Maalim Seif: Zanzibar iwe na Benki Kuu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif: Zanzibar iwe na Benki Kuu yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Dec 26, 2011.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.

  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.
  Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.

  Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar.
  "Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwiano huo ni mbaya katika suala la utoaji vipaumbele kwa maendeleo ya visiwani," alisema Maalim Seif.

  Alisema umuhimu kwa Zanzibar kuwa na benki kuu yake sio jambo jipya, kwani hata awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweka wazi madai ya aina hiyo ikitaka kila upande uwe na mambo yake katika masuala ya kibalozi, shughuli za polisi, uraia na sarafu.

  Alisema wakati wa kutoa maoni juu ya Katiba mpya, pamoja na kudai haki ya kuwa na benki kuu, wananchi waungane ili maoni yao yaweze kusaidia upatikanaji wa katiba itakayoondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.
  Maalim Seif alisema ukosefu wa umoja miongoni mwa wananchi katika suala la kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Katiba mpya ni hatari kwa utaifa wao.

  "Utakapofika wakati wa kutoa maoni tusahau itikadi zetu, tuungane kulinda maslahi ya Zanzibar, vyama vya siasa ni taasisi za kupita, ASP haipo, Tanu haipo na ZNP haipo, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo," alisema.

  Maalim Seif pia alisisitiza msimamo wa kutaka Katiba mpya itakayoundwa iweke utaratibu unaoruhusu mzunguko wa madaraka ya nafasi ya rais wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.

  "Mwandishi mmoja wa habari juzi alitaka nieleze maslahi ya Zanzibar ninayowahimiza wananchi kudai yawekwe ndani ya Katiba mpya, nikamwambia mfumo wa sasa wa uchaguzi umesbabisha nafasi ya rais wa muungano kubaki bara kwa muda mrefu," alisema Maalim Seif akiwa anarejea jibu alilotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari baaya kuulizwa swali hilo na Muhibu Said, Mwandishi wa habari mwandamizi wa NIPASHE.

  Akifafanua zaidi haja ya kuwepo utaratibu wa kikatiba unaoruhusu nafasi hiyo kutolewa kwa mzunguko, Maalim Seif alisema chini ya mfumo wa uchaguzi uliopo Zanzibar imeshika nafasi hiyo kwa miaka 10 tu wakati Tanzania bara imehodhi wadhifa huo kwa miaka 35.
  Alisema hiyo ni kasoro katika uendeshaji wa serikali ya muungano iliyoundwa na mataifa mawili ambayo ni nchi.
   
 2. Katambala

  Katambala Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  tutengane tu ndiyo jawabu
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mi nashauri muungano uvunjwe kila mtu akamate ustaarab wake mana longolongo zimekua nyingi mno
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Napata tabu sasa: Hiyo ni Kauli ya CUF kupitia Katibu wake Mkuu au ni Kauli ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Makamo wake wa Kwanza wa Rais?
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Serikali tatu, moja au kuvunja muungano ndio solution ya hizi chokochoko
   
 6. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hivi kwa sentiments hizi zinazotoka kwa mmoja wa viongozi wakuu wa SMZ bado kuna muungano kweli? nahisi muda wa kugawana mbao umefika sasa... halafu naona huyu bwana amechukua suala ya maslahi ya ZNZ ndani ya muungano kama agenda yake .... is this a calculated move kuonyesha kwamba yeye ndiye kiongozi pekee anayeweza kuwatetea wazanzibari?
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja yake ila sababu alizotoa hazina mashiko kabisaaaa. Nahili litimia tu muungano ndiyo basi ila alichelewa wangeingiza kwenye katiba yao mbona mambo mengi wameyafanya/ kuyaingiza kwenye katiba yao pasipo kuuliza upande wa pili na hili walipeleke kwenye bunge lao aka Baraza la Wawakilishi watafanikiwa tu kuwa na benki Maana wao wapo juu

  eg ...Ila akumbuke kuwa BoT wanakwenda watendaji na si eti kwa Sababu ya Uzanzabar tu
   
 8. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by zenjiboy // 26/12/2011 // Habari // 4 Comments

  Na Charles Mwankenja
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.
  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.
  Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.
  Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar.
  “Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwiano huo ni mbaya katika suala la utoaji vipaumbele kwa maendeleo ya visiwani,” alisema Maalim Seif.
  Alisema umuhimu kwa Zanzibar kuwa na benki kuu yake sio jambo jipya, kwani hata awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweka wazi madai ya aina hiyo ikitaka kila upande uwe na mambo yake katika masuala ya kibalozi, shughuli za polisi, uraia na sarafu.
  Alisema wakati wa kutoa maoni juu ya Katiba mpya, pamoja na kudai haki ya kuwa na benki kuu, wananchi waungane ili maoni yao yaweze kusaidia upatikanaji wa katiba itakayoondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.
  Maalim Seif alisema ukosefu wa umoja miongoni mwa wananchi katika suala la kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Katiba mpya ni hatari kwa utaifa wao.
  “Utakapofika wakati wa kutoa maoni tusahau itikadi zetu, tuungane kulinda maslahi ya Zanzibar, vyama vya siasa ni taasisi za kupita, ASP haipo, Tanu haipo na ZNP haipo, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo,” alisema.
  Maalim Seif pia alisisitiza msimamo wa kutaka Katiba mpya itakayoundwa iweke utaratibu unaoruhusu mzunguko wa madaraka ya nafasi ya rais wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika.
  “Mwandishi mmoja wa habari juzi alitaka nieleze maslahi ya Zanzibar ninayowahimiza wananchi kudai yawekwe ndani ya Katiba mpya, nikamwambia mfumo wa sasa wa uchaguzi umesbabisha nafasi ya rais wa muungano kubaki bara kwa muda mrefu,” alisema Maalim Seif akiwa anarejea jibu alilotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari baaya kuulizwa swali hilo na Muhibu Said, Mwandishi wa habari mwandamizi wa NIPASHE.
  Akifafanua zaidi haja ya kuwepo utaratibu wa kikatiba unaoruhusu nafasi hiyo kutolewa kwa mzunguko, Maalim Seif alisema chini ya mfumo wa uchaguzi uliopo Zanzibar imeshika nafasi hiyo kwa miaka 10 tu wakati Tanzania bara imehodhi wadhifa huo kwa miaka 35.
  Alisema hiyo ni kasoro katika uendeshaji wa serikali ya muungano iliyoundwa na mataifa mawili ambayo ni nchi.
   

  Attached Files:

 9. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mi nadhani muungano ni ni muhimu na ni jambo jema.
  Kwa maana tukivunja muungano tutalazimika pia kutangua au kufuta baadhi ya tunu na semi muhimu za kiswahili kama vile "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu"
  sidhani kama anaweza kutokea mtu(mimi siwezi) anayeweza kusema usemi huu ni makosa na umekuwa ukifundishwa kimakosa!

  Tupambane kuwepo na serkali tatu ili kuulinda umoja wetu.
  Serikali mbili ni kwa manufaa ya wanasiasa pekee, bali serikali tatu ni kwa manufaa ya wote wakiwamo wanasiasa.

  Marais watatu, mabunge matatu, ikulu tatu, jeshi moja, polisi mbili, uhamiaji moja.
  Nk nk nk.

  Shida ni nini?
   
 10. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Naomba Maalim Seif anijulishe TANZANIA BARA ni nchi gani hiyo katika ramani ya dunia?Pili inakuwaje anapozungumzia Zanzibar huwa hasemi TANZANIA VISIWANI huzungumzia Zanzibar? Tatu mbona anazungumzia sana AUTONOMY ya Zanzibar lakini kinamshinda nini kusema tuachane na kila moja aendelee na mambo yake. Nijibu Maalim Seif au waambie wapambe wako wanipe majibu tafadhali.
   
 11. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Wanao jihisi wamepoteza na kujuta niupande gani katika kitandawili hishi cha Muungano nashindwa kufahamu? kungekuwepo na Tanganyika nazani mambo mingi yangekuwa fair ktk Muungano, lakini chakuchangaza nikuwa mchirikika moja wa mungano kaji-suiceed mwenyewe halafu anajilaumu kuwa alitaka kufa na mwenzake. kwa nini Zanzibar bado ipo na hadhi yake yote ya kuwa nchi.

  Kifo cha Tanganyika nichakujitakia akili nyingi mbele kiza, mulitegemea muiuwe Tanganyika ili kuizibiti Zanzibar lakini nia safi hairogwi.
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Namfananisha Maalim Seif na kipaza sauti cha Msikiti. Yani tangu aingie kwenye 'SUK' hakuna anachokifanya zaidi ya uropokaji tu!
   
 13. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Kwa hili nakupinga ndugu. Solution ni kuwa na serikali moja tu. Vinginevyo ni kuongeza gharama za kuendesha hizo serikali na bado misuguano baina ya hizo serikali itatokea. Kila moja itataka ionekane Babu Kubwa zaidi ya Mwenzake. After all tunao mfano mzuri wa United States of America (USA). Zimeungana nchi zaidi ya 40. Je unaskia habari za serikali 40 na ya Muungano? Tusijidanganye! Miungano iliyodumu na yenye tija ni ile ya serikali moja tu!

   
 14. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata mimi nimeona. Huu sasa ni uchizi, yani atoke mtu kisiwani aje atawale bara kisa kupeana nafasi. Mbona urais wao hatubadilishani?! Hawa ni kuwapoteza tu
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  waambie magamba wakati wa malipo pale LUMUMBA
   
 16. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,141
  Likes Received: 3,330
  Trophy Points: 280
  hiyo ni kweli kabisa,
   
 17. s

  sitakuwafisadi Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jiulize maswali haya kisha utajua HAKUNA MUUNGANO nichanga la macho!!.........ALIE ONGOZA mapinduzi ya ZANZIBAR ni ...................[FONT=&quot][/FONT]field marshal............JOHN TITO OKELO.............je?... ALISAINI HATI YA MUUNGANO wa tanganyika na zanzibar ....JOHN TITO OKELO.[FONT=&quot][/FONT]...... clip_image002.jpg clip_image002.jpg kwanini hakuongoza tena serekali ya MAPINDUZI YA ZANZIBAR BAADA YA MUUNGANO NA TANGANYIKA ......................field marshal............JOHN TITO OKELO....mwenye kabutura katikati!!.
   
 18. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nitamuunga mkono aizungumzia kuuvunja kabisa huu Muungano ili Zanzibar anayoitaka iwe na vyote hivyo kwa uhuru zaidi, ni wakati sasa wananchi waamue kama wanautaka huu Muungano au tuachane kwa amani..
   
 19. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  I am a great admirer of the late Mwalimu Nyerere. Many people (Tanganyikans) of my age know fully well that without his policies of fair play and opportunities for all many of us would probably be out there in the interior and not writing in Jamii Forums like I am doing right now. But for KILLING our Tanganyika there I draw the line. I would say exactly this were Mwalimu to re incarnate and somehow we met.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mna hadhi gani kama mna hadhi mbona mnalalamika kiivyo tena mnayemlalamikia wenyewe mnasema kishajifia je angekuwa mzima ingekuwaje. Nyie mlie tu na tutalazimisha serikali moja ili zanzibar iwe mkoa kama katavi.
   
Loading...