Je, ni kweli kuwa katiba iliyopo haijatamka kuwa chama tawala kitaisimamia serikali?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,271
2,024
Pascal Mayalla ambaye ni mwanasheria wa kujitolea wa ccm atueleweshe
Mkuu Erythrocyte , kwanza asante kuni tag.
Ni kweli mimi ni mwanasheria wa kujitolea kutetea haki za binadamu ikiwemo haki katiba, na sio mwanasheria wa kujitegemea wa CCM!.
Wadau nimejaribu kuipitia KATIBA iliyopo ili kupata Kifungu kinachokipa Mamlaka CHAMA TAWALA kuisimamia SERIKALI lakini sijakiona.Ombi kwa Wanasheria wetu.

Je, ni kifungu gani kinachokipa Mamlaka CHAMA TAWALA kuisimamia SERIKALI? Tumeambiwa Tusome kwanza KATIBA iliyopo kabla ya Kupatiwa KATIBA MPYA

Pia soma: Mkutano wa 3 kuenzi Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 26, 2023 - Zanzibar
Mkuu Mzee wa Twitter, kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, chombo pekee chenye jukumu la kuisimamia serikali yetu ni Bunge la JMT!.

Serikali inayosimamiwa ni serikali iliyoingia madarakani baada ya kunadi ilani yake ya uchaguzi.

Hivyo chama kinawajibu wa kufuatia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
na sio kuisimamia serikali!.

Kupitia dhulma fulani kubwa, serikali ya CCM imechomekea ubatili fulani ndani ya katiba yetu ambao ndio umeotesha mapembe kwa CCM na Mwenezi mpya wa CCM anayatumia mapembe hayo kuwachoma waserikali.
P
 
Mfano umeahidi maji, elimu bure, umeme, SGR, bima ya afya kwa wote, uwajibikaji, kutokomeza rushwa, ufisadi, wizi, uonevu.

Chama chenu mhakikisha vipi ilani yenu inatekelezwa kwa wakati bila chenga?

Unafuatiliaje kama ilani mliyoinadi inatekelezwa, mbinu gani, mikakati gani? Majukwaa, mikutano gani? watumie Kuhakikisha utekelezaji wa ilani na kusikiliza changamoto za wananchi?

Serikali ikishindwa kutekeleza ilani ya chama, chama kinahakikisha vipi serikali inarudi kwenye mstari.
 
Mkuu Erythrocyte , kwanza asante kuni tag.
Ni kweli mimi ni mwanasheria wa kujitolea kutetea haki za binadamu ikiwemo haki katiba, na sio mwanasheria wa kujitegemea wa CCM!.
Mkuu Mzee wa Twitter, kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, chombo pekee chenye jukumu la kuisimamia serikali yetu ni Bunge la JMT!.

Serikali inayosimamiwa ni serikali iliyoingia madarakani baada ya kunadi ilani yake ya uchaguzi.

Hivyo chama kinawajibu wa kufuatia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
na sio kuisimamia serikali!.

Kupitia dhulma fulani kubwa, serikali ya CCM imechomekea ubatili fulani ndani ya katiba yetu ambao ndio umeotesha mapembe kwa CCM na Mwenezi mpya wa CCM anayatumia mapembe hayo kuwachoma waserikali.
P
Serikali inayowekwa imetokana na chama kwa kuwa ili ugombee kwa mujibu wa katiba ya sasa lazima upitie kwenye chama fulani. Hatujawa bado na mgombea binafsi.
Nadhani hili ni suala la kupigania. Ama sivyo bado serikali itasimamiwa na chama husika kilichowateuwa wanachama wake kugombea.

Na ndio maana baadhi ya vyama vya upinzani huwaagiza wawakilishi wake kugomea jambo fulani na endapo watakiuka wanaweza kufutwa uanachama! Chama kina nguvu juu ya serikali!
 
Hii inaweza kuwa kama ile ya kesi ikiwa mahakamani haitakiwi kujadiliwa
 
Wadau nimejaribu kuipitia KATIBA iliyopo ili kupata Kifungu kinachokipa Mamlaka CHAMA TAWALA kuisimamia SERIKALI lakini sijakiona.Ombi kwa Wanasheria wetu.

Je, ni kifungu gani kinachokipa Mamlaka CHAMA TAWALA kuisimamia SERIKALI? Tumeambiwa Tusome kwanza KATIBA iliyopo kabla ya Kupatiwa KATIBA MPYA

Pia soma: Mkutano wa 3 kuenzi Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 26, 2023 - Zanzibar

Chama tawala kinaunda serikali na si kusimamia serikali. Labda kusema kuwasimamia watu wao wanaoteuliwa kuunda serikali.
 
Serikali inayowekwa imetokana na chama kwa kuwa ili ugombee kwa mujibu wa katiba ya sasa lazima upitie kwenye chama fulani. Hatujawa bado na mgombea binafsi. Nadhani ili ni suala la kupigania. Ama sivyo bado serikali itasimamiwa na chama husika kilichowateuwa wanachama wake kugombea.
Mkuu bado hujajibu ni kifungu gani cha Katiba kinasema Chama Tawala kitaisimamia serikali?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Serikali inayowekwa imetokana na chama kwa kuwa ili ugombee kwa mujibu wa katiba ya sasa lazima upitie kwenye chama fulani. Hatujawa bado na mgombea binafsi.
Nadhani hili ni suala la kupigania. Ama sivyo bado serikali itasimamiwa na chama husika kilichowateuwa wanachama wake kugombea.

Na ndio maana baadhi ya vyama vya upinzani huwaagiza wawakilishi wake kugomea jambo fulani na endapo watakiuka wanaweza kufutwa uanachama! Chama kina nguvu juu ya serikali!
Kifungu gani cha katiba?
Watu wanataka rejea ya Kifungu cha katiba!
 
Mkuu bado hujajibu ni kifungu gani cha Katiba kinasema Chama Tawala kitaisimamia serikali?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Katiba imegeneralise mambo. Na ndio maana kuna kanuni ndogondogo zinazotokana na katiba.
Kwa kuteuliwa na chama kugombea nafasi ya kiserikali ni sawa na mzazi kumpeleka mtoto wake shule; ni lazima aletee taarifa ya matokeo kwa mzazi/mlezi!
 
Mkuu Erythrocyte , kwanza asante kuni tag.
Ni kweli mimi ni mwanasheria wa kujitolea kutetea haki za binadamu ikiwemo haki katiba, na sio mwanasheria wa kujitegemea wa CCM!.
Mkuu Mzee wa Twitter, kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, chombo pekee chenye jukumu la kuisimamia serikali yetu ni Bunge la JMT!.

Serikali inayosimamiwa ni serikali iliyoingia madarakani baada ya kunadi ilani yake ya uchaguzi.

Hivyo chama kinawajibu wa kufuatia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
na sio kuisimamia serikali!.

Kupitia dhulma fulani kubwa, serikali ya CCM imechomekea ubatili fulani ndani ya katiba yetu ambao ndio umeotesha mapembe kwa CCM na Mwenezi mpya wa CCM anayatumia mapembe hayo kuwachoma waserikali.
P
Mkuu mbona umemalizia kwa ukali sana? 😒Majukumu ya mwenezi wa chama kwa serikali inayoongozwa na chama chake hayako kwenye katiba. Hii ni nchi ya vyama vingi. Mwenezi anajituma tu kichama kwa serikali iliyotokana na chama chake ila ingekuwa ADC ndio wako madarakani isingekuwa hivyo.
 
Suala sio Kauli suala ni kifungu ktk KATIBA MKUU

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Mkuu siyo kila kitu kimeandikwa kwenye katiba;yaani ni sawa kuhoji pindi Rais anapokuwa usingizini usiku wa manane,nani huwa anaongoza nchi, obviously,ata kama haijaandikwa ni vyombo vya usalama ndiyo vinaongoza kwasababu vipo macho muda wote.
Kwa lugha nyingine kuna nadharia kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS ni kama Rais kivuli wa nchi.
Vilevile kwa chama,katiba inatamka kuwa mtu hawezi kugombea nafasi ya kisiasa bila kupitia chama cha siasa,sasa kama wewe umepewa madaraka kupitia Ilani ya chama,kwanini chama kisisimamie serikali kwa kufuatilia utekelezaji wa ilani yake?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Katiba imegeneralise mambo. Na ndio maana kuna kanuni ndogondogo zinazotokana na katiba.
Kwa kuteuliwa na chama kugombea nafasi ya kiserikali ni sawa na mzazi kumpeleka mtoto wake shule; ni lazima aletee taarifa ya matokeo kwa mzazi/mlezi!
Acha kuruka ruka Kama hakuna Kifungu sema ila sio eti Katiba imegeneralize mambo na Kama ni kanuni nayo ni ipi?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona umemalizia kwa ukali sana? 😒Majukumu ya mwenezi wa chama kwa serikali inayoongozwa na chama chake hayako kwenye katiba. Hii ni nchi ya vyama vingi. Mwenezi anajituma tu kichama kwa serikali iliyotokana na chama chake ila ingekuwa ADC ndio wako madarakani isingekuwa hivyo.
CCM ndio wenye ilani, serikali ndie mtekelezaji ilani, Bunge ndie msimamizi wa serikali, Mwenezi ana haki ya kufuatilia utekelezaji wa ilani, na kumuuliza yeyote kuhusu utekelezaji ilani.

Ilani inaitwaje kwa Kingereza?
 
Back
Top Bottom