Jimmy_Msukuma
Senior Member
- Nov 1, 2018
- 153
- 181
Wanabodi,
Katika mambo aliyojadili jana Mh. Rais Magufuli ni kwamba, alikiri kuwa Wananchi wanahitaji Katiba mpya, akasema hilo kwasasa sio kipaumbele chake na hatotoa Fedha ili watu wakalale Bungeni.
Kauli hii ina mambo 4:
1. Anakiri kwamba wananchi waliompa Urais wanahitaji Katiba Mpya
2. Maamuzi ya Mchakato wa Katiba Mpya ni yake
3. Pesa anatoa yeye.
4. Hatotoa kwasababu Wabunge hulala (hawafanyi kinachowapeleka Bungeni).
Namba 2 kwakweli sio kweli, maamumuzi ua Mchakato wa Katiba Mpya ni ya Wananchi, Rais ajue anatumikia Wananchi. Namba 3 sio kweli kwamba Pesa za kuendesha mchakato anatoa yeye, Pesa ni kodi za wananchi, hivyo Pesa ni za wananchi wenyewe, yeye ana dhamana tu. Namba 4, kwakweli Rais ameridharau Bunge kwa kupuuza shughuli za wabunge, kwamba muda mwingi wanautumia kulala etc, hivyo hatotoa mwanya huo. Mbona vikao na mambo mengine Bunge hutengewa pesa? Je, wakati wa mchakato uliopita Wabunge walilala?
Hadi sasa nashindwa nimpe hadhi gani Mh. Rais Magufuli: Je, amelewa madaraka? Je, yupo juu ya mihimili mingine? Je, ni kweli hakuna walezi wengine wa Taifa zaidi yake, hadi atoe toe kauli waziwazi za kuashiria yeye ndio mwenye kauli ya mwisho?
Nawasilisha.