Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,398
Wana bodi, kiukweli baadhi ya maamuzi ya taasisi za una za serikali ya Magufuli ni shaghalabaghala, yanaonyesha hakuna coordination Kati ya serikali na taasisi zake, haiwezekani taasisi ya serikali iseme hicieron, Kisha serikali ikanushe, halafu rais anaingilia kati anamtumbua mkuu was taasisi moja, kisha water wote tunashangilia as if it's a good move!. There must be something wrong somewhere. Mkuu Mkarimani, kupandisha bei ya umeme ni process ambayo inapitia hatua zifuatazo
1.Menejiment ya Tanesco inaomba kibali cha kupandisha gharama za umeme kwenye bodi ya Tenasco na kutoa sababu. Hiyo bodi ina serikali ndani yake, na ina ikulu ndani yake, M/Kiti ni mteule wa rais na anawajibika kwa waziri husika.
2. Bodi inapitia maombi, inajiridhisha, inatoa kibali cha kupeleka naombi Ewura, Waziri husika anajulishwa, ikulu inajulishwa.
3. Service provider ambaye ni Tanesco anatuma maombi ya ombi la kuongeza bei ya umeme kwa Ewura akiambatanisha sababu za msingi na mkokotoo wa gharama.
4. Ewura inapokea maombi, inaitisha kikao cha stakeholders kukusanya maoni yao na kufanya upembuzi yakinifu.
5. Ewura inafikia uamuzi inatangaza kusudio kw la kupandisha bei, inaitisha bodi ya Uwura kubariki ongezeko hilo. Ndani ya bodi ya Ewura, serikali imo na ikulu imo. Bodi inabariki uamuzi huo na kuipa Menejiment ya Ewura kutangaza huku waziri husika akihusishwa na ikulu ikitaarifiwa.
6. Ndipo Ewura wanatangaza Bei Mpya za Umeme.
Kwa mchakato huu, mtu akisema baadhi ya maamuzi ya taasisi za serikali ya Magufuli ni shaghala Baghala, tutakuwa tunawaonea? .
Kwa serikali ilijua kabla, ikulu ilijua kabla, kwa vile vyombo vyote hivyo vilipaswa kujua na kuzuia kabla ya kutangazwa ongezeko.
Kama ni kweli ikulu haikujua na serikali haikujua, hii ni gross negligence na wahusika sio Menejiment za Tanesco na Ewura.
Then wahusika ndio wawajibishwe!.
Ili Tanzania tusonge mbele, we need an effective systems and not a one man show! .
Happy New Year.
Paskali
Mkuu, unaifahamu nguvu kubwa ilokuwa nyuma ya Tanesco na ongezeko la gharama za umeme?