Maalim Seif: CHADEMA waroho wa madaraka

mbinguni

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
2,197
2,000
Mzee wa uliberali anadhani Elerai ni Zenji?Asubiri June 16, 2013 ataisikilizia kwenye bomba chadema itakavyowaunguza cuf na wenza wao,ccm.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hammad amekirushia kombora Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kile alichodai kinapoteza mwelekeo kutokana na fujo nyingi zinazotokea wakati wa vikao vya Bunge. Alisema fujo hizo, ni wazi zinaonekana kusababishwa na uroho wa madaraka.

Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Eralai, John Bayo.

Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.

Alisema kutokana na umoja na uaminifu ambao CUF ilikuwa nao, ndiyo ilimteua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa kuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

“Wakati CUF inaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, tulikuwa na umoja mno, tulishirikiana na vyama vyote vya upinzani na naibu wetu, alikuwa Dk. Slaa.

“Ila wao Chadema, walipopata wakaanza kusema wao ni wao, ndugu zangu ndio maana leo hii mnaona Bunge limekuwa la fujo utadhani soko, watu wanamwaga matusi kama cherehani, maadili ya Bunge yameachwa,” alisema Hammad.

Alisema CUF ni chama chenye dira na kinachoona mbali, kwa sababu kimeundwa kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi wote na dira yao.

Kwa upande wake, Bayo akiomba kura alijikuta akiangua kilio mbele ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

Bayo, ni moja ya madiwani waliotimuliwa CHADEMA kwa madai ya kupokea rushwa na kukisaliti chama hicho.

“Sijagusa hata senti kwa ajili ya kuwasaliti watu wangu, najua kitendo hicho kinakiuka maadili na kuwasaliti nyinyi mlionichagua.

Kwa hisani ya Mtanzania.
 
CANIMITO

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,279
2,000
Mleta thread,Maalim angetaja fujo 3 zilizofanywa na CHADEMA bungeni na aweke sababu za fujo hizo ili tupime.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,875
1,500
Hivi kuna mroho wa madaraka kama Maalimu Seif?

Hamad Rashid alipoonesha kugombea ukatibu wmkuu wa CUF Maalim Seif akamuundia zengwe na kumfukuza uanachama kabla ya kurudishiwa na Mahakama.

Maalim Seif na Lipumba WAMEJIFANYA wagombea wa kudumu wa U-Rais wa SMZ na JMT respectively tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1995.

CDM chama makini kilishawahi kuwaunga MKONO CUF kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 kwenye nafasi za URAIS wa JMT na SMZ. Kama CUF sio WAROHO wa madaraka basi nao waiunge mkono CDM 2015! thubutu yako Maalim.

CUF na CDM walishirikiana bungeni kuunda kambi rasimu ya UPINZANI kwasababu lilikuwa hitaji la kikanuni. CUF ilikuwa haina wabunge wa kutosha kuunda kambi ya UPINZANI peke yao.
 
Mtingaji

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
1,209
1,225
Tangu walivyotangaza wao ni walibarali, sisiem ikafunganao ndoa ya mkeka wakawa wapole kama wananyolewa. Wakawasaliti wazanzibari mchana kweupe! Hivi sasa anawashambulia CDM kwa vile chama chake kimekosa umaarufu Bara na visiwani.

Hamad Rashid nayeye alikuwa anatamani madaraka ya kuwa kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, alipoukosa pamoja na kusaidiwa na sisiem, akaugeukia u-Seif Sharifu Hamadi (Ukatibu Mkuu wa Kafu) ndipo alipokutana na teke lililo mpeleka ADC!

Hiyo yote ni uroho wa madaraka, sasa hivi maalimu ana kula keki ya Taifa taratibu bila kelele kwani alichokuwa anakitafuta (madaraka) keshayapata!
 
Galapagos

JF-Expert Member
Nov 26, 2012
252
195
Nashangaa na mimi kuwa Seif halioni hilo.

Dkt. Ulimboka alifanywa nini? Serikali imeshachukua hatua gani? Kisa madaraka....

Mwangosi alifanywa nini? Na bado Kamhanda kapandishwa cheo! Madaraka hayo....

Kibanda sasa miezi mitatu hakuna hata fununu ya uchunguzi! Kisa madaraka......

Propaganda za kitoto mara ugaidi, mara personal attacks kisa madaraka....
Mkuu usiangaike na huyo mliberali mzoefu
 
Kapwani

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
668
195
Wewe usipotoshe umma sisi tunafuatilia siasa za Tanzania wakati cuf inaamzishwa katibu Mkuu alikuwa shaaban mloo Kisha akaja maalim seif mkutano Mkuu Ndio uliompitisha kwa kura tukijaaliwa kwenu chadema wakati Zito Kabwe anataka uenyekiti walitoka kina mtei moshi kumtaka atoe jina lake harafunajiita chama cha democrasia cuf huziiwi na wazee jaza fomu wanachama Ndio wanaoamua nani mkweli ktk wagombea Kama unatumika hupewi kile ni chama cha ukombozi huwezi kupewa Mtu magumash utuulie Zito alivyotaka aongoze kambi ya upinzani bungeni mboe amekataa hata hilo hamulisemi kwa vile bepari mwenzenu
Una kumbu kumbu ya Prof Safari & uchaguzi CUF?
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hammad amekirushia kombora Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kile alichodai kinapoteza mwelekeo kutokana na fujo nyingi zinazotokea wakati wa vikao vya Bunge. Alisema fujo hizo, ni wazi zinaonekana kusababishwa na uroho wa madaraka.

Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Eralai, John Bayo.

Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.

Alisema kutokana na umoja na uaminifu ambao CUF ilikuwa nao, ndiyo ilimteua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa kuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

“Wakati CUF inaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, tulikuwa na umoja mno, tulishirikiana na vyama vyote vya upinzani na naibu wetu, alikuwa Dk. Slaa.

“Ila wao Chadema, walipopata wakaanza kusema wao ni wao, ndugu zangu ndio maana leo hii mnaona Bunge limekuwa la fujo utadhani soko, watu wanamwaga matusi kama cherehani, maadili ya Bunge yameachwa,” alisema Hammad.

Alisema CUF ni chama chenye dira na kinachoona mbali, kwa sababu kimeundwa kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi wote na dira yao.

Kwa upande wake, Bayo akiomba kura alijikuta akiangua kilio mbele ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

Bayo, ni moja ya madiwani waliotimuliwa CHADEMA kwa madai ya kupokea rushwa na kukisaliti chama hicho.

“Sijagusa hata senti kwa ajili ya kuwasaliti watu wangu, najua kitendo hicho kinakiuka maadili na kuwasaliti nyinyi mlionichagua.

Kwa hisani ya Mtanzania.
Hakuna sababu ya kuhangaika kumjibu huyu mliberali; hajui maana ya maneno aliyosema; ni mchecheto kutokana na hali alivyoikuta mbaya kwa mgombea wake, Msaliti John Bayo
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,194
2,000
Wewe usipotoshe umma sisi tunafuatilia siasa za Tanzania wakati cuf inaamzishwa katibu Mkuu alikuwa shaaban mloo Kisha akaja maalim seif mkutano Mkuu Ndio uliompitisha kwa kura tukijaaliwa kwenu chadema wakati Zito Kabwe anataka uenyekiti walitoka kina mtei moshi kumtaka atoe jina lake harafunajiita chama cha democrasia cuf huziiwi na wazee jaza fomu wanachama Ndio wanaoamua nani mkweli ktk wagombea Kama unatumika hupewi kile ni chama cha ukombozi huwezi kupewa Mtu magumash utuulie Zito alivyotaka aongoze kambi ya upinzani bungeni mboe amekataa hata hilo hamulisemi kwa vile bepari mwenzenu
Shibuda alipotaka kugombea urais kupitia CCM nini kilitokea Sheikh Yahaya alisemaje, acha unafiki pimbi weweCUFtumeshawaunga mkono mara ngapi? tulichotofautiana naCUF nikuigamakubaliano na CCM ya kumuunga mkono Kikwete kwa kuwa ni mwislamu na Lipumba ni mwislamu mwenzake wakaacha utaifa wakatanguliza dini zao sasa ulitaka tuendelee kushirikiana kwa lipi watu wameshajiweka wazi au hata video hujaziona na uliwekewa humu JF kama hujalizika na hizo muombe bi kiroboto maana alishapewa na Lema.
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,194
2,000
Kibaraka ni Mbowe aliekulia ikulu wakati wa Nyerere seif kafukuzwa na mwalim atokee kiongozi jasiri wa chadema atamke hadharani maovu ya mwalim Kama opeshen vijiji watu waliliwa na simba kupora majumba ya watu unga wa yanga tulikula ambacho ni chakula cha farasi marekani Lipumba na seif wanamkosoa mwalim slaa na Mbowe hathubutu kisema nani Kibaraka hapo huu si wakati wa propaganda chama chaukombozi huwahakibadili ovyo viongozi hadi nchi ikikombolewa Kama mandera mnataka. Wakae viongozi si waadirifu muje muwanunue kirahisi cuf hakai Mtu wa kutumika pale mbona hamumsakami mtikila toka dp ianzishwe m.kiti ni yeye na mzirai hamsemi nyie mnaifuata cuf mnaagenda gani mnaacha kuishutumu ccm iliyowatawala zaidi ya miaka 50 kila kukicha cuf vile mala vile mabepari wakubwa
Adui yako ni Mw. JK Nyerere? unataka wamseme Marehemu, hivi usivyo na akili hata ya kupengea kamasi unaweza kufananisha CCM ya Nyerere na uozo wa CCM ya sasa iliyojaa ufisadi ubinafsi wa kupindukia..Nyerere sisemi kuwa hakuwa na mapungufu lakini ukimlinganisha na nani hapa Tanzania
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,670
2,000
Seif akae kimya!watapewaje nafasi ya kambi ya Upinzani Bungeni wakati wameungana na CCM bungeni na Serikalini?Maalim anahoji uroho wa madaraka?...mbona yeye amehongwa umakamu wa Rais usio na nguvu sie tupo kimya?kawa kama Ceremonial,hana nguvu wala madaraka..raha yake kula marupurupu..amewauza CUF ktk ndoa ya CCM...Yupo kama Joka la Kibisa..haling'ati wala kutema mate..unaweza kuliweka hata ndani ya suruali na lising'ate...kama unataka ujue tabia ya Joka la kibisa,basi Ijumaa nenda Break Point pale Posta uone WANNE STAR anavocheza na joka na kisha kulifungia ktk box...SEIF umewauza CUF kwa ndoa ya CCM
 
KIJOME

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
3,085
1,225
Mleta mada ni gamba anamsaidia promotion mliberali wao kafu a.k.a mwanandoa wa gamba!!!
 
tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,554
1,195
Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.
Leo anamtambua Hamad Rashidi!... Mhhh hiki kituko.
 
tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,554
1,195
Mleta mada ni gamba anamsaidia promotion mliberali wao kafu a.k.a mwanandoa wa gamba!!!
Humjui!!... Ni mliberali.. Yuko pamoja na magamba mpaka JK akiondoka madarakani. Akigombea Lowasa anarudi kuendeleza mambo ya mombasa.
 
tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,554
1,195
Wewe usipotoshe umma sisi tunafuatilia siasa za Tanzania wakati cuf inaamzishwa katibu Mkuu alikuwa shaaban mloo Kisha akaja maalim seif mkutano Mkuu Ndio uliompitisha kwa kura tukijaaliwa kwenu chadema wakati Zito Kabwe anataka uenyekiti walitoka kina mtei moshi kumtaka atoe jina lake harafunajiita chama cha democrasia cuf huziiwi na wazee jaza fomu wanachama Ndio wanaoamua nani mkweli ktk wagombea Kama unatumika hupewi kile ni chama cha ukombozi huwezi kupewa Mtu magumash utuulie Zito alivyotaka aongoze kambi ya upinzani bungeni mboe amekataa hata hilo hamulisemi kwa vile bepari mwenzenu
Hee Zitto ni mwakilishi wa ccm, Cuf, kabila lako au dini yako?
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
46,576
2,000
Mliberali Maalim Seif hana uhalali uhalali wa kusimama na kuongea mbele ya raiya wenye akili timamu.

NB:

CCM na CUF hapa Arusha mnachezea pesa zenu bure kuhonga.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,660
2,000
Hana adabu kabisa Seif kwanza ujinga wake huo apeleke huko huko Zanzibar anakosema anataka mamlaka kamili anatafuta nini Arusha,Mgombea wa maisha CUF-Zanzibar huo sio uroho wa madaraka,fujo na matusi ya nguoni wanayotoa wabunge wake wa CUF na wa mumewe CCM hajaona hizo propaganda apeleke kwa mkewe vinginevyo anapoteza muda kutmia fedha za serikali kuja kumnadi mgombea mwizi wa fedha za ujenzi wa clinic ya olimpiki
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,988
2,000
Mume na mke huwa hawapishani matamko,kwa sababu mambo yote huwa wanayapanga wakiwa chumbani,
hakuna jipya hapo.
 
Top Bottom