Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,774
- 128,771
Kwahiyo wafanye makosa tu kadri wanavyoweza kwakua Spika yupo atawakingia kifua?
Mkuu inamaana huoni namna tunavyotengeneza matabaka hapa? Kwamba wengi e wanakamatwa tu na wengine mpaka ruhusa itoke kwa mtu flani?
What happened to Article 13 ya CURT of 1977?
Kimsingi sipingani na maelezo yako, lakini ukijaribu kuangalia kuna mtindo wa sheria kutekekezwa kwa kufuata double standard na yote hayo yanasababishwa na kitendo cha kutoshitakiwa kwa rais akiwa na baada ya kutoka madarakani. Kwa katiba ya nchi yetu ilivyo rais yuko juu ya sheria na ndio maana unaona kuna sheria zinakiukwa na utashi wa rais ndio unakuwa sheria. Laiti wote tungebanwa na sheria usingeona haya yanayoitwa makaburi na watu kujifanyia wanavyotaka kumfurahisha rais. Nchi ya Marekani pamoja na mapungufu yake hata rais anashitakiwa ndio maana unakuta sheria zinafuatwa na wote. Hapa kwetu rais anafanyo lolote na sheria haimgusi zaidi ya watu kulalamika, na hilo linaenda mbali zaidi mpaka wale wanaomzunguka wakiamua kutumia ukaribu huo nao wanakuwa juu ya sheria. Angalia awamu zote, wote waliokuwa karibu na marais wa awamu hizo ndio walioongoza kwa kuvunja sheria huku vyombo husika vikiwakalia kimya. Tukitoa kinga ya rais kushitakiwa basi kwa sehemu kubwa sheria zitafuatwa.