Maalumu kwa wakulima wa vitunguu na wanaotaka kuanza kilimo cha vitunguu

baraka607

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
845
195
Habari ndugu zangu,

Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.

Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.

Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com

Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.
 
Attachments

  • IMG-20130718-00032.jpg
    File size
    1.9 MB
    Views
    449

cha'

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
466
195
Mkuu,
shukran kwa taarifa, na moyo wako wa kujitojea. Mi mgeni kwenye taaluma hii, nitakusumbua sana kuhitaji taarifa na mbegu. Ninapo taraji kuelekea msimu unaanza jun/july. Unapatikana wapi, na ningependa fahamu kama kuna sehemu kuna misimu zaidi ya moja.
 
Mkuu naomba nipigie simu ili nikupatie maelekezo vizur. Niko dar
 
Nov 13, 2013
35
0
Tahadhari bei ya kitunguu haipo fixed sokoni inategemea na msimu nadhani bwana mkubwa ametoa hiyo bei ya 130,000/= elikuvutia watu wanunuwe mbegu yake hiyo. Piya kilimo cha vitungu kina gharama sana hususani kwenye mbolea na madawa. Unaweza kutumia hadi milioni 4 kwa heka halafu ukavuna gunia 60 hadi 80 na ukakutana na bei ya sh 30,000/= nimeshawahi kulima vitunguu nilipovuna bei ya vitunguu ikawa hairudishi hata gharama nilizotumia kulima ikabidi ni hifadhi kwa muda eli bei ipande nilipoweka store nikawa napata kazi ya kuanika na kutoa vilivyoharibika 30% viliharibika store.
 
Kaka ingekua ivo basi ningeshakua nimehama mjini. Makosa ulofanya wewe yasiwanyime fursa ya mafanikio wenzako. Ndo mana nikakwambia mwanzo wa bandiko langu, utanufaika endapo utafuata maelekezo ya mtaalamu. Kwa maelezo yako tu inaonyesha dhahili hukuwa unauelewa na kitu unachofanya.
 
baraka607

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
845
195
Na hizo lazima zilikua gunia mbili. Kwasababu ungezalisha tons za kutosha usingekua na uwezo wa kuwa unaanika na kuanua. Uhifadhi wa vitunguu unafanyika kwenye chanja lililojengwa maalum kwa shughuli hiyo na huwa limejengwa kwa matete ili liwe na uwezo wa kupitisha hewa na sio sebelen wala kibarazan kwako.
 
baraka607

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
845
195
Tahadhari bei ya kitunguu haipo fixed sokoni inategemea na msimu nadhani bwana mkubwa ametoa hiyo bei ya 130,000/= elikuvutia watu wanunuwe mbegu yake hiyo. Piya kilimo cha vitungu kina gharama sana hususani kwenye mbolea na madawa. Unaweza kutumia hadi milioni 4 kwa heka halafu ukavuna gunia 60 hadi 80 na ukakutana na bei ya sh 30,000/= nimeshawahi kulima vitunguu nilipovuna bei ya vitunguu ikawa hairudishi hata gharama nilizotumia kulima ikabidi ni hifadhi kwa muda eli bei ipande nilipoweka store nikawa napata kazi ya kuanika na kutoa vilivyoharibika 30% viliharibika store.

Nna ushahidi wa risiti za mauzo kutoka sokoni, kama kuna gunia nilishauza chini ya elfu 85 toka nimeanza biashara basi ntafuta tangazo langu.
 
Nov 13, 2013
35
0
Mkuu kuwa mkweli piya tuwe tunamuogopa mungu, ukiendeleya kudanganya nitaweka contact za watu walio mashambani muda huu maeneo ya ruaha mbuyuni, mang'ola karatu na singida mimi mwenyewe nimelima vitunguu mang'ola na ruaha mbuyuni. Piya hiyo bei ya 600,000/= kwa debe moja ni kubwa sana. Wadau kabla ya kulima vitunguu ni vizuri ukatembelea hayo maeneo unayotarajia kulima eli upate full information kuliko kusikia tuu humu jf
 
Nov 13, 2013
35
0
Ukiwa na muda nenda kaangalia mang'ola watu wana anika mpaka gunia 2000, mtu kama awake anavuna gunia 10000/= na bado ana anika. Hakuna bei ya mbegu ya vitunguu inayofika 600'000/= kwa lita 20. Huo ni wezi bei ya mbegu inajulikana acha kuibia watu, wewe unaponekana kama tapeli
 
mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,495
1,225
ndugu usiwaingize chaka watu,...bei ya mbegu ya kitunguu lita moja nikati ya 10,000 na 15000 pekee na heka moja inatosha lita saba.

kwa wale wa ruaha mbuyuni kuna wazee kule idodomya wanasifika kwa kuandaa mbegu nzuri huu ndio muda wa kukamata bodaboda from mbuyuni ukainunue............

biashara ya kitunguu kwa mwaka huu ilikua balaa tupu...binafsi nilitoa kitunguu cha kwanza na niliuza gunia 65,000 mwez wa saba....bei haikufika hata laki japo nakiri kuna wakat inapanda sana.....kitunguu ni bahat na sibu na mtu ambaye anasimamia kwa remot controo simshauri ata chembe akatie milion zake pale utaishia kula hasara mazima......
 
mtz one

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
4,195
2,000
Habari ndugu zangu,

Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.

Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.

Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com

Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.
kula like mkuu vijana wajifunze ujasiriamali sio kukaa vijiweni kulalamikia serikali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom