Maalim Seif 'aunguruma' Manzese - Dar

Shujaa anaepozwa na pesa,anaweza kuuza jeshi lake.
Tusubiri sarakasi mm ntakuwa muangaliaji
 
kwanini aje dar anafuata nini? watu tuna mambo mengi ya msinhi ya kufanya siyo kusikiliza watu wanaotetea matumbo yao alaah!
 
Naamini katika mkutano akina mama hawataruhusiwa kuchanganyika na kinababa.Pia baraghashia zitajaa mkutanoni
 
Kabla hamjaanza mkutano pitieni kwanza Ujumbe wa muhasisi wa CUF James Mapalala. (source: Tanzania Daima Jan 7 2012)

James Mapalala amlipua Maalim Seif
• Atuhumiwa kutumia ‘walevi’ kumfukuza 1994

na Asha Bani

MUASISI na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Wananchi (CUF), James Mapalala, alisema yanayotokea ndani ya chama hicho hayamshangazi kwa kuwa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad alitumia watu ‘walevi’ kumfukuza ndani ya chama hicho mwaka 1994.

Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana, Mapalala alisema Maalim Seif ni kiongozi anayewatumia baadhi ya wanachama wake kupata mafanikio, na kisha hutumia nguvu kuwafukuzwa kwa vitimbi kama alivyofanyiwa yeye na sasa Hamad Rashid Mohamed.

Alidai kuwa Maalim Seif aliwahi kumtumia yeye kama daraja mwaka 1992 kwa kuzunguka nchi nzima bara na Zanzibar, akilala vijijini kwa lengo la kukitangaza chama ili waweze kuwakomboa wananchi wanyonge lakini matokeo yake alimfukuza kwa visingizio mbalimbali ambavyo si vya kweli.

Mapalala alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Maalim Seif si mtu wa kawaida hasa unapogusia masuala ya madaraka kwa kuwa ni mtu ambaye anapenda fedha na madaraka, huku akiyatumia vibaya kwa kuwakandamiza wanyonge.

“Hakuna mtu ndani ya CUF asiyejua kwamba Hamad Rashid alikuwa ni mtu muhimu sana ndani ya chama hicho kwani ndiye kiongozi wa pekee mwenye uwezo wa kutafuta fedha nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha chama, lakini Maalim amemtimua kama ilivyokuwa kwangu baada ya kufanikiwa kupata mafanikio mbalimbali hadi kuwa Makamu wa Rais,” alisema Mapalala.

Mapalala alidai kuwa Maalim Seif anapenda kila atakalosema yeye ndilo litendwe na watu wote ndani ya chama bila kuzingatia maoni ya watu wengine hata kama si jambo zuri kwa maslahi ya chama.

Akizungumzia kufukuzwa kwake ndani ya chama, alisema kuwa mwaka 1994 katika mkutano uliyofanyika mkoani Tanga alitimuliwa bila kupewa sababu za msingi na kwamba waliofanya maamuzi katika mkutano huo hawakuwa wanachama halali na nakala za barua na majina yao anayo hadi sasa.

Aidha aliwaonya viongozi mbalimbali wa CUF kuwa wanapozungumzia matatizo yao ndani ya chama hasa katika kipindi hiki ambacho wamemfukuza Hamad wasitolee mfano jina lake kwa kuwa ana vielelezo vyote vya Maalim Seif na wenzake kutumia ‘walevi’ wa pombe ambao walihongwa huku wakiwa si wajumbe ili waweze kunifukuza.

“Tena sitaki kabisa wasijipe umaarufu kusafisha dhambi zao kwa kunitaja mimi. Katika mkutano ule wa Tanga waliokuwa wameitisha kwa ajili ya kunifukuza mimi, nilipewa barua masaa machache na kwamba mkutano ulifanyika usiku, wajumbe walikuwa si halali na vielelezo hadi sasa ninavyo wasitake niwaumbue,” alisema Mapalala.

Mapalala alisema Maalim Seif bila kujiingiza katika migogoro alitakiwa kuangalia hali ya wananchi wa Zanzibar hasa Pemba ambao tangu kuingia kwa serikali ya mseto mambo ndiyo yamezidi kuwa magumu zaidi.

“Sharif Hamad ni kiongozi ndani ya CCM ndio maana anashindwa kuwatetea wananchi, ameua chama; watu wanahoji anakuja juu, watu wanahoji matumizi ya fedha anakuja juu, ni mtu ambaye anapenda sana madaraka na hili ndilo tatizo kubwa ambalo linaua demokrasia ndani ya vyama hasahasa chama hicho,” alisema Mapalala.

Aidha alimshauri mbunge huyo wa Wawi kama ana nia ya kuwakomboa wananchi hasa wakazi wa Pemba basi aendelee kwa kuanzisha chama chake asirudi CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kimeungana na Maalim Seif.

Mapalala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Chausta amemkaribisha Hamad Rashid kujiunga nacho kwa vile anaamini ni kiongozi makini na mchapa kazi hodari
 
Ataongea kama katibu wa cuf ama kama ""makamo" rais visiwa vya zanzibar? hpe atasisitiza ile inshu ya zanzibar kuwa na benki kuu yao!
 
Pale Manzese wameweka/wamesimamisha bendera ya CUF(kushoto mwa jukwaa) na ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (kulia mwa jukwaa)

Sijaona bendera ya JM wa Tanzania.
 
Enyi cuf tupeni anachoongea ms au mkutano haujaanza? au wote humu jamvini mlikuwa washabiki wa HR
 
Kabla hamjaanza mkutano pitieni kwanza Ujumbe wa muhasisi wa CUF James Mapalala. (source: Tanzania Daima Jan 7 2012)

James Mapalala amlipua Maalim Seif
• Atuhumiwa kutumia ‘walevi’ kumfukuza 1994

na Asha Bani

MUASISI na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Wananchi (CUF), James Mapalala, alisema yanayotokea ndani ya chama hicho hayamshangazi kwa kuwa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad alitumia watu ‘walevi’ kumfukuza ndani ya chama hicho mwaka 1994.

Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana, Mapalala alisema Maalim Seif ni kiongozi anayewatumia baadhi ya wanachama wake kupata mafanikio, na kisha hutumia nguvu kuwafukuzwa kwa vitimbi kama alivyofanyiwa yeye na sasa Hamad Rashid Mohamed.

Alidai kuwa Maalim Seif aliwahi kumtumia yeye kama daraja mwaka 1992 kwa kuzunguka nchi nzima bara na Zanzibar, akilala vijijini kwa lengo la kukitangaza chama ili waweze kuwakomboa wananchi wanyonge lakini matokeo yake alimfukuza kwa visingizio mbalimbali ambavyo si vya kweli.

Mapalala alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Maalim Seif si mtu wa kawaida hasa unapogusia masuala ya madaraka kwa kuwa ni mtu ambaye anapenda fedha na madaraka, huku akiyatumia vibaya kwa kuwakandamiza wanyonge.

“Hakuna mtu ndani ya CUF asiyejua kwamba Hamad Rashid alikuwa ni mtu muhimu sana ndani ya chama hicho kwani ndiye kiongozi wa pekee mwenye uwezo wa kutafuta fedha nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha chama, lakini Maalim amemtimua kama ilivyokuwa kwangu baada ya kufanikiwa kupata mafanikio mbalimbali hadi kuwa Makamu wa Rais,” alisema Mapalala.

Mapalala alidai kuwa Maalim Seif anapenda kila atakalosema yeye ndilo litendwe na watu wote ndani ya chama bila kuzingatia maoni ya watu wengine hata kama si jambo zuri kwa maslahi ya chama.

Akizungumzia kufukuzwa kwake ndani ya chama, alisema kuwa mwaka 1994 katika mkutano uliyofanyika mkoani Tanga alitimuliwa bila kupewa sababu za msingi na kwamba waliofanya maamuzi katika mkutano huo hawakuwa wanachama halali na nakala za barua na majina yao anayo hadi sasa.

Aidha aliwaonya viongozi mbalimbali wa CUF kuwa wanapozungumzia matatizo yao ndani ya chama hasa katika kipindi hiki ambacho wamemfukuza Hamad wasitolee mfano jina lake kwa kuwa ana vielelezo vyote vya Maalim Seif na wenzake kutumia ‘walevi’ wa pombe ambao walihongwa huku wakiwa si wajumbe ili waweze kunifukuza.

“Tena sitaki kabisa wasijipe umaarufu kusafisha dhambi zao kwa kunitaja mimi. Katika mkutano ule wa Tanga waliokuwa wameitisha kwa ajili ya kunifukuza mimi, nilipewa barua masaa machache na kwamba mkutano ulifanyika usiku, wajumbe walikuwa si halali na vielelezo hadi sasa ninavyo wasitake niwaumbue,” alisema Mapalala.

Mapalala alisema Maalim Seif bila kujiingiza katika migogoro alitakiwa kuangalia hali ya wananchi wa Zanzibar hasa Pemba ambao tangu kuingia kwa serikali ya mseto mambo ndiyo yamezidi kuwa magumu zaidi.

“Sharif Hamad ni kiongozi ndani ya CCM ndio maana anashindwa kuwatetea wananchi, ameua chama; watu wanahoji anakuja juu, watu wanahoji matumizi ya fedha anakuja juu, ni mtu ambaye anapenda sana madaraka na hili ndilo tatizo kubwa ambalo linaua demokrasia ndani ya vyama hasahasa chama hicho,” alisema Mapalala.

Aidha alimshauri mbunge huyo wa Wawi kama ana nia ya kuwakomboa wananchi hasa wakazi wa Pemba basi aendelee kwa kuanzisha chama chake asirudi CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kimeungana na Maalim Seif.

Mapalala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Chausta amemkaribisha Hamad Rashid kujiunga nacho kwa vile anaamini ni kiongozi makini na mchapa kazi hodari

Kama kweli Mapalala alionewa mbona asikiki tena kwenye hicho chama chake cha CHAUSTA? CUF ni kubwa kuliko mwanachama yeyote na ukiwa msaliti lazima watakung'oa. Mapalala hajiulizi kwanini Wazanzibar wanaimani na maalim Seif? Kusema anapenda hela si kweli. Maalim Seif hana hata Nyumba Unguja na ana nyumba ya kawaida Pemba huyu mtu si fisadi na ana historia nzuri katika matumizi ya ofisi ndio maana Wazanzibar wana imani naye.

Mtapiga kelele mpaka mchoke aliyeandikiwa A ni A tu.
 
Kwakuwa wamemfukuza HR na wenzake nimeanza kuamini hakuna chama cha maana Tanzania; kulikuwa na haja gani ya kumfukuza busara gani ilishindikana kabisa kutumika..

Nilikuwa namuamini Seif lakini nimeanza kuweka alama ya kuuliza?? i am watching him closely
 
Kama kweli Mapalala alionewa mbona asikiki tena kwenye hicho chama chake cha CHAUSTA? CUF ni kubwa kuliko mwanachama yeyote na ukiwa msaliti lazima watakung'oa. Mapalala hajiulizi kwanini Wazanzibar wanaimani na maalim Seif? Kusema anapenda hela si kweli. Maalim Seif hana hata Nyumba Unguja na ana nyumba ya kawaida Pemba huyu mtu si fisadi na ana historia nzuri katika matumizi ya ofisi ndio maana Wazanzibar wana imani naye.

Mtapiga kelele mpaka mchoke aliyeandikiwa A ni A tu.

Unaonaje tukimpa urais wa Tanzania?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom