Maamuzi ya Serikali ni Shaghala Baghala! No Coordination! Do We Need a System, or Hii ya 1-Man Show inatosha?

Suala la kujifukiza mbona ni la kawaida Afrika!
Kwa sisi tuliokulia vijijini na tulioishi na wazee wa zamani,kila tunapopatwa na homa ya aina yeyote ile huwa tunafukizwa nyungu.
Hata Mapepo hukimbia kwa Nyungu na mafusho.
Suala la kussema Temperature kuathiri ngozi,inategemea na umakini wa wa ufanyaji wa kufusha.
Khusu kuathiri mfumo wa kupumua,hilo halijawahipo kusikika huku kwetu,kwani Nyungu ni miti maalumuinayofahamika kwa tiba, haina fumes enye Madhara ya papo kwa papo.
Labda Daktari atuthibitishie kwa data na reserch iliyofanywa na kugundulika madhara ya aina fulani ya muda mrefu.
Bado Magufuli yuko Very right kwa hili.Hizi ni tiba zetu za Kiafrika,kwa vile hakuna tiba rasmi 'yet'
Mkuu hujui kama kweny pua Kuna capillaries nyingi ambazo hupasha joto hewa ili iingie kweny trachea ikiwa na uvuguvugu lakn unapojifukiza mvuke kwanza hewa inakuwa ina contains kias kubwa na maji na kwa sabab ni hewa ya moto Kuna hatar pia Kupasua blood vessels kweny pua au tranche huoni ilo ni tatizo??

Ni vile tu tunafanya vitu kienyeji lakn kitaalam hicho kitu ni kibaya kwa respiratory system 🙏
 
Mkuu huoni tatizo apo et??
Mtu anasema karantini ni ujinga kwel?? Mtu ukiwa na corona ruksa kuwaambukiza wengine
Mtu anasema tutumie mvuke lakn naibu waziri mtaalam wa magonjwa ya mripuko Dr faustine alitoa tamko kujifukiza mvuke ni hatar sababu mvuke wamoto kuleta some complications kweny respiratory system Alafu wewe unakuja kuona ni Sawa et?? Ok kila mtu na uwezo wake wa kufikiria we are on right track wacha liende 🙏
Fuata uliloambiwa na wataalam wa afya..kama experts wamesema hiyo ya mvuke ipo poa,ifanye....sababu kuna wale waliopona corona walisema wana mazoea ya kunywa maji ya moto...cha msingi fuata kilichopitishwa na wataalam........hao watu wa milipuko bongo sijaona hata msaada wao.
 
Pascal,

Katika utumbuaji ambao namuunga mkono Bw. Magufuli ni huu wa mkurugenzi wa Tanesco.

Kwanza tukubaliane kuwa bei za umeme tayari ziko juu sana. Mkurugenzi wa Tanesco kama mtaalam wenye dhamana ya kuendesha shirika kwa ufanisi ana wajibu wa kuwa mbunifu (innovative) na kutumia fursa lukuki zilizopo za kupunguza gharama na kuongeza ufanisi badala ya kulala tu na kuota kupandisha bei za umeme. Kiuhalisia, Tanesco tayari inapaswa kupunguza bei ya umeme kwa kiasi kikubwa.

Madahifu makubwa ya Tanesco kiutendaji ni pamoja na kutokuwajali wateja wake (poor customer service) na kukumbatia gharama za kijinga zisizo na tija.

Biashara kuu ya Tanesco ni kuuza unit za umeme na ili kuongeza mauzo ni lazima iwe na ufanisi katika kuongeza wateja. Hapa kuna tatizo kubwa! Tanesco inanyanyasa sana wateja wanaoomba kufungiwa umeme. Dar pekee kwa sasa kuna maelfu ya wateja (vikiwepo viwanda) walioomba kufungiwa umeme na kulipa gharama zote lakini hawajafungiwa kwa visingizio vya kijinga. Kisingizio kikubwa wanachotoa Tabesco siku hizi ni kukosekana kwa nguzo. Kweli? Hakuna nguzo? Sasa huyo mkurugenzi anafanya nini kama hawezi kuhakikisha input muhimu kwenye core business anayosimamia inapatikana? Lakini tujiulize, kweli hakuna nguzo?

Halafu kuna mantiki gani ya wafanyakazi wa Tanesco kutumia umeme bure wakati wanalipwa mishahara, tena minono? Hiyo mishahara wanayolipwa wanafanyia nini? Hii ni biashara kweli au ni shamba la bibi? Tanesco inapaswa kuwajibika kwa wateja wake ni sio kwa wafanyakazi wake.

Katika nchi nyingi kazi wa kuunganisha umeme kwa wateja hufanywa na private contractors ili kupunguza gharama za uendeshaji. Wale wale mafundi walioidhinishwa kufanya wiring ya umeme kwa wateja wanapaswa ndio hao hao waunganishe umeme kwa kuwa na mkataba na Tanesco. Hatua hii itapunguza maelfu wa mafundi waliojiriwa moja kwa moja Tanesco na hivyo kupunguza wage bill na kupunguza pia kwa kiasi kikubwa gharama ya usafirishaji.

Huyo mkurugenzi alipaswa atekeleze haya (na mengine) badala ya kufikiria kuwabebesha mzigo wateja.
Naomba niongezee kidogo.nchi Kama afrika kusini matatizo madogo madogo pamoja na kuunganishiwa umeme shughuli zote hizi hufanywa na contractors .hii inaongeza ufanisi wa kazi hakuna kuringa Wala rushwa .wilaya Kama ya kinondoni inakuwa na contractors Kama 30 likitokea tatizo ukipigiwa simu usipoenda anapigiwa mwingine anachukua kazi wewe unalala na njaa.ni kawaida sana kukuta watu wakifanya kazi saa Saba usiku
 
Mkuu nashukuru sana kwa mchango wako, na unatoa nafasi ya akili pevu kushugulishwa.
Ukitaka kumfahamu Rais Magufuli na maamuzi yake au maamuzi ambayo anataka yatokee lazima ufanye uchambuzi wa kina wa mambo yake yote yafuatayo.

Nitaanza kwa kuuliza Rais Magufuli ni nani?
  1. Aina ya makuzi yake ?
  2. Ni nani amekuwa akishirikiana nao
  3. Utotoni
  4. Kipindi cha masomo yake
  5. Kipindi cha wakati akifanya kazi
  6. watu gani amechanganyika nao na kutumia muda mwingi akiji changanya nao
  7. Wato ambao anawahusudu ( role model wake)
  8. Aina ya taratibu ambazo anafuata kupata majawabu ya vitu avifanyavyo
  9. Utamaduni wa jamii (kabila) analotoka.

Hakika moja ambayo haipingiki ni: Rais Magufuli ni Kiongozi ambaye ana fanya shughuli zake akitaka matokeo tuu, hasa yale anayo kusudia yatokee.

Kazi hii ni kubwa lakini itatupa nafasi ya kujua mambo mengi pamoja na Viongozi anao wataka katika teuzi zake.

Suala la maamuzi yake kuwa sahhihi au laa, matokea ya kutimiza nia yake na kufikia majibu anayo yataka ? Hili ni jambo jingine kabisa’

Nchi hii inaweza kupata maumivu mengi , lakini wangepatikana Magufuli 300 katika ngazi mbali mbali za utawala wake katika teuzi zaidi 2500 ambazo Rais anatakiwa kizufanya naamini nchi yetu ingeenda mbali sana. ( He is a results oriented,realist and full of dreams leader).

Tatizo letu wengi ni kupenda kufuata urasimu hata usio na matokeo...Tunafarijika tu pale tunapofuata taratibu ili tusipatwe na matatizo ya kuulizwa kwanini hili limetokea...Waoga waoga wa kutafuta suluhu hata kama utawajibika kwalo.

Mh. Rais siyo mwanasiasa tu, anatumia siasa kupata nafasi lakini ni mtendaji anayependa kuona mambo yakienda kwakutumia akili uwezo na mazingira halisi. Wengi wetu tuko so abstract, tunapenda hadithi ndefu zisizo na results!
 
Tatizo letu wengi ni kupenda kufuata urasimu hata usio na matokeo...Tunafarijika tu pale tunapofuata taratibu ili tusipatwe na matatizo ya kuulizwa kwanini hili limetokea...Waoga waoga wa kutafuta suluhu hata kama utawajibika kwalo.

Mh. Rais siyo mwanasiasa tu, anatumia siasa kupata nafasi lakini ni mtendaji anayependa kuona mambo yakienda kwakutumia akili uwezo na mazingira halisi. Wengi wetu tuko so abstract, tunapenda hadithi ndefu zisizo na results!
Thanks so much for your contribution, a good analysis of how he does things, but have you ever visit the consequences on many decisions he makes ? He should do so to minimize the negative impacts if any?
 
Wana bodi,
Mfano ni hili la kupanda bei ya umeme, japo Watanzania hatukuwahi kujulishwa rasmi, lakini naombeni niwajulishe rasmi kuwa lile deni la tozo ya Dowans, ambalo watu walijiapiza kuwa hatulipi, na wengine hadi kudai, "over my dead body hatulipi!" , ukweli ni kuwa tumelipa every cent!, hivyo Umeme lazima upande bei Watanzania wote kwa umoja wetu, tufidie deni hilo kupitia kupanda kwa bei ya Umeme!.

Happy New Year.

Paskali
Mtu ukisema kitu cha uongo kwa hisia tuu, mfano kama nilivyosema hapa 5 years ago, kuwa "fedha za Dowans zimelipwa."

Baadae ukagundua ulisema uongo, ni ustaarabu kukubali kosa na kuomba radhi. Hivyo wanabodi kwa post hii nawaomba msamaha, sikusema kweli Bali ni nilihisi to kwa hisia kuwa fedha za Dowans zimelipwa. Ukweli ni kuwa, miaka mitano hii ya nyuma, fedha za tozo ya Dowans, haikuwa imelipwa, Ila sasa ndio tozo hii imelipwa na serikali ya awamu ya 6.
Mnisamehe Sana,
Nimekosa mimi
Nimekosa mimi
Nimekosa Sana.
P
 
Ukweli ni kuwa, miaka mitano hii ya nyuma, fedha za tozo ya Dowans, haikuwa imelipwa, Ila sasa ndio tozo hii imelipwa na serikali ya awamu ya 6.
Mnisamehe Sana,
Nimekosa mimi
Nimekosa mimi
Nimekosa Sana.
Ni la kweli hili ?, Amelipwa kiasi gani huyu Dowans ?na kwanini iwe sasa ?
 
Ni la kweli hili ?, Amelipwa kiasi gani huyu Dowans ?na kwanini iwe sasa ?
Tozo za ushindi mahakamani, ziko za Aina mbili, Ile awards ya kwenye hukumu sio siri, inajulikana, baada ya serikali yetu kushindwa mahakamani, na waliosababisha kujiapiza ," over our dead bodies", hatulipi!.

Serikali ilikubali settlement out of court, hivyo waka negotiate na mdai, the settlement deed is not public, sasa hii ni biashara na inalindwa na vipengele vya confidentiality. Hivyo hatujui amelipwa nani na kiasi gani. Subirieni ripoti ya CAG mid April bungeni ndio tutajua.
P
 
Wana bodi,

Kiukweli kabisa, baadhi ya maamuzi ya taasisi za umma za serikali ya Magufuli ni shaghalabaghala!, yanaonyesha hakuna coordination kati ya serikali na taasisi zake, haiwezekani taasisi moja ya serikali iseme kitu hiki, kisha taasisi nyingine ya serikali hiyo hiyo ikanushe!, Waziri mmoja wa wizara hiyo aseme hivi, kisha naibu waziri wa wizara hiyo hiyo aseme vingine, halafu katibu mkuu nae aseme lake!. Haiwezekani rais aseme jambo, halafu waziri anakuja kilikanusha, kama Ile ya "fyatueni watoto tutawasomesha bure" kisha Waziri anakanusha. Mkuu wa mkoa anapanga kufanya jambo fulani kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, anaita waandishi wa habari, analitangaza jambo hilo, serikali ipo, imesikia mipango hiyo, imekaa kimya. Kisha serikali ya mkoa inaanza utekelezaji, ndipo Waziri anaibuka na kusema this is wrong!. Tukisema baadhi ya maamuzi ya serikali hii ni shaghalabagala, tutakuwa tunaionea?.

Kiukweli baadhi ya watendani wa Magufuli wanafanya kazi kwa nidhamu ya woga, sheria, taratibu na kanuni za kufanya mambo zipo, hazifuatwi, sasa kila kitu kinategemea maamuzi ya mtu mmoja tuu, anatakaje, sio bodi tena, sio menejimenti tena, sasa ni bwana Mkubwa tuu, anachotaka ndicho!. Kwa mtindo huu, ni lazima abadilike, vingenevyo kiukweli kabisa, hatutafika salama!, serikali hii itakuwa ni hire and fire, kuanzia kwa mawaziri, managements na bodi kuliko awamu nyingine yoyote because no one is sure what next!.

Mfano ni hili la kupanda bei ya umeme, japo Watanzania hatukuwahi kujulishwa rasmi, lakini naombeni niwajulishe rasmi kuwa lile deni la tozo ya Dowans, ambalo watu walijiapiza kuwa hatulipi, na wengine hadi kudai, "over my dead body hatulipi!" , ukweli ni kuwa tumelipa every cent!, hivyo Umeme lazima upande bei Watanzania wote kwa umoja wetu, tufidie deni hilo kupitia kupanda kwa bei ya Umeme!.

Kupanda kwa bei ya Umeme is a process, Ikulu ilijua, Prof. Muhongo alijua, rais alijua halafu rais anaingilia kati kujifanya hakujua!, waziri nae anajifanya hakujua!, hivyo rais anaamua kumtumbua mkuu wa taasisi moja tu!, kisha watu wote tunashangilia as if it's a good move!. There must be something wrong somewhere!.

Kwenye politics kuna kitu kinaitwa "scapegoat" Kizaramo ni "bangusilo", ambapo mambo yakiharibika, unajikosha mbele ya umma kwa kumtafuta mtu wa kumtoa kafara ili watu wakushangilie, yaani watu wanashangilia bangusilo badala ya kudeal na the real usues zinazopandisha bei ya umeme! kama IPTL, Simbion etc.Mkuu Mkarimani, kupandisha bei ya umeme ni process ambayo inapitia hatua zifuatazo
Kabla sijaitaja hii process ya kupandisha bei ya Umeme, naomba niwasaidia members kujua kuwa kwenye watumishi wa serikali, wamegawanyika sehemu mbili, kuna watumishi wa serikali ambao ni watumishi tuu, na kuna watumishi wa serikali, ambao sio watumishi tuu, bali ni watumishi kwa upande mmoja na kwa upande wa pili, ni "wale Jamaa", nikisema hivi naamini mnanielewa, "wale Jamaa" ni kina nani!. Sasa hawa "wale Jamaa". wapo katika kila idara ya serikali nzima, wako kwenye kila shirika, wako kwenye kila taasisi ya umma, wako kwenye kila management, wako kwenye kila bodi, karibu ma secretary wote ni wale, wapika chai ni wale, wafagizi ni wale, madereva ni wale etc. etc.
Mkuu wa nchi anapata 5 daily briefings daily,
  1. daily security briefing toka director wa TISS,
  2. daily defense briefing toka kwa CDF,
  3. daily government briefing toka kwa PM,
  4. daily international briefing toka MFA,
  5. daily financial briefing kutoka Hazina na
  6. daily press briefing toka kurugenzi yake ya habari kuhusi kila kilichoandikwa kwenye media.
Process ya kupandisha bei ya Umeme.
1.Menejiment ya Tanesco inaomba kibali cha kupandisha bei Umeme kutokana na gharama za uzalishaji na kufidia Madeni, ombi hilo linapelekwa kwenye bodi, kabla hata ombi hilo halijafika bodi, wale Jamaa walioko menegment wanaripoti kunako!. Kwenye bodi ya Tenasco ina serikali ndani yake, na Jamaa wa bodi nao wanaripoti kunako! na ina ikulu ndani yake, M/Kiti ni mteule wa rais na anawajibika kwa waziri husika.
2. Bodi inapitia maombi, inajiridhisha, inatoa kibali cha kupeleka naombi Ewura, Waziri husika anajulishwa, ikulu inajulishwa rasmi lakini wale Jamaa nao wanaripoti.
3. Service provider ambaye ni Tanesco anatuma maombi ya ombi la kuongeza bei ya umeme kwa Ewura akiambatanisha sababu za msingi na mkokotoo wa gharama.
4. Ewura inapokea maombi, inaitisha kikao cha stakeholders kukusanya maoni yao na kufanya upembuzi yakinifu. Ndani ya Ewura wale Jamaa wapo nao wanaripoti.
5. Ewura inafikia uamuzi inatangaza kusudio kw la kupandisha bei, inaitisha bodi ya Uwura kubariki ongezeko hilo. Ndani ya bodi ya Ewura, serikali imo na ikulu imo na wale jamaa wamo. Bodi inabariki uamuzi huo na kuipa Menejiment ya Ewura a go ahead ya kutangaza huku waziri husika akihusishwa na ikulu ikitaarifiwa na wale Jamaa wakiripoti.
6. Ndipo Ewura wanatangaza Bei Mpya za Umeme.
Kwa mchakato huu, mtu akisema baadhi ya maamuzi ya taasisi za serikali ya Magufuli ni shaghala Baghala, tutakuwa tunawaonea? .

Kwa serikali ilijua kabla, ikulu ilijua kabla, kwa vile vyombo vyote hivyo vilipaswa kujua na kuzuia kabla ya kutangazwa ongezeko.

Kama ni kweli ikulu haikujua na serikali haikujua, hii ni gross negligence na wahusika sio Menejiment za Tanesco na Ewura bali ni lile jicho la serikali inside Tanesco na inside Ewura, na wale jamaa zetu, unless they were all compromised! .

Wakati wa Nyerere madudu kama haya hayakuwepo kwa sababu no one was sure of who is who, sometimes hadi mfagizi na mpika chai, info zinafika kunako! .

Uamuzi wowote wa kupandishwa kwa gharama za utilities (umeme, maji, gesi) is a due process na kote menejment zinaomba kibali kwenye bodi zao ambako serikali ipo na ikulu ipo, na wale Jamaa wapo, Waziri husika lazima anatumiwa copy ya board resolutions zote za bodi zilizo chini yake, hivyo mtu mmoja tuu asifanywe ndio kondoo wa kafara, wahusika wote nao wawajibishwe!.

Japo Bangusilo ni boss wa Tanesco tuu, lakini amini nawaambie huku ya karma, haitamuacha salama Prof. Mhongo na boss wa Ewura!.

Ili Tanzania tusonge mbele, we need an effective systems and not a one man show!. Hii hire and fire ya mawaziri na watendaji wakuu kila uchao, ambayo wengi wanaishangilia, kwa ma deep thinkers, ni dalili ya incompetence kwenye upande wa vetting, hivyo pia ni uthibitisho wa shaghalabagala. Atakapo kuja kumaliza miaka yake 10, rais Magufuli anaweza kuingia kwenye records kuwa ndiye rais aliye hire na ku fire kuliko rais mwingine yoyote wa Tanzania. Kwa wengine hii hire and fire ni plus on Magufuli, kwa wengine ni minuses, why hire incompetent people in the first place halafu kuja kuwafire?!

Happy New Year.

Paskali
Leo Mama Samia ka prove kuwa hakuna coordination aliporudisha tozo ya mafuta.hongera kwa kuliona hilo mkuu
 
Back
Top Bottom