Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,547
- 47,199
Hivi majuzi Mh. Spika alihitimisha mjadala wa muendelezo wa debate sehemu mbali mbali kuhusiana na vitwndo vya Polisi kuwakamata wabunge, kwa kutoa kauli kwamba, of is a yoyote anayemhitaji mbunge lazima amwambie!
Ingawa kwa macho ya wabunge wengi ni kauli sahihi, lakini Spika na wabunge wanasahau kwamba wabunge hawapo katika makundi ya watu wenye immunity ya kushtakiwa kutokana na makosa wanayoyafanya wakiwa wabunge kama kosa hilo halijafanyika ndani ya Bunge, ingawa Kuna utaratibu wa kumwajibisha mbunge kwa kosa atalolifanya akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge!
Kwakua basi wabunge wanastatus sawa kabisa na raia wengine wanapokua nje ya ukumbi wa Bunge sio vyema kuanza kutengeneza matabaka ya watu katika nchi hii tunayoishi wote.
Haiingii akilini kwanini mtu afanye kosa halafu itoke ruhusa ya Kumkamata au kutomkamata! Huko ni kupotoka na kuelewa madaraka tu tuliyowapa sisi kwa kura zetu wenyewe.
Katiba ya nchi haimuweki Mbunge juu ya sheria za nchi, wala haimpi mamlaka Spika ya kuzuia vyombo vya dola kufanya kazi yake pale inapotakiwa kufanya hivyo!
Ningependa kujua, agizo hilo la spika limetokana na sheria ipi na litakua na vigezo gani kwa spika kutoa ruhusa ya Mbunge kukamatwa!
Je, spika haoni kwamba ruhusa yake itakua imeprejudice court process!
Mfano akaletewa hati ya kukamatwa kwa mbunge! Akasema hapana asikamatwe! Haoni kwamba atakua amechukua jukumu la polisi na mahakama at the same time? Na je kwa katazo hilo haoni kwamba atakua amezuia haki ya upande mwingine kupatikana?
Sidhani kama wabunge wamechukulia kwa uzito kauli zao na kuzipima na namna katiba inavyotaka au namna jamii inavyolichukulia swala zima la usawa mbele ya sheria?
Kwa uchache ni kuwa Bunge limeonesha ubinafsi wa hali ya juu, na kuzidi kutengeneza matabaka baada ya kuendelea kuwa kada inayopokea masarufu mengi na mazuri kuliko wengine.