Maana na matumizi ya neno "Hayati" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana na matumizi ya neno "Hayati"

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by EMT, Apr 10, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ninavyoelewa origin ya neno "hayati" ni kwenye lugha ya Kiarabu ambalo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni "my life". Lakini kwa mujibu wa dictionary ya Kiingereza neno "hayati" linatumika zaidi "in an affectionate way usually towards someone who means a lot to you." Kwa mfano, "Goodbye my life" ni sawa na "Goodbye my Hayati".

  Kwenye Kiswahili, neno "hayati" huwa linatumika zaidi kwa mtu ambaye ni marehemu. Je, lina maana sawa na ile maana ya Kiarabu? Ni marehemu wa aina gani wanaostahili kuitwa "hayati"?
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa aliyekufa
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  "Mheshimiwa" ni mtu wa aina gani?
   
 4. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu kwa ufafanuzi. Kwa hiyo kwenye lugha ya Kiswahili hayati inaweza kutumika kwa marehemu yoyote, na sio tuu kwa "waheshimiwa" kama mchangiaji mmoja aliposema hapo juu? Maana wengi tunadhani kuwa "hayati" huwa inatumika zaidi kwa viongozi au watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii na "marehemu" kwa kila mtu.
   
 6. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa kiswahili cha Tanzania Hayati limetumika kisiasa zaidi. Huwatambulisha Marehemu ambao katika uhai wao walikuwa na mchango mkubwa na tena maarufu kwa jamii. Mifano ni baadhi ya viongozi wakuu wa kabila waliopambana vikali kuupinga ukoloni, viongozi walioshiriki kwa namna mbalimbali harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, Zanzibar, na wale waloshika uongozi wa Taifa ngazi za juu. HaaMifano ni Hayati Chifu Mkwawa, Hayati Seti Benjamin, Hayati Abedi Amani Karume, Hayati Moringe Sokoine, Hayati Julius Kambarage Nyerere, nk.
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo unaweza kuonisha vipi na Steven Kanumba kuitwa hayati?
   
 8. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hayati inatakiwa itumike kwa kila mfu mwanadamu na kwa aliye hai,kama wewe ni islamic kuna aya inasema(Fih hayati dunia wal akhera)sina hakina na spelling.Hii inamaanisha kwamba kuna hayati wa duniani na hayati wa akhera.
  Ila kwa taratibu za kibinadamu aliye hai huwezi kumuita hayati ingawa aya hii inamaanisha kwamba aliye hai ni hayati mtarajiwa bila kujari kipato chake.
  So ata wewe hata kama unaishi under $1 per day ukifa inatakiwa tukuite"hayati EMT"
   
 9. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa misingi ya kisiasa nakijamii niloitaja mwanzo Kanumba hakuwa na sifa kama nilowataja na hivyo hayati halimstahili. Bado hatuna jinsi ya kuwazuia rafiki wala ndugu kumtaja wapendavyo ila kwenye kumbukumbu rasmi za Serikali ya Tanzania ndo hatutegemei aorodheshwe kama hayati.
   
 10. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Yea, Uarabuni mtu anaweza kuitwa Hayati kama first name. Ni jina kama majina mengine tuu. Lakini lugha ya Kiswahili sidhani kama unaweza kumwita mtu hai Hayati.
   
 11. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  .

  Mkuu, EMT,

  Neno Hayati lina maana mbili:


  Maana ya Kwanza: deceased, departed


  Hayati huwakilisha mtu aliyekufa … yaani the late Mfano The Late Sokoine etc


  Maana ya Pili: Life


  Hayati huwakilisha Uhai (maisha) mfano kama una mgonjwa anaumwa alafu mtu akikuuliza vipi EMT anaendeleaje unaweza kumjibu .. Aah yupo yupo tu si hayati wala si mamati ikimaanisha EMT is still unwel  Haya hii hapa ni kwa mujibu wa
  KAMUSI ya TUKI kuhusiana na tafsiri / Matumizi ya Hayati  hayati nm [a-/wa-]


  1. deceased, departed, the late: ~ Shaaban Robert the late Shaaban Robert.


  2. life. (mt) Si hayati si mamati, si mzima si mgonjwa he/she is still unwell.


  .
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280

  Tatizo la Lugha, neno moja linalotoholewa kwenye lugha nyingine linaweza likabaki na maana ileile ama inayofanana na ile au ni kinyume kabisa,
  Lakini cha muhimu ni kulichukulia hilo neno jipya kama lilivyo na linavyotumika katika hiyo lugha husika, hata Lugha za kibantu pia zina hiyo tabia

  mfano wa maneno yaliyobadilika maana ni wa Kiswahili na Kishona (Zimbabwe,Botswana,SouthAfrika/Mozambique)

  KISU (Swahili) , Shona wao waasema BANGA(PANGA)
  MAVU.ZI (Swahili), Shona wao wanasema NUWELE (NYWELE)
  NYWELE (
  Swahili), Shona wao wanasema MAVUDZI
  MAJI (Swahili),
  Shona wanasema MVULA (MVUA)
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kilimanjaro hotel mbona nayo yaitwa Hayati?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Neno KUKAZA ndilo linanipa shida sana katika kiswahili
   
 15. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  vp unatafuta neno la kumwita ndugu yenu kanumba?
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nilidhani inaitwa Hyatt? Mmoja wa wamiliki wa kwanza kabisa wa hizo hoteli alikuwa anaitwa Hyatt von Dehn
   
Loading...