Maalim Seif Akimfariji Mhe Hamadi Rashid

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,408
[h=5]Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa

Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd[/h] seif.jpg
 
Mungu amfariji ndugu yetu aliyeachwa, watoto familia na marafiki wote. Ni jambo la huzuni sana. Kikubwa ni kukubali mpango wa Mungu na kuandaa maisha yetu maana hatujui siku wala saa. Tunahitaji kujua ipo siku nasi tutaondoka. Kikubwa sasa ni kujua baada ya kufa unaenda wapi? Kuna uzima wa milele na mauti ya milele. Ukimwamini Yesu utaishi milele na usipomwamini Yesu utaenda katika mauti ya milele.

Tukilitambua hilo, Mungu atusaidie tupate kujua kwamba kuishi ni mara moja na baada ya kifo ni hukumu. Hakuna matengenezo ya maisha baada ya kufa.Tunapaswa kumpokea kumwamini na kumwishia Yesu. Ili maisha haya yanapokoma, tuwe na sehemu katika makao ambayo alipokuwa akiondoka duniani alisema kwamba anakwenda kuyaandaa. Pale alipo na wamwaminio ndipo watakapo kuwa. Ndiyo maana Yesu alisema yeye ndiye njia kweli na uzima mtu hatakwenda kwa Mungu ila kwa njia ya Yesu.

Mungu tusaidie sana na sisi tuliobaki duniani tuijue na kutembea katika njia yako kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo.
 
Pole Hamadi. Hapo naona ule msemo 'Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba' in action.

Ila cha kushangaza ni unafiki wa wanasiasa - huyu jamaa kumbe ana makazi za kudumu Bara (Dar) wakati CUF wanayoiongoza inapigania ZNZ kujitenga.
 
pole sana babaaa ndicho alicho kipanda mwenyezi mungu sasa niwakati wa mavuno yapaswa kushukuru
 
Pole Hamadi. Hapo naona ule msemo 'Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba' in action.

Ila cha kushangaza ni unafiki wa wanasiasa - huyu jamaa kumbe ana makazi za kudumu Bara (Dar) wakati CUF wanayoiongoza inapigania ZNZ kujitenga.

Nyerere alienda kuudai uhuru hukohuko kwa Wasungu, hivyo Hamadi kazidisha action kwa kuamua kudai uhuru akiwa nyumbani mwa mtawala pengine kelele zake zitasikika kuliko akiwa Pemba.
 
Mungu amfariji ndugu yetu aliyeachwa, watoto familia na marafiki wote. Ni jambo la huzuni sana. Kikubwa ni kukubali mpango wa Mungu na kuandaa maisha yetu maana hatujui siku wala saa. Tunahitaji kujua ipo siku nasi tutaondoka. Kikubwa sasa ni kujua baada ya kufa unaenda wapi? Kuna uzima wa milele na mauti ya milele. Ukimwamini Yesu utaishi milele na usipomwamini Yesu utaenda katika mauti ya milele.

Tukilitambua hilo, Mungu atusaidie tupate kujua kwamba kuishi ni mara moja na baada ya kifo ni hukumu. Hakuna matengenezo ya maisha baada ya kufa.Tunapaswa kumpokea kumwamini na kumwishia Yesu. Ili maisha haya yanapokoma, tuwe na sehemu katika makao ambayo alipokuwa akiondoka duniani alisema kwamba anakwenda kuyaandaa. Pale alipo na wamwaminio ndipo watakapo kuwa. Ndiyo maana Yesu alisema yeye ndiye njia kweli na uzima mtu hatakwenda kwa Mungu ila kwa njia ya Yesu.

Mungu tusaidie sana na sisi tuliobaki duniani tuijue na kutembea katika njia yako kwa kumwamini Bwana Yes Kristo.

Eeeeh Mungu, nami niwezeshe kutambua haya na kuishi hivyo, amin!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom