Maalim Seif: Tumepokea barua kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na tunaifanyia kazi

Itakuwa ni aibu kubwa kwa Maalim na ACT kukubali kuingia kwenye hiyo Serikali dhalimu.

Ni mtego mkubwa kwa Maalim na kwa ACT. Wakikubali tu, wapewe Wizara ya Mambo ya Ndani ili wafanye kazi ya kukanusha kuwa hakuna raia aliyeuawa na Polisi wakati wa uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu mfumo wa vyama vingi uanze, Awami zote, uchaguzi uliofanyika 2015 haukuwa na figisu. Unajua kwanini? Ulikuwa wa huru na uwazi. Yaani wakala akitia sign tu form ya matoeo apo apo imerushwa makao makuu. 2015 CCM ilijiona imeishiwa pumzi, na hii yote ni kwa sababu Maalim alikuwe ndani ya serikali. Kwa mara ya kwanza wazanzibari waliweza kupiga kura kwa amani, uhuru na haki na kila kitu kuwekwa wazi. Nitajie uchaguzi mmoja tu ambao Maalim hakuwemo serikali halafu ukawa wa amani, huru na haki. Hata Maalim Seif anajua 2015 uchaguzi ulikuwa upo sawa. Ila CCM walikuwa na mbinu yao tayari, kuufuta uchaguzi na kuurudia na kutumia Jeshi kusimamia (ambalo loyalty yake inajulikana iko wapi) lakini wakakuta kuwa Maalim hakutaka kurudia na ndio wakafnya kikawaida bila kutumia nguvu za jeshi.

Uchaguzi ule hakukuw na wizi maana Maalim alikuwa na power. Tizama alivoacha serikali sasa, CCm wamerudia kuiba tena kwa waziwazi na wala hawaogopi.
Inawezekana dhana yako ni kweli, mkuu! Lakini pia, awamu hii, tukubaliane kuna mambo mazito yamefanyika bila aibu kabisa! Naunga mkono kabisa Maalimu kuingia mle, na hata wanawake wa CHADEMA, nafikiri ni muhimu wakaingia hivyo hivyo, hata kama kulikua na kuminywa haki!
 
Inawezekana dhana yako ni kweli, mkuu! Lakini pia, awamu hii, tukubaliane kuna mambo mazito yamefanyika bila aibu kabisa! Naunga mkono kabisa Maalimu kuingia mle, na hata wanawake wa CHADEMA, nafikiri ni muhimu wakaingia hivyo hivyo, hata kama kulikua na kuminywa haki!
Awamu hii wametia fora kwenye figisu zao. Mimi binafsi sikuwa nikijali hizi siasa, nilijua zamani kuwa Maalim hawampi ata vipi, wao wenyewe wanajisifia kuwa anashinda lakini hawampi. Yaani ni kama wamekula kiapo. Kilichoniudhi mara hii, ni jinsi walivoiba. Yaani Pemba walivokuwa hawana haya wamejipa majimbo yote? Pemba hii tunayoijua hasa? Yaani Pemba mpaka dunia itamaliza mda wake basi CCM hawapati kitu kule. Au mfano Jimbo la Malindi eti wamelichukua wao!

Cha msingi saivi Maalim akubali kuingia serikalini akiwa na masharti yake, nimeona ameweka la tume huru. Wakikubali basi aingie tu hamna namna na awe na lengo la kuhakikisha 2025 watu wana amani na wanachagua wamtakae. Japo najua kuwa CCM watakuja tu na mbinu nyengine, lakini ikibidi urudiwe, maalim asisuse, ale nao sahani moja.
 
Maalim akiingia kwenye serikali hiyo ya dhulma siyo tu kwamba atakuwa amewasaliti Wazanzibari bali atakuwa amesurrender kwa wanyang'anyi.

Atawasaidia kuwapa CCM legitimacy wasiyoistahili, na atakwamisha jitihada ya kufanyika kwa reforms za msingi nchini za kikatiba za upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi na hata katiba mpya

Atawasafisha wauaji waliovamia Zanzibar kuteka na kupora maamuzi ya Wazanzibar dhidi ya dhambi yao ya kuua, kupiga na kutesa wananchi wa Zanzibar wasio na hatia.

Na kibaya zaidi ACT ikiingia katika serikali hii itaipa serikali ya muungano life Support ya kidiplomasia ambayo inaihitaji sana baada ya dunia kuinyooshea kidole kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Nawaomba wana za ACT, kikubwa na cha msingi siyo kugawana vyeo bali ni reforms za msingi. Tupambane tupate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, Kama mkijiunga kwenye serikali haranu ya Zanzibar, mtakosa moral authority ya kudai haya mambo kwa nguvu zote kwa sababu na nyie mtakuwa sehemu ya serikali.

Kumpa Maalim umakamu ni kumpoza yeye lakini hakuna manufaa ya maana kwa wananchi wa Zanzibar.

Maalimu kumbuka, hawa wanaotaka kukupa cheo ndiyo haohao waliokufanyia hila kukutoa kwenye CUF. Sasa leo hii uzuri wako kwao umetokea wapi?

ACT, Achaneni na hizi nafasi mlizorushiwa chambo!., Mkihalalisha haya mtakuwa mmeunga mkono udhalimu na nyie mtakuwa sehemu ya udhalimu, Sisi Wananchi tutawadharau na kuwapuuza!

Hivi leo eti maalimu apate kura 19% si ushenzi huo na matusi yaliyoje?

Maalim akikubali kukalia hiyo nafasi wakati wamemfanyia hiyana nzito na kumdhalilisha, Wazanzibar waramuondolea heshima kubwa sana wwliyompa. Ni bora akastaafu kwa heshima akaacha legacy ya kutukuka ya kupigania maslahi ya Wazanzibar badala ya kustaafu huku wakiwa wamemtukana kwa kumpa cheo ambacho wao CCM wwnajua ukweli kuwa alistahili kuwa zaidi ya hapo!.
Umechelewa kumpa ushauri
 
Madam Mazrui wamemuachia hakuna haja tena kushirikiana na madhalim, wapinzani jipangeni upya kule bara Chadema nayo ilibugi sana kumteuwa Tundu Lissu kugombea urais, Lissu amekuwa na hofu kuliko mtu yeyote yule bado hajaiva kwenye siasa yeye ni kiongozi wa upinzani alikuwa mgombea urais lakin jambo dogo limemtoa kwenye mstari, Bobi Wine ameshikwa muda huu na unafkiri akitoka atakimbia nchi no ataendelea kusalia Uganda na kumtibua zaidi na zaidi M7.

Na madam Bobi ni kiongozi wa upinzani ata iweje M7 hana ubavu wa kumpiga risasi pamoja na udikteta wake wote ule, Tundu Lissu amepata simu basi brek ya kwanza ni ubalozi wa Ujerumani
Hahahaaaa nimecheka hyio sentence ya mwisho
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar sasa limebakia kwa ACT-Wazalendo baada ya Rais Hussein Mwinyi kukiandikia barua ya kutaka jina la Makamu wa Kwanza wa Rais na kutentenga nafasi mbili za uwaziri kwa chama hicho.

Wakati ukweli ukiwa huo, mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye aliwania urais Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 amesema bado wanatafakari kuhusu suala hilo.

Awali ACT ilikataa kutambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu huo kikidai kuchezewa rafu, lakini Maalim Seif alipata zaidi ya asilimia 10 za kura zinazokipa chama hicho nafasi ya kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kwa mujibu wa katiba.

Jana, Rais wa Awamu ya Nane, Dk Mwinyi aliwaambia waandishi wa habari wakati wa kutangaza baraza la mawaziri kuwa ametimiza utashi wa kikatiba wa kukiandikia chama kilichopata kura zinazotakiwa ili kitoe jina la mtu atakayeshika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na ameacha nafasi mbili za uwaziri kwa ajili ya chama hicho.

“Tumepokea barua kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na tunaifanyia kazi,” alisema Maalim Seif jana.

Alipoulizwa kama wapo tayari kushiriki kuunda SUK, Maalim Seif alisema bado wanatafakari.

“Chama hakijafanya uamuzi, kiko katika hatua ya mashauriano. Pia chama kipo katika hatua ya mashauriano kuhusu waliopewa ubunge, uwakilishi na udiwani kwenda kula kiapo au la,” alisema Maalim Seif.

Alipoulizwa kama atakubali ikiwa atateuliwa kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif alisema: “Nitaheshimu maamuzi ya chama.”

ACT-Wazalendo imepata wawakilishi wanne, lakini wamebakia watatu baada ya mwakilishi mteule wa Pandani, Abubakar Khamis Bakary kufariki dunia hivi karibuni.

Katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya mwaka 2010-15 iliyongozwa na Dk Ali Mohamed Shein akiwa Rais, Maalim Seif alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya chama chake cha zamani chas CUF kupata zaidi ya asilimia 10 za kura.

Pia chama hicho kiliongoza Wizara ya Afya iliyokuwa chini ya Juma Duni Haji, Biashara na Viwanda (Nassor Mazrui), Elimu (Zahra Hamad) na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Fatma Ferej).

Hata hivyo, umoja huo ulianza kulegalega mwishoni mwa muhula huo na hali ikawa mbaya zaidi baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Rais na wawakilishi kufutwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), iliyoamuru urudiwe na hivyo CUF kuususia.

Kutokana na CUF kuususia, hakuna chama cha upinzani kilichopata zaidi ya asilimia 10 ya kura za urais na hivyo Dk Shein kulazimika kuendeshas serikali bila ya Makamu wa Kwanza wa Rais, huku akimteua Hamad Rashid Mohamed wa ADC kuwa Waziri wa Kilimo na baadaye akawa Waziri wa Afya.

Mwingine ni Said Soud Said wa chama cha AAFP, aliyekuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Yafaa watafakari kweli kweli kwani tuliyoyaona ni ya kisayansi zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom