Maamuzi ya Kijinga Yananigharimu

Maamuzi ya Kijinga Yananigharimu

Fastaaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2016
Posts
575
Reaction score
855
Amani iwe kwenu wana wa MMU.

Katika pita pita na pilika za maisha nikapata kumjua mrembo moja matata jirani na kibarua changu.

Nikapewa namba na outing moja sehemu nzuri, sijui niliikosea hiyo date, maana tangu hapo amekuwa anaruka ruka kukutana tena.

Kosa langu kubwa nilishatongoza kwenye sms na kadhalika.

Akiwa na shida ndogo hivi tunasaidiana, mara ananikopa na cha ajabu analipa tofauti na wengine, basi nikatia nia kuwa endapo atanielewa basi huyo ndo mtarajiwa.

Nini Kimenileta kwenu? Juzi tumechat chat saana, tukafikia hatua tunachagua style za nywele ili apendeze sikukuu, siku hiyo karibu kila txt aliyokuwa ananitumia ilikuwa na neno 'dia' , jana nikatuma pesa za kumtosha saloon na vitu vidogo vidogo, cha ajabu baada tu kutuma pesa, chatting haikuwa ya kiviiile, zaidi nikajikuta nimeomba appointment j2, akasema sikukuu huwa hatoki, nikaomba basi hata jmoc au j3, akasema kwa ujumla hapendi kutoka. na alishaniambia sema najisahaulisha.

Nilichokifanya.
Nilirudisha ule muamala usiku ule ule, na baada ya hapo hajanitxt wala me sijamtxt.

Tatizo liko wapi?
Bado namtaka huyu binti kwa kweli, sasa najihisi nshavuruga, ingawa naye tabia yake ndo imesababisha. karoho kaniniuma, nifenyejeee???
 
Ko umebetti muhamala ukapotea hella zikarudi, unataka kubetti tena angali umejua kabisa mechi zimekaa vibaya
Anyways, ni ngum mwanamke kukutana na mwanaume asiyempenda, ila kama anakupenda, aahhh!!! Ata chooni atakuita
 
Kitendo cha wewe kurudisha muamala ndilo kosa lako.
Unaporudisha muamala ujue unakata relationship yako na mrembo. Hutakiwi kurudisha tena majeshi huko ,itakugharimu mno zaidi ya mwanzo.
 
Ni maamuzi ya kijinga kwelikweli.

Utupie tena muamala wa mwanzo then una mute, akitulia utamtafuta na story zingine zisizohusiana na muamala huo
 
As the man you need to grow some balls, it is clear that women manipulate guys these days , what surprise me is the tendency of guys to fall in the victim category , as for women they are able to take your money and runaway but you guys dont feel doing the same , you continue with the act of losing money hoping that some miraculous day she will come to her sense and attend your needs this is ultimate bullshit grow some balls dude , once a woman friendzone you the only thing you can do is take your things and leave or continue to play a victim forever.
 
Ki hapakazitu hapakazitu 2019

Tunasema ulizingua kiwango cha standard gauge.
 
Uswahili tu ilikuwaje ukarudisha muamala sababu kakukatalia kutoka?

Haya sasa pambana na hali yako mkaka ndio umeshaachwa.
daah laiti ungeona nlivyokuwa najibiwa kabla na baada ya kutuma hela usingeongea hivi. nipe tu ushauri wa kujenga
 
tatizo alikuwa mpole na mnyenyekevu wakati anataka hela
Ko umebetti muhamala ukapotea hella zikarudi, unataka kubetti tena angali umejua kabisa mechi zimekaa vibaya
Anyways, ni ngum mwanamke kukutana na mwanaume asiyempenda, ila kama anakupenda, aahhh!!! Ata chooni atakuita
 
inauma mzee baba, yan mkubaliane apendeze afu usimuone hata kumuona, tena anasema kabisa, hicho hakitakaa kitokee daah, niliona kama dharau hivi.
Kitendo cha wewe kurudisha muamala ndilo kosa lako.
Unaporudisha muamala ujue unakata relationship yako na mrembo. Hutakiwi kurudisha tena majeshi huko ,itakugharimu mno zaidi ya mwanzo.
 
Back
Top Bottom