Maalim Seif alishinda – Zitto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif alishinda – Zitto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi Maalum - Mwanahalisi
  Imechapwa 11 January 2012

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe amenukuliwa akisema Maalim Seif Shariff Hamad alishinda uchaguzi mkuu wa 2010.

  Hii ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote ndani ya vyama vya siasa kunukuliwa akijadili suala hili tangu uchaguzi huo ulipokwisha.

  Akimwandikia Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa Ladhu, mbunge huyo alisema hata Jussa anajua kuwa Maalim Seif alishinda uchaguzi.


  Zitto anasema Maalim Seif alikubali kutangazwa kuwa ameshindwa na kwamba Jussa anajua kuwa kiongozi wake huyo alishinda urais wa Zanzibar.


  Kauli ya Zitto imepatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forum (JF). Imeelezwa kuwa mawasiliano hayo yalichotwa kutoka mtandao wa Zitto wa Face Book tarehe 5 Januari 2012.


  "Ndugu Jussa," ananukuliwa Zitto akiandika, "kama rafiki yako mkubwa na unajua ninavyomheshimu Maalim Seif kama kiongozi thabiti. Leo nakwambia usilolipenda. Sio sahihi katika demokrasia kama yetu kumfukuza Mbunge Hamad Rashid au hata wanachama wengine wa chama chenu cha CUF."


  Tarehe ya waraka huu inaonyesha ndiyo siku ambayo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lilikutana mjini Zanzibar kufukuza baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed.


  "Kama Maalim aliweza kumsamehe Salmin, aliweza kumsamehe Karume, aliweza kukubali kutangazwa kushindwa ilhali hata wewe (Jussa) unajua alishinda Urais wa Zanzibar, iweje iwe muhali kumaliza tatizo hili dogo la Hamad Rashid?" anahoji Zitto.


  Katika mawasiliano hayo, Zitto anasema, "Hamad ana makosa lukuki. Nimefanya naye kazi bungeni. Hamad pia ana mazuri mengi kafanya. Hamad amejitoa muhanga. Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kumfukuza uanachama ufikiriwe upya."


  Zitto, kwa mujibu wa mawasiliano hayo, alikuwa akijaribu kumsihi Jussa kumshawishi Maalim Seif kuangalia upya uamuzi wa kumfukuza uanachama Hamad Rashid na wenzake waliopo katika mvutano wa uongozi.


  Salmin aliyemlenga Zitto anafikiriwa kuwa ni Dk. Salmin Amour Juma (Komandoo) na kwa Karume inasadikika kuwa ni Amani Abeid Karume aliyeongoza kuanzia Novemba 2000 mpaka Oktoba 2010.


  Viongozi wote hao, Komandoo na Karume, walitangazwa washindi huku CUF iliyomsimamisha Maalim Seif ikilalamikia matokeo kwa maelezo kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilikula njama kuvuruga uchaguzi ili kunufaisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Matokeo hayo yalisababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa na kujenga uhasama kati ya viongozi hao, Maalim Seif na uongozi wa CUF.


  Hata hivyo, wakati Dk. Salmin alikataa kutekeleza muafaka wa 1996 wa CCM na CUF uliofikiwa chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Madola, Karume aliingia katika mazungumzo ya siri na Maalim Seif yaliyozaa utawala wa ubia kati ya vyama hivyo viwili.


  Kauli ya Zitto kwamba Jussa anajua Maalim Seif alivyokuwa ananyimwa ushindi, inaelekea kuthibitisha kauli za malalamiko ya hivi karibuni ya Hamad Rashid kuwa Jussa "alishindwa" kuwasilisha baadhi ya fomu za matokeo zilizokusanywa vituoni Unguja.


  Gazeti hili lilinukuu vyanzo mbalimbali ndani ya CUF vilivyosema kuwa timu ya kampeni iliyoongozwa na Jussa ilizembea kukusanya na kuwasilisha matokeo ya urais katika baadhi ya majimbo Unguja.


  Aidha, kuna madai kuwa Jussa alimshinikiza Maalim Seif kukubali matokeo ya kura za urais hata kabla matokeo ya mwisho kupatikana.


  Madai hayo yametumiwa na kina Hamad Rashid kulalamika kuwa wanasakamwa isivyo halali wakati kuna viongozi walioumiza chama hicho kutokana na kushindwa kuwajibika wakati wa uchaguzi kiasi cha kumkosesha ushindi mgombea wao.


  Zitto ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amekuwa rafiki wa karibu wa Jussa, wote wakiwa ni wanasiasa vijana wanaokiri waziwazi kuwa na uhusiano wa karibu na mfanyabiashara Rostam Aziz ambaye pia ni kada mwenye nguvu ndani ya CCM.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kama Zitto ulijua hayo kwanini Mlikaa kimya? ina Maana hata CCM walijua hayo?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu vipi Zitto ana kauli gani juu ya uchaguzi wa JmT wa mwaka 2010z
   
 4. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tunajua Seif alishinda Zanzibar, ila alihongwa na Magamba katika mkutano wao Ikulu. Rejea thread ya "JK, huu mtandao ni hatari!Be Careful, otherwise waweza kuwa historia"
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,946
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  Tukichapana hii nchi ndo tutaheshimiana
   
 6. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Propaganda!
   
 7. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Haya,...siipendi siasa kabisa
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni wazi sasa rafiki yangu kubenea ameshikwa pabaya na mafisadi,yani anawezaje kuja humu ku copy story na kwenda kuipaste kwenye gazeti lake?kwanini asitafute story zake mwenyewe kama zamani?na sheria zinasemaje kuhusu kuiba story za humu na kwenda kuzipublish kwenye magazeti yao huku wanalipana mishahara kwa kazi ya kutafuta story?je huu ndio uandishi wa habari za uchunguzi kucopy na kupaste?Nakumbuka miaka ya nyuma tuliwahi kumshambulia mhariri wa gazeti la kulikoni wakati huo kwa mchezo kama huu huu alipochukua mjadala wa fulani humu ukimhusisha bwana zitto kabwe huyu huyu na wadau humu kuhusu tabia yake ya kutia mashaka baada ya kutoa kauli tata za kumbeba mkurugenzi wa tanesco wakati huo dk idrisa rashid na pia ule ushauri wake wa serikali inunue mitambo ya dowans,mlioishi wakati huo humu mtakumbuka hii kitu.Tukamkemea sana yule mhariri kwa uvivu haya mambo yakaisha,sasa kubenea na gazeti lake wameanza tena huu mchezo.
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Una Maana Gani? Mtandao Gani ni Hatari? sasa tunatishwa?
   
 10. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndio maana kila kukicha wana rap mapinduzi daima! This is bad.
   
 11. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Zitto atuambie vipi DR Slaa nae alishinda?
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwani zitto alikuwa sayari ipi wakati matokeo yanatangazwa? alikuwa wapi kusema muda wote? siasa za kinafiki. sikutarajia Zitto kunyamaza kwa zaidi ya mwaka mzima kuhusu matokeo hayo labda kama ana agenda ya siri
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  umaarufu wa zitto utaendelea kupungua kama ataendelea kudandia hoja mfu kama hizi na kukaa kimya kwenye agenda hai za sasa.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hii inaonyesha kwamba Dr Slaa alishindwa kihalali na Jk kwani Zitto angeanza na chama chake kama ni kweli Dr Slaa alishinda kama inavyodaiwa. Ama sivyo tukubaliane kwamba ndani ya chadema kuna mgogoro wa chini chini kati ya Zitto maslahi, Dr Slaa maslahi na mbowe maslahi.
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kauli za Zitto utata mtupu na mara nyingine sio kwa maslahi ya chama chake.
   
 16. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilitaka kukujibu lakini baada ya kusoma jina lako nimeamua kukaa kimya uendelee na porojo mama
   
 17. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aondoke na unafiki wake,kisha ishiwa hoja huyu kijana
   
 18. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dua la kuku...
   
 19. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kinachoshangaza ni kuwa sio Zitto pekee anayefahamu kuwa Maalim Seif alishinda, ina Maana kuna watu ndani ya CCM na CUF wanajua na Viongozi wa Uchaguzi wanajua, ni nani huyo mwenye nguvu aliyetua Ushauri wa kuchakachua Ushindi wa Maalim Seif? na walimpa Pesa? za kuishi? na walizipata pesa wapi? au ndio wizi huo? kushibishana?

  Ndio Maana Maalimu Seif ana nguvu ndani ya CUF na hawezi kuwa na Mpizani, Mpinzani yoyote anafukuzwa CUF???

  * WHERE IS REAL DEMOCRACY IN TANZANIA? DO WE REALLY NEED OPPOSITION THEN? IF THEY EAT THE SAME TABLE WITH THE FAKE RULING PARTY???
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Hehehe ..... LoL
   
Loading...