Maamuzi haya ya mahakama yananishangaza: sehemu moja Rushwa na nyingine Haki

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Kesi mbili zimenivutia mpaka naziweka jukwaani.
1. kwanza ni kesi iliyokuwa Mahakamani Kisutu ambako kampuni ya simu ya Tigo imeamriwa kuwalipa sh. BIL. 2. wasanii wa bongo fleva AY na MWANA FA kupiga nyimbo zao za 'usije mjini' na 'dakika moja' kama miito ya simu bila idhini yao. Nimejiuliza: wakiuza albam nzima.wanapata pesa hiyo? au wakipanda jukwaani kwa nyimbo mbili wanapata pesa hiyo? nakubali si vzr kutumia kazi ya mtu bila idhini yake ila adhabu ni kubwa mno. hapa nimenusa harufu ya RUSHWA! Tigo wamekata rufaa
2. Pili ni kesi ambayo FASTJET wameamriwa kumlipa wakili wa mahakama kuu sh. MIL. 30 kwa kuahirisha safari bila kumjulisha mapema. wakili aliomba MIL. 50 ila mahakama ikasema ni nyingi mno. hapa naona busara nzuri zaidi na HAKI.
UJUMBE: Tujitahidi tufuate sheria lasivyo itakula kwetu na pia tutende haki kwa kuamuru fidia zinazoendana na uhalisia
 
Nadhani utakua ni layman...kesi ikipelekwa mahakamani mpeleka kesi anakua na maombi yake...i.e. milioni 50, kwaio mpeleka kesi atajitahidi kujuatify kwa nini alipwe pesa hio...wakati huo yule anaedaiwa/kushitakiwa atakua anapinga nwisho wa siku ni utetezi wako ndo utakao kisaidia na hakimu au jaji anaamua nani kamzidi hoja mwenzie...
 
shida iko wapi ktk uzi? nenda moja kwa moja kwenye point
 
Tatizo ni wengi kutokujua haki zetu na gharama za wanasheria na hadaa za wanasheria kwa upande mmoja ndio janga jingine
Ila kuna kesi nyingi mtu ukikomaa zinakutoa
 
kweli mkuu. wengi tumekuwa washamba wa mambo ya sheria
 
Mkuu kuna hii hapa chini nayo kali,ongezea hapo juu(Kuna watu wabishi kweli aisee)
AIFIKISHA MAHAKAMANI BENKI KWA KUKIUKA MAKUBALIANO.
MWANAMKE mmoja mkazi wa mkoani Njombe ameamuakuipandisha mahakamani Benki ya wananchi Njombe Community Bank(Njocoba), kwa madai ya kuuza vitu mbalimbali vya ndani tofauti na mkataba wa mkopo aliokopa katika Benki hiyo.

Ilielezwa mahakamani hapo na wakili wa Mwanamke Jane Mganwa, wakili Hilmar Danda, Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo hakimu John Kapokolo, Kuwa benki hiyo iliuza mali za mwanamke huyo tofauti na mkataba wa mali zilizoku zimeandikwa katika mkatapa wa kupata mkopo.

Akifafanua mkataba mkopaji huyo mahakamani hapo baada ya kuulizwa na wakili Danda, wakili wa Benki hiyo Frank Ngafumika, alisema kuwa mkataba wa mkopaji huyo uliandika vitu vitakavyo chukuliwa kama
kutakuwa na kukiukwa kwa mkataba.

Ngafumika alisema Mkopaji alisaini mkataba wa kuleta shilingi 78,500 kila baada ya wiki moja na kuwa aliweka dhamana ya vitu vya ndani ambavyo ni pamoja na Luninga mbili zenye thamani ya mil 1.2, radio
moja mil.1.5, Kochi 3 zenye thamani ya 900,000, pamoja na chumba cha biashara, chenye thamani ya milioni 2.

Alisema kuwa kwa vitu hivyo Mwanamke Jane alikopa pesa taslimu milioni 3 ambapo ilielezwa kuwa mkopaji aliacha kupeleka fedha hizo katika wiki ya pili ambapo aliendelea hivyo mpaka wiki ya 9, na kuwa alikuwa amevunja mkataba.

Afisa wa mkopo wa mkopo wa Benki hiyo, Felix Kapinga, aliiambia mahakama kuwa baada ya kuona mkopaji hatimizi masharti ya mkopo alifikisha taarifa kw ameneja wa benki, na benki ilichukua hatua ya
kuuza vitu vya mkopaji.

Awali mama huyo aliiambia mahakama kuwa ameamua kuifikisha benki hiyo mahakamani kutokana na kukiuka wakati wa kuuza vitu na kuuza vitu tofauti na vilivyo kuwa vimeandikwa katika mkataba.

Alisema kuwa Benki hiyo ilitumia dalali kuingia nyumbani kwake na kuuza vitu mbalimbali vya ndani mbali na vilivyo kuwa vimeorodheshwa katika mkataba aliouandika yeye na benki hiyo.

Kesi hiyo iliahilishwa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Hakimu Kapogolo na kuendelea Disemba 15 mwaka huo(kama sikosei 2014).

Then 2015(Hukumu)
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoani Njombe imeiamuru benki ya wananchi Njocoba kumlipa shilingi milioni 20,aliyekuwa mteja wao kwa kmuvunja mkataba wa mkopo kama fidia ya usumbufu na kuuza mali zake alizo weka kama dhamana ya mkopo wake.

Mteja huyo Jane Mganwa aliipandesha benki hiyo mahakamani kwa kuvunja mkataba akiwa na lengo la kulipwa fidia na benki hiyo kwa kumfanyia vurugu na kuvunja mkataba walioandikiana wakati anachukua mkopo.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo yenye namba 7/2013 hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi wa makahakama hiyo, John Kapokolo alisema kuwa mdai ambaye alikuwa ni mteja wa benki ya Njocoba katika mkopo alifungua kesi hiyo mwaka 2013 akidai fidia ya kunyanyaswa dhidi ya benki kiasi cha shilingi milioni 50.

Alisema kuwa mahakama hiyo imesikiliza kesi ya ushahidi upande wa mdai na mdaiwa na kuona Jani ana haki ya kulipwa pesa hizo kama fidia ya kufanyuwa unyanyasaji na kuuzwa vitu vyake kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.

Alisema kuwa baada ya Mahakama kujiridhisha imeona mdai atalipwa pesa hizo na kuwa kuanzia siku ya hukumu mdai atatakiwa kulipwa fidia hiyo na kuwa rufaa ya kesi hiyo ipo wazi ndani ya siku 30.
Akisoma maelezo ya kesi hiyo Hakimu Kapokolo alisema kuwa mdai Jane alikopa kutoka katika benki hiyo mwaka 2012 mwezi juni na mkataba ulikuwa unasema anatakiwa kulipa kila wiki pesa na kuwa alilipa kwa muda wa miezi miwili na baada ya hapo alikutanan na Meneja kumuomba kuwa atashindwa kurejesha pesa hizo kwa kuwa alikuwa anauguza baba yake.

Alisema kuwa mdai baada ya kuomba kuto peleka pesa hizo benki ililipo ona pesa za mteja wao hazipelekwi ilitafuta dalali na kwenda kuuza mali zake ambapo inadaiwa kuwa ziliuza luninga, vyombo vya nyumbani, vitanda na vitu mbalimbali ambavyo aliweka kama dhamana ya mkopo ikiwa ni pamoja na sehemu yake ya biashara.

Ukisomwa mkataba wa kuchukua pesa hizo uliowekwa na benki hiyo na hakimu ambao uliwekwa mahakamani hapo kama kielelezo ulikuwa unasema kuwa mdaiwa atatakiwa kuchukuliwa pesa zake ambazo anaweka katika vkikundi chake na kama hazitatosha itatakiwa kuuzwa vitu vyake.

“Mkataba ambao uliwekwa mahakamani hapa kama moja ya ushahidi katika kesi mkataba huo unasema kuwa mkopaji kama atashindwa kulipa atatakiwa kuulizwa na kisha kama atashindwa vitu vyake vitauzwa,” alisema Hakimu Kapokolo.

Mahakama ilitoa ushauri kwa vyama vya mikopo kuto fanya maamuzi ya haraka kwa wakopaji wao na kujua matatizo ya wateja wao kabla ya kuuza vitu vyao.

Aidha mahakama iliona mshitakiwa ambaye ni benki itatakiwa kulipa pesa mdai huyo shilingi milioni 20 kwa lengo la kumfidia kwa fedheha alizozipata, mali zilizouzwa na kuwa baada ya kuuzwa kwa vitu vyake.

duh! hii ni kiboko. wenye nguvu wajifunze kuheshimu haki na mikataba
 
Unajua mkuu kesi kama hizi lazima upate wakili makini na asie na tamaa na anaemuogopa Mungu.

Maana taasisi hizi zikiona kama zinaenda kushindwa,basi zina deal na wakili wako kona.Sasa utaona hapo wakili njaa anavyotapatapa na tamaa.Maana ni wagum sana kukubali kulipa fidia kirahisi kwa namna yoyote ile watafanya figisu figisu.

Maana wanacheza na Wakili wako na Hakim,miaka ya nyuma ilikuwa shida sana na watu wameonewa saana,ila kwa vile sasahivi kuna Takukuru basi kila mmoja anamuogopa mwenzie,maana siku hizi kila mtu akipeleka kesi na akihisi utata basi ana CC takukuru,angalau heshima ya Mahakama imerudi kwa namna moja au nyingine

Nampongeza Sana Wakili Hilmar Danda kwa kumsimamia huyo Mdada kupata haki yake,ni Mawakili wachache sana wenye kuwa na ujasiri wa namna hiyo na hofu ya Mungu
 
ndo maendeleo haya. Mungu atusaidie
 
Back
Top Bottom