa namna za ajabu na machafuko kama yote.?!

Mungu anapaswa kujitetea mwenyewe na Ndiyo maana ya kuitwa Mungu iwapo atatetewa na Wanadamu basi werevu wataanza kutilia Shaka Uungu wake!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom