ICHANA
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 4,765
- 3,598
ICHANA Mnapokuwa mmeingia kwenye ndoa, hapo sasa ndipo utumwa hukamilika! Sio rahisi kutoka tena (hasa kwa Wakristo) lakini mume/mke huyo atakuonyesha kila aina ya vimbwanga kuthibitisha kuwa hana mapenzi na wewe.
Inawezekana ukahitaji haki yako ya ndoa lakini akawa mgumu kukupa, kwa sababu hakupendi! Alikuoa/olewa na wewe kwa sababu ya shinikizo na sio mapenzi, lakini kwa kuwa tayari unakuwa umeshazoeana naye inakuwa vigumu kumtoa moyoni mwako.
ni kweli usemayo na ndo mana tunasema tujitahid kufanya maamuzi sahihi hta kama yatakuwa yanatuumiza kwa wakati kuliko kuchelewa kufanya uchaguzi mzuri kwenye mapenz.....
ndoa nyingi zimekaa mkao ya chura ukiulza kulikoni utagundua mmoja wao alimpenda mwingine kwa sababu ya kitu fulani/au alishawishiwa na mtu fulani/alimsaidia kwenye jambo fulani badala ya kumpenda the way she/he is na tabia yake
mapenzi ya kupenda kwa sababu ndo unakuta hta tendo la ndoa watu wanaombana huna uhuru na ndoa yako hujiamin hta kidogo
kutokujiamin kwa wanandoa wanakosa kauli za kurekebishana malalamiko yasiyoisha ndo hapo utumwa unapozidi