G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,704
- 36,456
Hatimaye Maalim Seif Sharif Hamad amevunja ukimya kuwa lengo lake ni kumng'oa Dr. Ali Mohamed Shein mapema iwezekanavyo. Maalim anadai kuwa wiki ijayo ataanza rasmi harakati za nguvu kumng'oa kiongozi huyo wa Zanzibar aliyeingia madarakani kimizengwe.
Hivi karibuni kumekuwa na purukushani za aina yake Zanzibar baada ya Maalim kutua katika visiwa hivyo.
Aidha Maalim anadai kuungwa mkono na wapenda haki wengi duniani.
"Nitaendesha harakati za amani kabisa kumng'oa Shein, hata kama tutapigwa mabomu hatutarudi nyuma" anasema Maalim.
Rais Shein aliingia madarakani hivi karibuni kutokana na uchaguzi wa aina yake kuwahi kutokea ambapo chama chake cha CCM kilijitwalia asilimia mia moja ya ushindi katika ngazi zote. Uchaguzi huo uligubikwa na utata na mizengwe mikubwa ambapo umeigharimu kwa kiasi kikubwa nchi ya Tanzania.