Maalim Seif atoa masharti ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo Zanzibar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametoa masharti ambayo yakifuatwa chama hicho kitakuwa tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafuta suluhu ya mgogoro wa siasa visiwani humo.

Alikuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya International Republican Institute (IRI) mjini Washington DC, Marekani juzi.

Maalim Seif alisema: “Tuko tayari kushirikiana na Serikali ya CCM visiwani Zanzibar kwa kuunda Serikali ya mpito ya Umoja wa kitaifa itakayooongoza kwa muda.”

“Baada ya hapo tutakuwa tayari kwenda kushiriki uchaguzi mpya kwa sharti tu usimamiwe na chombo huru cha kimataifa”.

Seif alisema hayo wakati akieleza hali ya siasa visiwani humo pamoja na matukio yaliyopelekea hali hiyo.

Licha ya ukandamizaji huo kutoka serikali na vyombo vya dola, alieleza jinsi chama chake kinavyoendesha kampeni ya upinzani kwa njia ya amani bila kuhusisha machafuko.

Seif alisisitiza kwamba Zanzibar haiwezi kuendeshwa kwa staili ya biashara kama kawaida.

Alitahadharisha kwamba bila hatua kuchukuliwa kuokoa hali mbaya ya siasa visiwani humo, kuna uwezekano mkubwa Zanzibar kugeuka kuwa maficho ya Waislamu wenye itikadi kali.

“Hofu yetu ni kwamba kwa kadiri ya njia za demokrasia zinapoendelea kufungwa, makundi ya dini ya msimamo mkali yatapata nafasi.

“Zanzibar kwa muda mrefu ina uhusiano na kambi zinazohusiana na harakati za wanamgambo wa Kiislamu kama vile Somalia, sehemu za Pwani ya Mashariki ya Kenya na hata Mashariki ya Kati.

“Kinachotokea Zanzibar ni mfano wa visababishi kwa jamii kuchagua kuangukia katika machafuko ya itikadi kali, utawala dhaifu wa uchumi; umasikini na ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana. Yote yakisababishwa na hali ya kukata tamaa, ukosefu wa haki na ukandamizaji na ukosefu wa uhuru wa siasa,” alisema na kuongeza:

“Ndiyo maana tunakataa kukata tamaa na ndiyo maana harakati zetu za demokrasia ni zaidi ya Zanzibar.

‘Sisi ni nchi ndogo, lakini kinachotutokea kina athari mbaya na pana kwa bara Afrika na duniani kwa ujumla– iwe kwa namna nzuri kama kichocheo cha maendeleo ya uchumi katika eneo hili au namna mbaya kuwa ukandamizaji unakigeuza kisiwa chetu kiwe mwathirika wa makundi yenye itikadi kali za dini”.
 
Kwani ni nani amemwambia wakae kwenye meza ya mazungumzo? Atakaaje kwenye meza ya mazungumzo na serikali ambayo haitambui????? Nadhani ni busara aendelee na kampeni zake huko majuu.
 
Serikali ya mpito ya nini tena Maalim ya nini tena ? Tuanze kushirikiana na hawa akina Ali Karume tena ! Napinga , Seif Urudishiwe urais wako tu .
 
Kwani ni nani amemwambia wakae kwenye meza ya mazungumzo? Atakaaje kwenye meza ya mazungumzo na serikali ambayo haitambui????? Nadhani ni busara aendelee na kampeni zake huko majuu.
maalim sefu, haitambui serikali alafu analalamika, wafuasi wake wanamuita Rais, sasa nani wa kusuluhisha ikiwa kila mtu mbabe
 
maalim sefu, haitambui serikali alafu analalamika, wafuasi wake wanamuita Rais, sasa nani wa kusuluhisha ikiwa kila mtu mbabe
AMESUSA WENZAKE WALA NA SASA ALALAMIKA ameona hapa hakuna amsikizae ameenda huko ughaibuni pengine atatokea wa kuilazimisha TZ kufanya uchaguzi mwingine.
 
Ameshalegea huyo. Si alisema kuwa yeye ni Rais wa mioyo ya Wazanzibari? Sasa uchaguzi wa nini? Si asubiri baada ya miaka mitano? Sisiemu hatutakubali kuchezewa kama mdori

Wewe hujui diplomasia ya siasa. Unafikiri hao CCm wana amani? Nchi imerudi nyuma sana na uhasama umeingia. Yeye kaonesha dalili za pa kuanzia kutatuwa hali huko visiwani. Unafikiri ikiwa itafika mahala jumuiya za kimataifa zitoe oda kwa mashauri ya kura kule UN CCM watakaidi na kujitia kiburi? ( lakini wanaweza hawa)

Kumbuka KADIRI MGOGORO UNAVYOZIDI UNAWAUMIZA WAZANZIBARI NA HILO CCM HAWAJALI NDIO MAANA WAKAKATAA MAZUNGUMZO NA KULAZIMISHA UCHAFU WA MARUDIO

Kama ni utaalamu wa siasa maalim ni gwiji na hata wazungu hilo wameliona. Nini kitafuata ? muda utasema.
 
Mtaalamu Mhhhh...Hujasikia CCM wameshamjibu.Unguja Iko shuari....mwambieni atafute jengine
 
Wewe dai urais wako,acha mambo ya serikali za mpito sijui ya umoja wa kitaifa...ccm hawakuhitaji.
 
Maalim kwisha habari yake amekua mlaini anaomba poo!!! Sasa hayo masharti anampa nani na kwa foroum ipi? Njaa imembana anakumbuka serekali ya umoja wa kitaifa ma.ma.eee
 
Njaa ni mbaya! Sasa Maalim anatafuta suluhu na watu ambao hawana ugomvi naye. Yeye anasema ni rais lkn hana ki2. Hana jeshi, ikulu, mamlaka, dola etc. anajidanganya anacheka kama chizi! Rais hatishiwi nyau kwani ana dola. Asubiri 2020 na ashiriki uchaguzi bila kususa. Vinginevyo dola itakushukia!
 
Back
Top Bottom