Maamuzi ya BRELA juu ya logo yangu

Maamuzi ya BRELA juu ya logo yangu

Mr sule

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2021
Posts
606
Reaction score
1,115
Naomba kusaidia hili wakuu.

Nilikuwa na mpango nianzishe brand ya kutengeneza viatu, nguo, kofia na vitu vingine, maana nilitaka itambulike kabisa Brela.

Nilituma maombi ya usajili wa jina na logo(trademark) lakini Brela wamekataa maombi yangu kisa imefanana na logo ya Ferrari.

Lakini ukiangalia logo yangu na ya Ferrari haziendani hata kidogo.

Naweza kufanyaje ili kulalamika juu ya hili ili ipitiwe upya.

Dora brand

IMG_3117.png

ferrari logo​

IMG_3131.png

naona kama zinatofautiana sana hata haziendani.
 
Tatizo ni huyo mnyama hapo umecopy na kupaste, hata mimi nisingekubali huo ujinga.

Unafikiri ni mimi tu ndo natumia huo mnyama, mbona kuna kampuni nyingi zinatumia
 
Unafikiri ni mimi tu ndo natumia huo mnyama, mbona kuna kampuni nyingi zinatumia
Ahaa sasa umefunguka mwenyewe, kumbe ulikopi toka moja ya makampuni uliyoyakusanya logo zao, Logo hutakiwi kukusanya za makampuni mengine kisha unakopi na kufanya mabadiliko kidogo, toa yako kichwani, nakushauri tumia kiwavi jeshi, utampenda.
 
Naomba kusaidia hili wakuu.

Nilikuwa na mpango nianzishe brand ya kutengeneza viatu, nguo, kofia na vitu vingine, maana nilitaka itambulike kabisa brela.

Nilituma maombi ya isajili wa jina na logo(trademark) lakini brela wamekataa maombi yangu kisa imefanana na logo ya ferrari,

lakini ukiangalia logo yangu na ya ferreri haziendani hata kidogo.

naweza kufanyaje ili kulalamika juu ya hili ili ipitiwe upya.

dora brand
View attachment 2127972

ferrari logoView attachment 2127973
naona kama zinatofautiana sana hata haziendani.
Hao jamaa ni pasua kichwa na huwa wanajiona wako sahihi sana..anyway ukiweza fika mwenyewe ukaongee na mkubwa wao
 
toa farasi, weka wekundu wa msimbazi aka Simba anatafuna swala..
 
Hao jamaa ni pasua kichwa na huwa wanajiona wako sahihi sana..anyway ukiweza fika mwenyewe ukaongee na mkubwa wao
Kuna system wanatumia, mfano kama umeweka picha ya dog, wao huwa hawaangali kingine zaidi ya kuingiza jina dog na kama system itaonesha kufanana kwa asilimia 50% ya kampuni zingine! Basi itoshe kuikataa logo yako!

At least mfano unatakiwa uwe chini ya 50%
 
Aisee huyo aliyekukataza atakua mzee wa miaka tisini huko sio kijana, Mbona logo iko tofauti na Ferarri. Ushauri: Mzee avue miwani atazame upya logo yako.
 
Umeshaenda sajili kampuni au hiyo logo unaisajili chini ya miliki ya Nini?
 
Ahaa sasa umefunguka mwenyewe, kumbe ulikopi toka moja ya makampuni uliyoyakusanya, Logo hutakiwa kukusanya za makampuni mengine kisha unakopi na kufanya mabadiliko kidogo, toa yako kichwani, nakushauri tumia kiwavi jeshi, utampenda.

Baada ya brela kukataa maombi ilibidi niangalie makosa yangu, nilikutana na makampuni mengine yanatumia farasi, maana brela wamesema farasi inatumiwa kwenye kampuni ya ferrari.

Kama kisa ni farasi mbona kampuni fulani imeweka farasi.
 
Back
Top Bottom