Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,689
- 119,326
Wana bodi,
Kiukweli kabisa, baadhi ya maamuzi ya taasisi za umma za serikali ya Magufuli ni shaghalabaghala!, yanaonyesha hakuna coordination kati ya serikali na taasisi zake, haiwezekani taasisi moja ya serikali iseme kitu hiki, kisha taasisi nyingine ya serikali hiyo hiyo ikanushe!, Waziri mmoja wa wizara hiyo aseme hivi, kisha naibu waziri wa wizara hiyo hiyo aseme vingine, halafu katibu mkuu nae aseme lake!. Haiwezekani rais aseme jambo, halafu waziri anakuja kilikanusha, kama Ile ya "fyatueni watoto tutawasomesha bure" kisha Waziri anakanusha. Mkuu wa mkoa anapanga kufanya jambo fulani kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, anaita waandishi wa habari, analitangaza jambo hilo, serikali ipo, imesikia mipango hiyo, imekaa kimya. Kisha serikali ya mkoa inaanza utekelezaji, ndipo Waziri anaibuka na kusema this is wrong!. Tukisema baadhi ya maamuzi ya serikali hii ni shaghalabagala, tutakuwa tunaionea?.
Kiukweli baadhi ya watendani wa Magufuli wanafanya kazi kwa nidhamu ya woga, sheria, taratibu na kanuni za kufanya mambo zipo, hazifuatwi, sasa kila kitu kinategemea maamuzi ya mtu mmoja tuu, anatakaje, sio bodi tena, sio menejimenti tena, sasa ni bwana Mkubwa tuu, anachotaka ndicho!. Kwa mtindo huu, ni lazima abadilike, vingenevyo kiukweli kabisa, hatutafika salama!, serikali hii itakuwa ni hire and fire, kuanzia kwa mawaziri, managements na bodi kuliko awamu nyingine yoyote because no one is sure what next!.
Mfano ni hili la kupanda bei ya umeme, japo Watanzania hatukuwahi kujulishwa rasmi, lakini naombeni niwajulishe rasmi kuwa lile deni la tozo ya Dowans, ambalo watu walijiapiza kuwa hatulipi, na wengine hadi kudai, "over my dead body hatulipi!" , ukweli ni kuwa tumelipa every cent!, hivyo Umeme lazima upande bei Watanzania wote kwa umoja wetu, tufidie deni hilo kupitia kupanda kwa bei ya Umeme!.
Kupanda kwa bei ya Umeme is a process, Ikulu ilijua, Prof. Muhongo alijua, rais alijua halafu rais anaingilia kati kujifanya hakujua!, waziri nae anajifanya hakujua!, hivyo rais anaamua kumtumbua mkuu wa taasisi moja tu!, kisha watu wote tunashangilia as if it's a good move!. There must be something wrong somewhere!.
Kwenye politics kuna kitu kinaitwa "scapegoat" Kizaramo ni "bangusilo", ambapo mambo yakiharibika, unajikosha mbele ya umma kwa kumtafuta mtu wa kumtoa kafara ili watu wakushangilie, yaani watu wanashangilia bangusilo badala ya kudeal na the real usues zinazopandisha bei ya umeme! kama IPTL, Simbion etc.
Kabla sijaitaja hii process ya kupandisha bei ya Umeme, naomba niwasaidia members kujua kuwa kwenye watumishi wa serikali, wamegawanyika sehemu mbili, kuna watumishi wa serikali ambao ni watumishi tuu, na kuna watumishi wa serikali, ambao sio watumishi tuu, bali ni watumishi kwa upande mmoja na kwa upande wa pili, ni "wale Jamaa", nikisema hivi naamini mnanielewa, "wale Jamaa" ni kina nani!. Sasa hawa "wale Jamaa". wapo katika kila idara ya serikali nzima, wako kwenye kila shirika, wako kwenye kila taasisi ya umma, wako kwenye kila management, wako kwenye kila bodi, karibu ma secretary wote ni wale, wapika chai ni wale, wafagizi ni wale, madereva ni wale etc. etc.
Mkuu wa nchi anapata 5 daily briefings daily,
1.Menejiment ya Tanesco inaomba kibali cha kupandisha bei Umeme kutokana na gharama za uzalishaji na kufidia Madeni, ombi hilo linapelekwa kwenye bodi, kabla hata ombi hilo halijafika bodi, wale Jamaa walioko menegment wanaripoti kunako!. Kwenye bodi ya Tenasco ina serikali ndani yake, na Jamaa wa bodi nao wanaripoti kunako! na ina ikulu ndani yake, M/Kiti ni mteule wa rais na anawajibika kwa waziri husika.
2. Bodi inapitia maombi, inajiridhisha, inatoa kibali cha kupeleka naombi Ewura, Waziri husika anajulishwa, ikulu inajulishwa rasmi lakini wale Jamaa nao wanaripoti.
3. Service provider ambaye ni Tanesco anatuma maombi ya ombi la kuongeza bei ya umeme kwa Ewura akiambatanisha sababu za msingi na mkokotoo wa gharama.
4. Ewura inapokea maombi, inaitisha kikao cha stakeholders kukusanya maoni yao na kufanya upembuzi yakinifu. Ndani ya Ewura wale Jamaa wapo nao wanaripoti.
5. Ewura inafikia uamuzi inatangaza kusudio kw la kupandisha bei, inaitisha bodi ya Uwura kubariki ongezeko hilo. Ndani ya bodi ya Ewura, serikali imo na ikulu imo na wale jamaa wamo. Bodi inabariki uamuzi huo na kuipa Menejiment ya Ewura a go ahead ya kutangaza huku waziri husika akihusishwa na ikulu ikitaarifiwa na wale Jamaa wakiripoti.
6. Ndipo Ewura wanatangaza Bei Mpya za Umeme.
Kwa mchakato huu, mtu akisema baadhi ya maamuzi ya taasisi za serikali ya Magufuli ni shaghala Baghala, tutakuwa tunawaonea? .
Kwa serikali ilijua kabla, ikulu ilijua kabla, kwa vile vyombo vyote hivyo vilipaswa kujua na kuzuia kabla ya kutangazwa ongezeko.
Kama ni kweli ikulu haikujua na serikali haikujua, hii ni gross negligence na wahusika sio Menejiment za Tanesco na Ewura bali ni lile jicho la serikali inside Tanesco na inside Ewura, na wale jamaa zetu, unless they were all compromised! .
Wakati wa Nyerere madudu kama haya hayakuwepo kwa sababu no one was sure of who is who, sometimes hadi mfagizi na mpika chai, info zinafika kunako! .
Uamuzi wowote wa kupandishwa kwa gharama za utilities (umeme, maji, gesi) is a due process na kote menejment zinaomba kibali kwenye bodi zao ambako serikali ipo na ikulu ipo, na wale Jamaa wapo, Waziri husika lazima anatumiwa copy ya board resolutions zote za bodi zilizo chini yake, hivyo mtu mmoja tuu asifanywe ndio kondoo wa kafara, wahusika wote nao wawajibishwe!.
Japo Bangusilo ni boss wa Tanesco tuu, lakini amini nawaambie hukumu ya karma, haitamuacha salama Prof. Mhongo na boss wa Ewura!.
Ili Tanzania tusonge mbele, we need an effective systems and not a one man show!. Hii hire and fire ya mawaziri na watendaji wakuu kila uchao, ambayo wengi wanaishangilia, kwa ma deep thinkers, ni dalili ya incompetence kwenye upande wa vetting, hivyo pia ni uthibitisho wa shaghalabagala. Atakapo kuja kumaliza miaka yake 10, rais Magufuli anaweza kuingia kwenye records kuwa ndiye rais aliye hire na ku fire kuliko rais mwingine yoyote wa Tanzania.
Kwa wengine hii hire and fire ni plus on Magufuli, kwa wengine ni minus, why hire incompetent people in the first place halafu kuja kuwafire?!
Mfano mwingine wa shaghalabaghala ni tumepitisha sheria mpya ya rasilimali za taifa kuwa uwekezaji wote kuanzia sasa utatumia sheria zetu za Tanzania!, Mwekezaji gani atakubali such a risk ya FDI yake bila assurance ya kutendewa haki kwenye a neutral ground kwa international laws!
Tunapitisha sheria mbovu kwa mbwembwe leo halafu kesho tunazibadili kimya kimya. Hili nimelisema hapa Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?
Happy New Year.
Paskali

Mkuu Mkarimani, kupandisha bei ya umeme ni process ambayo inapitia hatua zifuatazoMuhongo kashasema yeye na wizara yake hawakuhusishwa kwa hilo, alafu nyie jamaa mnasema walikuwa wanataarifa before, mbaya zaidi mnaenda mbali zaidi eti na ikulu walikuwa wanataarifa!! Jaribuni kuwa mnaelewa japo kidogo basi.
Kabla sijaitaja hii process ya kupandisha bei ya Umeme, naomba niwasaidia members kujua kuwa kwenye watumishi wa serikali, wamegawanyika sehemu mbili, kuna watumishi wa serikali ambao ni watumishi tuu, na kuna watumishi wa serikali, ambao sio watumishi tuu, bali ni watumishi kwa upande mmoja na kwa upande wa pili, ni "wale Jamaa", nikisema hivi naamini mnanielewa, "wale Jamaa" ni kina nani!. Sasa hawa "wale Jamaa". wapo katika kila idara ya serikali nzima, wako kwenye kila shirika, wako kwenye kila taasisi ya umma, wako kwenye kila management, wako kwenye kila bodi, karibu ma secretary wote ni wale, wapika chai ni wale, wafagizi ni wale, madereva ni wale etc. etc.
Mkuu wa nchi anapata 5 daily briefings daily,
- daily security briefing toka director wa TISS,
- daily defense briefing toka kwa CDF,
- daily government briefing toka kwa PM,
- daily international briefing toka MFA,
- daily financial briefing kutoka Hazina na
- daily press briefing toka kurugenzi yake ya habari kuhusi kila kilichoandikwa kwenye media.