Maamuzi ni yako kati ya KUISHI ama KUDUMU

chillo clan conscious

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
852
1,559
Naam wana Jamii Forum (Jukwaa)

Binafsi me ni mzima na nyie natamani muwe hivyo ila kama kuna mmoja wetu hayupo sawa kiakili, kiafya, kiuchumi basi asikaribishe nia ya kukata tamaa.

Nafkiri andiko juu lina someka vizuri "MAAMUZI NI YAKO KATI YA KUISHI NA KUDUMU".

Nafkiri misamiati mikuu ya mada ni miwili (2) ambayo ni KUISHI AMA KUDUMU.

NIANZE MOJA KWA MOJA NA:

{1}KUISHI
Kuishi ni kitendo cha kiumbe hai anachojaaliwa maisha ndani ya muda. Kwenye kuishi kuna miko mingi sana ya kuzingatia ili kuepuka kuanguka katika maisha,kujuta katika maisha, kuhuzunika katika maisha,kupoteza uhai katika maisha na mifanano na hayo.

90% ya binadamu katika hii dunia tunapenda KUISHI kuliko KUDUMU

Kwanini namaanisha kuishi,unakuta mtu ana kuwa na matamanio ambayo ni vigumu kuyafikia kwa njia salama matokeo yake anafanya njia batilifu ili kutimiza matamanio yake na hii kupelekea kupata matokeo hasi (-)

{2}KUDUMU
Kudumu ni ile hali ya kiumbe hai/kiumbe kisicho hai kukaa muda mrefu(usio na kikomo fikirika) katika uso wa dunia. Ila katika mada hii napenda tutumie akili ya Fasihi kuchambua na kunielewa vizuri nini na maanisha.

Naomba nije na dondoo kamili za kuleta mada husika ili nieleweke vizuri kati ya KUISHI NA KUDUMU

i) Unakuta mtu ana mwenza wake ni mzuri kila kiungo chake ukionacho kuanzia kichwani mpaka mguuni,na mtu huyo ana mmiliki vizuri tu,lakini unakuta mtu huyo hana imani juu yake,au ana mtesa muda wote ni kulia,kuhisi kunyanyaswa ukiona hivyo huyo si daraja lako hivyo usipende KUISHI,tafuta wa KUDUMU nae ambae hatokupa SHINIKIZO.

ii)Kuna kipindi unakuta una miliki hela nyingi ambazo labda hukutarajia,ama sawa ulitarajia lakini hukuzipangia mkakati wowote ule madhubuti wa jinsi ya kuzitunza vizuri na kufanyia miradi tofauti ili ziongezeke zaidi,ila ndani ya muda mfupi unakuta kwenye 100% ya zile hela umebakisha 20% basi tambua maamuzi yako yalikuwa ni KUISHI na si KUDUMU katika kuziendeleza zile hela.

iii) Kupenda kumiliki vitu vikubwa kwa haraka,kama unajua wewe una penda vitu vizuri kwa haraka na mfanano wake ndugu yangu upo kwenye KUISHI na sio KUDUMU.Jifunze na jipe muda rafiki na wa kutosha kuanza na kitu kidogo ili ukifanye kiwe kikubwa,hii hatua itakusaidia pindi utakapo kuwa na hiko kidogo cha kukiendeleza utapitia hatua tofauti tofauti kwenye kukikuza,utapitia wakati wa kuanguka,utanyanyuka na mia mfanano wake mpaka hiko kitu kikikuwa utakuwa umeimarika kifikra,kiutendaji na mfanano wake.

Kwa mfano:

Unakuta mtu ana tamani kuwa na ghorofa tatu na hela anazo cash ila nyumba hana na amepanga,cha kushauri hapo kwanza jenga nyuma ambayo yatakufanya upumzike pindi uchokapo na pia sehemu tulivu ya kuyapanga jisi ya kuyaendea.

iv) Dada mtengeneze huyo kijana {mpenzi} mwenzio ili awe mume bora wa KUDUMU kuliko kila siku kuji lengesha kwa wanaume wenye hela watakufanya wa KUISHI na wao kuondoka ikiwa labda umeachwa salama ni kukuachia mimba na umlee mtoto asie na baba,ama kukuacha bila mimba matokeo mengine (-) ni kukutoa MASEGA (MARINDA) ama kukuachia magonjwa na mikosi ya balaa.Ipo wazi tunaona madada wanavyopitia hivi

v) Kaka mfanye mke (mpenzi) wako awe bora na mzuri kuliko mke (mpenzi) wa jirani yako,hili vijana wenzangu wa kiume tulizingatie,kama una mmoja ulie jitosa nae kwenye swala zima la KUDUMU basi mfanye awe bora kuliko wa jirani yako,ukishindwa kufanya hivyo na ukawa una mmendea mke(mpenzi) wa jirani yako basi tambua wewe upo kwenye KUISHI na mwisho wa siku jirani yako akisha gundua na akaja kusibitisha kwa basi tambua jamaa lazima a'KUISHI yani hapo kuna kitu jamaa % kubwa lazima akufanyie ili ujute,uumie na mfanano wake,mtunze mkeo ADUMU(KUDUMU).

vi) Wengi walio soma elimu yao HAIDUMU kutengeneza vizazi bora,ila matokeo yake Mtu ana amua KUISHI kutokana na elimu yake,Elimu yako ina DUMU vipi ikiwa unavuta sigara iliyo andikwa ONYO. Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako,tunajua madhara ya sigara, pombe (madawa ya kulevya) ila kwa kuwa tumeamua KUISHI basi tuna ishi kwa kuvitumia hivi vitu kila siku na sio kwamba kuzingatia elimu IDUMU kuwa tahadharisha vizazi vijavyo matokeo yake sisi kuvifakamia kabisa.

WANA JUKWAA SIWEZI ANDIKA VYOTE ILA NAOMBA HIVYO VICHACHE TUVIZINGATIE NA KAMA KUNA VYA KUONGEZEA BASI KARIBUNI.

NDANI NA UANDISHI HUU KAMA KUNA SEHEMU NIMEKOSEA BASI NI SEHEMU YA UPUNGUFU YA BINADAMU, ILA PIA NATAMANI KILICHOKUWA NDANI YA KICHWA CHANGU NIKILETE PAAP HAPA KWENYE HILI JUKWAA ILA NAONA BADO SIJAFIKIA LENGO NAOMBA TUPOKEE HIKI.
 
Wengi walio soma elimu yao HAIDUMU kutengeneza vizazi bora,ila matokeo yake Mtu ana amua KUISHI kutokana na elimu yake,Elimu yako ina DUMU vipi ikiwa unavuta sigara iliyo andikwa ONYO. Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako, tunajua madhara ya sigara, pombe(madawa ya kulevya) ila kwa kuwa tumeamua KUISHI basi tuna ishi kwa kuvitumia hivi vitu kila siku na sio kwamba kuzingatia elimu IDUMU kuwa tahadharisha vizazi vijavyo matokeo yake sisi kuvifakamia kabisa.
 
Back
Top Bottom